Peter Kibatala: We need a Police to Police the Police

Peter Kibatala: We need a Police to Police the Police

Hiyo si sababu na msiendelee kukariri kwamba Polisi hawana elimu. Polisi 10k+ Kwa Sasa Wana Dr, Masters, bachelor, dip au form 6. Tatizo la ukosefu wa weledi nchini halihusiani na elimu zào. Bungeni kuna maprofesa lakini bado ni Bunge la ovyo kuliko la 1975.
🤝
 
Ww nenda kituo cha police chochote ukaone vichekesho na pia huzuni mtu anaonewa waziwazi yaan unakuta kiafande kibajiona tz ni ya baba yake ubafokewa fokewa tu km watoto nilisha fanya vurugu kituo kmoja baada ya kuona huu usenge wakaniweka ndani na kutishoa kunipa kesi wazano kibao tu nikawaambia nipeni hata ya mauaji walipo ona najiamini sana wakasanuka wakajua mm labda ni kitengo Kumbe 🤣🤣🤣
 
Naunga mkono hoja hii mkuu,KATIBA MPYA ndio kitu nchi inahitaji,umeongelea IPID hii imeshawahi sana kuandikwa humu,taasisi hii isipokuwepo police wetu wapo above the laws na wanajifanyia wanavyotaka maana wananchi wengi ni wapumbavu na waoga uliojaa uzuzu,mpumbavu mmoja pale kagera anatishia kuwapoteza watanzania wengine kisa utofauti wa kiitikadi,RPC pale anafwata mkia,IGP naye kimyaa,CJ yupo kimya,ukweli police wamemuua yule raia na police hapa ni suspects ilitakiwa nao wachunguzwe,Tanzania tumekua tunapata strong state persons na sio ICONS
Mkuu naunga hoja Kibatala na ya kwako. Pamoja na hayo nami napendekeza yafuatayo:

1. Muundo wa polisi ubadilishwe uwe ni wa kuhudumia wananchi. Badala ya kuwa police force ya mkoloni iwe police service ya kisasa.

2. Jeshi la polisi la sasa ligawanywe katika sehemu mbili zinazo jitegemea. Pawepo na huduma ya polisi na huduma ya upelelezi inayojitegemea kimuundo, kiuongozi, kimamlaka na kiutendaji

3. Polisi waboreshwe maslahi yao, angalau yakuweza kukimu/kumudu maisha ya sasa badala ya kutuma upolisi wao na bundiki kuendesha maisha yao. Huu ndio mzizi wa rushwa ndani ya polisi.

4. Askari polisi wote na vitengo vyao waishi kambini. Kambi zao ziboreshwe za kufaa kuishi binadamu. Ila askari upelelezi ndio waishi mtaani /changanyikeni/uraiani maana shughuli zao zinataka hivyo.

5. Katika mafunzo yao, mbali na mazoezi pawepo na somo la lazima la uelewa wa sheria, katiba, muongozo wa polisi na haki za raia kwa kila askari.

6. Kwa upande wa askari upelelezi pawepo na ukomo wa muda wa upelelezi, muda usizidi miezi 3, vinginevyo mahakamani ndio iongeze muda iwapo pana ulazima na usizidi miezi 3.

7. Katika zoezi lolote la ukamataji wa raia, raia yeyote wa jirani aruhusiwe kuchukua video ya tukio zima, video hiyo itumike kama sehemu ya ushahidi mahakamani ya mwenendo wa askari katika ukamataji na kusimamia haki ya raia.

9. Polisi wapewe vitendea kazi muhimu kama magari, pikipiki, fenicha, stationery na kadhalika kwa wakati ili kutimiza majukumu yao kwa ueledi bila ubabaishaji kama ilivyo sasa.

10. Ofisi, choo na mahabusi za polisi ziwe na hadhi nzuri kwa design, rangi na space. Hii itawamotivate askari kutenda haki. Majengo mengi ya polisi ukifika tu, unajua haki huipati! Nyingi ni mahabusu za kikoloni. Pia pawepo na vituo vya polisi kila ilipo ofisi ya serikali ya mtaa ili kurahisisha huduma.

11. Polisi iwatumikie raia wote kwa usawa. Jeshi la polisi lifuate sheria. Lisiwe jeshi la chama tawala lilojaa upendeleo. Ambalo kila askari ni mwanachama chama wa chama hiko na kusimamia ilani na sera za chama hicho. Lisiegemee upande wowote wa siasa.

Pawepo na clear separation.

12. Pawepo na muangalizi huru na maalum wa polisi ambaye kwa maoni yangu aweze kupokea malalamiko ya raia dhidi ya polisi, kuchunguza na kukarapia na kusimamisha askari yeyote kazi. Hii italeta nidhamu kwa askari dhidi ya raia.

13. Mwisho pawepo na utaratibu wa kila baada ya miaka 10, kupitia na kuoverhaul jeshi la polisi ili liweze kuendana na muda na mazingira ya dunia ya wakati huo.

Nawasilisha!
 
Polisi Tanzania ni aibu kubwa kabisa. Ina maana jeshi lote limejaa wajinga tu? Hakuna angalau watu wenye ku reason kwa kutumia logic? Je hakuna wenye ufahamu wa utawala wa kisheria?

Kuna mambo jeshi la polisi wanafanya yanakufanya ujiulize maswali mengi ya kukera.
Incopetence ni kubwa mno( japo si wote), na ukiangalia top leadership inachaguliwa kwasababu y maguvu, si wenye smart records ya kudeal na uncertain events.

