Peter Gasaya, Boss wa JATU apandishwa Mahakamani. Wale mliotapeliwa na JATU poleni

udanganyifu .... Umasikini wa mawazo na Ujinga ni janga linaloitafuna TZ, baadae atachiwa huru ka Mr Kuku na kundelea na maisha yake ka kawaida
 
Mbona huyo mkubwa tu.

Umemsahau Mr Kuku (Tariq Machibya) alipiga watu 17B akiwa 29yr pekee.

Alipokiri kosa zikataifishwa 5.4B zilizokuwa zimetulia tu kwenye account yake.

Wajinga ni fursa nene ukichekecha vizuri ubongo!
 
Hizi kampuni za upatu zina watu wakubwa nyuma yake, Wataanza hivi hivi baadae wanamfanya mmojawapo mbuzi wa kafara na hiyo ni mipango tu ili ionekane kuwa watu wameibiwa na serikali imeliona hilo.
JATU, Mr Kuku, Vanila village ni watu wazito Serikalini, Jiulize Mr Kuku yuko wapi? Alishafungwa jela? Tena ametoka na akawakolia waganga watoe tena ili aje alipe awalipe taratibu kinyume chake yeye hana hela zimechukuliwa na Serikali.
Mkitaka kujua hizi biashara zina watu wakubwa nyuma yake, fanyeni kitu kimoja tu, kagawaneni mali zote kuanzia majengo na vinginenvyo vamieni muone moto wa serikali, yaani hapa mali hizo zitalindwa kwa nguvu zote.
Wale wanaomdai Mr Kuku siku jotoeni ufahamu kavamieni shamba lake la kuku mbebe kuku wa kutosha kufidia deni muone nguvu ya mlevi.
 
Hii kitu hata Mimi nilitaka kuingia!!,
 
Kijana mzembe alitakiwa aondoke nchini kwenda kuishi ulaya, wenzie raia waki geni wakivuna pesa za wajinga wanaondoka
 
Kinachoniuma bado watu hawashtuki yan wa TZ ni kama tuko mazezeta vile. Wataibuka wengine na wengine na bado watu wataenda kuwekeza tu.

Elimu, Elimu Elimu+Exposure minus Africanacity
Mkuu mbona ukichunguza vizuri walio tapeliwa ni watu wenye elimu ya juu, kwasababu mwananchi wa chini kabisa hawaijui hii kampuni
 
Walikuwepo pale sabasaba kuhamasisha watu wanunue hisa..........
 
Ona kalivovaa mtu anaevaaga visuruali vya kipumbavu kama vya bwana JATU huwa namuona na yeye mpumbavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…