Naunga mkono hoja hii mkuu,KATIBA MPYA ndio kitu nchi inahitaji,umeongelea IPID hii imeshawahi sana kuandikwa humu,taasisi hii isipokuwepo police wetu wapo above the laws na wanajifanyia wanavyotaka maana wananchi wengi ni wapumbavu na waoga uliojaa uzuzu,mpumbavu mmoja pale kagera anatishia kuwapoteza watanzania wengine kisa utofauti wa kiitikadi,RPC pale anafwata mkia,IGP naye kimyaa,CJ yupo kimya,ukweli police wamemuua yule raia na police hapa ni suspects ilitakiwa nao wachunguzwe,Tanzania tumekua tunapata strong state persons na sio ICONS
Mkuu naunga hoja Kibatala na ya kwako. Pamoja na hayo nami napendekeza yafuatayo:
1. Muundo wa polisi ubadilishwe uwe ni wa kuhudumia wananchi. Badala ya kuwa police force ya mkoloni iwe police service ya kisasa.
2. Jeshi la polisi la sasa ligawanywe katika sehemu mbili zinazo jitegemea. Pawepo na huduma ya polisi na huduma ya upelelezi inayojitegemea kimuundo, kiuongozi, kimamlaka na kiutendaji
3. Polisi waboreshwe maslahi yao, angalau yakuweza kukimu/kumudu maisha ya sasa badala ya kutuma upolisi wao na bundiki kuendesha maisha yao. Huu ndio mzizi wa rushwa ndani ya polisi.
4. Askari polisi wote na vitengo vyao waishi kambini. Kambi zao ziboreshwe za kufaa kuishi binadamu. Ila askari upelelezi ndio waishi mtaani /changanyikeni/uraiani maana shughuli zao zinataka hivyo.
5. Katika mafunzo yao, mbali na mazoezi pawepo na somo la lazima la uelewa wa sheria, katiba, muongozo wa polisi na haki za raia kwa kila askari.
6. Kwa upande wa askari upelelezi pawepo na ukomo wa muda wa upelelezi, muda usizidi miezi 3, vinginevyo mahakamani ndio iongeze muda iwapo pana ulazima na usizidi miezi 3.
7. Katika zoezi lolote la ukamataji wa raia, raia yeyote wa jirani aruhusiwe kuchukua video ya tukio zima, video hiyo itumike kama sehemu ya ushahidi mahakamani ya mwenendo wa askari katika ukamataji na kusimamia haki ya raia.
9. Polisi wapewe vitendea kazi muhimu kama magari, pikipiki, fenicha, stationery na kadhalika kwa wakati ili kutimiza majukumu yao kwa ueledi bila ubabaishaji kama ilivyo sasa.
10. Ofisi, choo na mahabusi za polisi ziwe na hadhi nzuri kwa design, rangi na space. Hii itawamotivate askari kutenda haki. Majengo mengi ya polisi ukifika tu, unajua haki huipati! Nyingi ni mahabusu za kikoloni. Pia pawepo na vituo vya polisi kila ilipo ofisi ya serikali ya mtaa ili kurahisisha huduma.
11. Polisi iwatumikie raia wote kwa usawa. Jeshi la polisi lifuate sheria. Lisiwe jeshi la chama tawala lilojaa upendeleo. Ambalo kila askari ni mwanachama chama wa chama hiko na kusimamia ilani na sera za chama hicho. Lisiegemee upande wowote wa siasa.
Pawepo na clear separation.
12. Pawepo na muangalizi huru na maalum wa polisi ambaye kwa maoni yangu aweze kupokea malalamiko ya raia dhidi ya polisi, kuchunguza na kukarapia na kusimamisha askari yeyote kazi. Hii italeta nidhamu kwa askari dhidi ya raia.
13. Mwisho pawepo na utaratibu wa kila baada ya miaka 10, kupitia na kuoverhaul jeshi la polisi ili liweze kuendana na muda na mazingira ya dunia ya wakati huo.
Nawasilisha!