Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Upungufu wa dola ya Marekani katika maeneo mbalimbali unaanzisha mnyukano wa sarafu ya akiba kati ya dola na yuan. Pesa ya Yuan ya China ambayo ilikuwa inafanya kazi katika soko la biashara kati ya China, Australia na Japan sasa inakwenda kupanua wigo wake katika nchi za kiafrika na nchi nyingine duniani ambazo zinaguswa na uhaba wa Dola ya Mmarekani.
Thamani ya Dola ipo kwenye upande wa kufanya miamala, Telegraphic transfer (TT) kupitia mfumo wa SWIFT, sasa Mchina ataweza iwapo ataipiku swift na tayari baadhi ya mabenki hapa nchini Tanzania yameanza kutuma miamala kwenda China kwa pesa ya Yuan badala ya Dola, punde tutaiona miamala mingi ya pesa ya Yuan.
Hofu ya Dola kuyumba inakuja baada ya Bloomberg kuhitaja China kuongoza kuuza bidhaa kwa Dola za Kimarekani trillion 3.87 ukilinganisha na Marekani iliyouza bidhaa zenye thamani ya Dola za Kimarekani trillion 3.82 kwa wiki iliyopita ya mwezi February.
Mdororo wa kiuchumi, kushuka kwa uwezo wa kununua kwa Wamarekani, na uwezo huo kuongezeka kwa Wachina, kiwango cha pesa inayoingia na kutoka baina ya nchi hizo inaashiria kuanza kukomaa kwa pesa ya Yuan ya China na kufifia kwa Dola ya Mmarekani.
Hii inaturejesha kwenye njia ile ile iliyopita pesa ya Ugiriki Silver Drachma, Coin ya Warumi, Dinari ya Mwarabu na dhahabu ya Wabyzantini bila kusahau Silver coin ya Hispania na Pound ya Muingereza.
Ni dhahiri ili nchi iwe na uchumi mzuri na wenye tija kuna baadhi ya masuala ya kiuchumi yanapaswa kuzingatiwa ili mambo yawe stable, mfano kuna vitu vinaitwa Balance of Trade, Balance of Payment, Import na Export.
Kwa kugusia tu ili kuupata uchumi wenye tija ni lazima kuwe na Export (kuuza nje) kubwa kulinganisha na Import (kununua nje ya nchi) ili watengeneze faida kimantiki.
Sasa hapo kwenye Export ni procedure nzima ya kuuza zaidi nje kuliko kuingiza, sasa shida moja kama pesa yako ina nguvu sana, basi itafanya wateja wasije kununua kwako sababu wakija kununua na shilingi wakifika uko nje watapata pesa ndogo ya kununua bidhaa.
Ngoja nikupe mfano, Mtanzania anaenda kununua bidhaa China akifika, China anakuta rate Dola 1 sawa na Yuan 6.84 mahesabu yatakuwa hivi 10,000 ÷ 2380 *6.84 =28.7 ambayo ndio Yuan utakayotumia kufanya manunuzi yako ukiwa China.
Kama Yuan itakosa nguvu na kuwa Dola 1 sawa na Yuan 7 mahesabu yatakuwa hivi 10,000*2380*7=29.4, ndio Yuan utakazotumia kufanya manunuzi ukiwa China, utakuwa na ziada ya Yuan 0.7.
Sasa nitolee mfano wa Mzambia au Mkongo anayekuja na Dola Kariakoo, Tanzania kununua bidhaa akakuta rate Dola 1 sawa na shilingi 2380, akija na Dola 100 *2380=238,000 hizo ndizo Shilingi atakazotumia kufanya manunuzi akiwa Kariakoo, Tanzania,
Mzambia au Mkongo akija Kariakoo, Tanzania akakuta thamani ya Shilingi imeimarika Dola 1 sawa na shilingi 2300, mahesabu yatakuwa hivi; 100*2300=230,000 hizi ndizo Shilingi atakazotumia kufanya manunuzi akiwa Kariakoo, Tanzania.
Hivyo basi thamani ya pesa ya nchi ikiongezeka mgeni akija ndani ya hiyo nchi anapata pesa kidogo ya manunuzi, hivyo mteja ataenda kule thamani ya pesa ya nchi husika haijapanda thamani.
Mfano Marekani na China, kila mteja atapenda kwenda China maana akibadili pesa yake atapata pesa nyingi ya kufanya manunuzi, hii ni kutokakana na hela ya China (Chinese Yuan) kuwa na value ndogo uki compare na pesa yetu dhidi ya pesa kama Dola ya Marekani, lakin kwa benki zetu kutuma shilingi moja kwa moja nchini China, mfano unatuma 10,000 na rate ni 355.87 mahesabu yatakuwa hivi 10,000÷355.87=28.1.
Mwaka 1944 kwenye mkutano wa Breton Wood Conference, uliofanyika katika Hotel ya Mount Washington, ilijulikana kuwa Marekani ndio ilikuwa inamiliki hazina kubwa ya gold duniani. Marekani alikuwa na 2/3 ya dhahabu zote duniani, sifahamu kwa kipimo gani ikiwa sisi Tanzania tulikuwa na migodi ya dhahabu zaidi ya kumi haijaanza kuchimbwa.
Akalazimisha kuwa gold na US dollar zitumike kuipa thamani kila sarafu ya nchi iliyo duniani. Nchi za Ulaya hazikuwa vizuri kutokana na WWII, ilibidi tu wakubali ni USSR pekee ndiye aliyekataa huu mkataba, na hapo ndipo pia ilizaliwa IMF.
Hiki ni moja ya kitu kilichofanya Dola ya Marekani kuwa maarufu sana japokuwa huu mkataba ulivunjika mwaka 1970, ni kweli Marekani ni taifa linaloongoza kuexport bidhaa zao kuliko nchi yeyote duniani ikifuatiwa na China,l akini pia uchumi wa nchi nyingi duniani unaendeshwa na Marekani.
Nimalizie kwa kusema kuwa, wakati sisi tunawaza ujinga ujinga, Wachina walikuwa kazini wakitafuta mbinu yoyote ili kuidhibiti Dola na vijidola au pesa za madafu pamoja na hizi Covid na zile zinazotaka kuleta mgogoro wa vita kuu ya tatu.
Miaka ya nyuma China ilijikita kuozi Dollar ya Kimarekani bila kutoka nje na kufanya wafanyabiashara wengi kwenda na Dollar mpaka ikawa inashikilia pesa hiyo kwa kukopesha na mambo mengine ya kijamii.
Marekani ilipoona hivyo, ikataka kubadilisha series ya pesa na kuishusha thamani series iliyokuwa inatumika, ndipo China alitumia njia ya busara kuweka kwenye mzunguko, lakini kuna kipindi Dollar zilijaa China na zilikuwa hazitoki.
Mmarekani akaona hii si sawa, siku Mchina akiziachia zote basi Dollar itakosa thamani, sasa basi ni dhahiri Pesa ya Yuan itaanza kuvuka boda kutokana na kuyumba yumba kwa mzunguko wa Dollar unaotumika dunia nzima.
Yuan itatumika kwa raia wa China wote ndani na waliokuwa wageni wakiwemo China, ni dhahiri Yuan italinda mzunguko na thamani kubwa ya Yuan katika soko la kigeni.
Nikiishia hapa, mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publications;
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.