Peter Kibatala: Askofu Gwajima yupo mafichoni, mteja wangu hajakamatwa

Peter Kibatala: Askofu Gwajima yupo mafichoni, mteja wangu hajakamatwa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kanisa hilo mpaka sasa limezungushiwa utepe wa njano wenye maandishi meusi, likiwa chini ya ulinzi wa polisi na hakuna muumini anayeruhusiwa kusogea, tangu alfajiri ya kuamkia Juni 3, 2025.

Juni 2, 2025, Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa alitangaza kulifuta kanisa hilo kutokana na kukiuka Sheria ya Jumuiya Sura ya 337 kwa kile alichokieleza ni kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa nia ya kuichonganisha Serikali na wananchi.

1749105101183.png

Tangu kuzungushiwa utepe kanisa hilo na kuwa chini ya ulinzi wa polisi wenye silaha na gari ya maji ya kuwasha, waumini wanakusanyika upande wa pili wa barabara wakitaka kujua ni wapi alipo kiongozi huyo.

Soma zaidi Jumanne Muliro: Askofu Gwajima akitaka, akate rufaa (rufaa inakatwa kwa Waziri Bashungwa)

Akizungumza na Mwananchi Jumatano Juni 4, 2025 wakili wa Askofu Gwajima, Peter Kibatala amesema mbunge huyo yupo mahali salama.

"Mteja wangu (Askofu Gwajima) hashikiliwi (hajakamatwa), yuko wapi ni suala ambalo siwezi kulitolea maelezo kwa sababu mbalimbali.”

"Ambacho naweza kukithibitisha hadi muda huu (saa 7:15 mchana wa Juni 4, 2025) hashikiliwi, yupo salama, hajakamatwa," amesema Kibatala.

Amesema kuna mambo wanayoendelea kuyafanya na Askofu Gwajima kuhusiana na hatua kadhaa za kisheria baada ya hatua ya msajili.

"Kwa sasa itoshe kusema hashikiliwi, yupo salama," amesema.

Kushughulika na Polisi wanaolinda kanisa

Akizungumzia ulinzi unaoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi, makao makuu ya kanisa hilo eneo la Ubungo Kibo jijini Dar es Salaam, Kibatala amesema tayari wameanza taratibu za kisheria juu ya suala hilo.

"Hayo wanayoyafanya, wanafanya kwa misingi gani ya kisheria? kama polisi wanatekeleza kinachoitwa kufutwa kwa kanisa, hakuna kitu hicho," amesema wakili huyo.

Kibatala amesema kama taarifa ya kufungiwa kwa kanisa ni ile inayosambaa kwenye mtandao, basi kuna upungufu kisheria.

"Wao wamefuta kanisa linaitwa Glory of Christ Church, kanisa la mteja wangu (Askofu Gwajima) linaitwa Glory of Christ Tanzania Church, kuna changamoto za kisheria na kimantiki," amesema.

Amedai mteja wake, hajaambiwa chochote, wala hawajapewa barua na mtu yeyote kuhusu kufutwa kwa kanisa akidai utaratibu wa kisheria ni mteja wake kupewa barua, utaratibu ambao anadai haujafanyika huku akihoji polisi wanaolinda kanisa hilo wanafanya nini pale.

"Suala la Polisi kuwa pale tunalishughulikia kisheria, walioko pale wako pale kwa hicho kinachoitwa kufutiwa usajili, lakini ni kifaa kazi gani kilitumika kufuta usajili? ni hiyo barua inayosambaa kwenye mitandao au kitu kingine? Amehoji.

Amesema utaratibu wa kisheria kuhusu Polisi kulinda kanisa hilo umeshaanza kufanyika Dar es Salaam na Dodoma.

Chanzo: Mwananchi
 
Picha linaanza kapost clip yupo ndani ya kanisa na Maaskofu Saa Tano usiku.Mara Pap! Umeme Ukazimwa Mara Pap! Wahuni wamekamatwa Gwaji boy Hayupo kweli bado ni kijana aseee! Daah!😂😂🙌

#arushatvonline
1749113365128.jpg
 
Ukishajua itakusaidia nini? Leteni hoja za maana, au ndio story za vijiweni zinaendelea. Fanyeni kazi Watanzania fursa zipo kibao kama serikali yenu imeshindwa kuwapanga basi msubiri ufa mafara.
 
Ukishajua itakusaidia nini? Leteni hoja za maana, au ndio story za vijiweni zinaendelea. Fanyeni kazi Watanzania fursa zipo kibao kama seikali yenu imeshindwa kuwapanga basi msubiri ufa mafara.
Mbona kama makasiriko mkuu 😂
 
Gwaji boy alipenyezewa taarifa mapema akasepa usifikiri humo kwa wenye mamlaka hakuna anaeungana na jasusi la mbinguni

kama tu ndani ya selikali kuna wanaompa taarifa kimambi aje akoswe gwaji boy taarifa ya nini kinaendelea

Unaambiwa jasusi lilijirekodi eti nipo kanisani saa tano za usku tumezingilwa na polisi kumbe hakuna lilisepa mapema ndipo likaenda kujirekodi kwingine na na maaskofu yakwamba lilijiandaa mapema kwa hilo
 
Gwaji boy alipenyezewa taarifa mapema akasepa usifikiri humo kwa wenye mamlaka hakuna anaeungana na jasusi la mbinguni

kama tu ndani ya selikali kuna wanaompa taarifa kimambi aje akoswe gwaji boy taarifa ya nini kinaendelea

Unaambiwa jasusi lilijirekodi eti nipo kanisani saa tano za usku tumezingilwa na polisi kumbe hakuna lilisepa mapema ndipo likaenda kujirekodi kwingine na na maaskofu yakwamba lilijiandaa mapema kwa hilo
AISEEEE
 
Back
Top Bottom