Incopentrnce ni kubwa mno
 
Hiyo si sababu na msiendelee kukariri kwamba Polisi hawana elimu. Polisi 10k+ Kwa Sasa Wana Dr, Masters, bachelor, dip au form 6. Tatizo la ukosefu wa weledi nchini halihusiani na elimu zào. Bungeni kuna maprofesa lakini bado ni Bunge la ovyo kuliko la 1975.
Mmmh police gan mwenye Masters? PhD? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Aaah wee hapanaa.
 
Hiyo si sababu na msiendelee kukariri kwamba Polisi hawana elimu. Polisi 10k+ Kwa Sasa Wana Dr, Masters, bachelor, dip au form 6. Tatizo la ukosefu wa weledi nchini halihusiani na elimu zào. Bungeni kuna maprofesa lakini bado ni Bunge la ovyo kuliko la 1975.

Correct, shida ipo kwenye uongozi wa Kitaifa.
 
Ww nenda kituo cha police chochote ukaone vichekesho na pia huzuni mtu anaonewa waziwazi yaan unakuta kiafande kibajiona tz ni ya baba yake ubafokewa fokewa tu km watoto nilisha fanya vurugu kituo kmoja baada ya kuona huu usenge wakaniweka ndani na kutishoa kunipa kesi wazano kibao tu nikawaambia nipeni hata ya mauaji walipo ona najiamini sana wakasanuka wakajua mm labda ni kitengo Kumbe [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
NCHI HII KUBWA: Bora Taharuki kuliko Mauaji.

ANAANDIKA BABA ASKOFU BENSON BAGONZA

Sifa moja muhimu ya kiongozi ni kufanya maamuzi yenye maslahi mapana kwa jamii.

Nyumba inapoungua moto, ni bora kuokoa hata godoro moja kuliko kuua panya wanaokimbia moto unaounguza nyumba.

Mitandao ya kijamii usiku wa leo (25/4/2024) imejaa habari za Mwanaharakati wa haki za kijamii Malisa GJ na Mwanasiasa/Mwanaharakati Jacob Boniface kukamatwa na polisi kwa KUSABABISHA TAHARUKI wakati wanaripoti “mauaji” ya mtu mmoja aitwaye Mushi.

Kama ningelikuwa jeshi la polisi ningetafakari haya kabla ya kufanya maamuzi:

1. Nchi hii ni kubwa sana. Jeshi la polisi ni dogo kuliko uhalifu. Wanaojitolea kutoa taarifa za uhalifu ningewafanya marafiki kuliko maadui.

2. Ni kweli Mushi amekufa. Ningeshughulika na wauaji kuliko kushughulika na waliosababisha taharuki.

3. Ningejiuliza; taharuki imesababishwa na ripoti ya kifo au kifo chenyewe? Kifo kisicholeta taharuki si kifo kamili.

4. Malisa GJ ameisharipoti matukio mengi ya kihalifu ambayo jeshi la polisi ama halikujua au lingepata taabu sana kujua. Kwa hili la kifo cha Robert Mushi, Jeshi la polisi lingemzawadia nishani ya utumishi wa kujipendekeza kwa polisi kuliko kumkamata na kumpekua.

5. Badala ya kumpekua Malisa GJ na Boniface Jacob, ningewatumia na mitandao yao kutafuta na kujua gari linalodaiwa kumgonga marehemu Moshi.

6. Kwa kuwa nchi ni kubwa sana; ningetumia muda kuchunguza ndani na nje ya jeshi la polisi kuhusu uwezekano wa polisi vishoka wanaodaiwa kumkamata marehemu Robert Mushi kabla ya kifo chake!

7. Ningeazimia kuwalinda wanaojitolea kutoa taarifa za uhalifu kuliko wanaodaiwa kukosea katika kutoa taarifa za uhalifu ili kwa njia hiyo niongeze wigo wa watoa taarifa za uhalifu.

Lakini kwa kuwa mimi si Jeshi la polisi bali ni mtu ninayejifanya Askofu wakati hata uaskofu umenishinda, nabakia kutamani kuwa polisi huku nikijua kuna polisi wanatamani kuwa Askofu.

Natamani Jeshi la polisi liwaachie huru Malisa GJ na Boniface Jacob ili linufaike na harakati zao katika kukomesha uhalifu wa kidola na kiraia.
 
Andiko kuntu!
 
Yuko wapi kipigo Cha mbwa Koko? Kikokotoo kilimuacha salama au kilimpitia?
Yuko polisi mmoja amefanya kazi ya upolisi miaka nenda Rudi kuitetea serikali ya CCM. Alipostaafu mafao' aliyopewa hayatoshi hata kununua IST showroom. Ameshindwa kurudi kwao maana atajielezaje kwa mates wa umri wake.
Tufanye kazi tukijua Kuna maisha baada ya kazi.
Ni hayo tu huku nikiwaza kikokotoo na NHIF.
Kipigo cha mbwa Koko ni mlinzi wa kampuni ya gadworld
 
Murilo akishauriwa atakwambia UNANIJUA MIMI NANI ? Amejaa mabavu matupu na ukiritimba wa ccm

Polisi wetu, nadhani wanaamini kuwa polisi hakuhitaji kutumia akili ili maguvu tu. Ndiyo maana tuna matendo mengi ya hovyo yanayofanywa na jeshi la polisi.
 
Kipigo cha Mbwa Koko Afande Moroto baada ya kustaafu Polisi kwa sasa ni Security Manager Kampuni ya Tembo Nickel Ngara,ni Kampuni ya Kimataifa inayojishughulisha na Uchimbaji wa Madini ya Nickel Ngara,kwa kifupi analipwa Mshahara mkubwa kuliko aliokuwa analipwa Polisi
 
Back
Top Bottom