Peter Madeleka: Kutishia watu kuwapeleka Magereza ili wateseke ni Ushamba na ulimbukeni. Kuuza bandari za Watanganyika ni ufisadi

Wakili huyu kwanini anaandamwa sana na serikali hii? Ana siri gani anazozijua wakihofu kuendelea kuzilipua hadharani hadi wakeshe wakifikiria namna ya kumrejesha gerezani? Kwanini wananchi wasiamini serikali hii imejaa uonevu kwa kutumia kichaka cha demokrasia ambayo ni garasha tupu?

Serikali acheni kumtesa wakili huyu kutokana na madhaifu yenu na watu wenu
 
Hii imeenda!
 
Yaani siku hizi ni kama awamu ya magufuli tu.

Makosa na maovu wanafanya wao ula kuyaficha wanatesa watu bure
 
I don't know why but huyu jamaa huwa nahisi bado ni mtu wa system.... Nashangaa wapinzani wanaji attach naye sana, he might be the mole in the opposition. Maana aliminywa maslahi yake akiwa kwenye mfumo akakosana nao so simply akirudishiwa maslahi yake anaweza kuplay double agent.

We should be very careful na Hawa moles wa CCM.
 
Kwa hili la Bandari wauzaji wameshindwa kupambana kwa HOJA na hii inatokana na unanganyifu mkubwa waliofanya ktk kuficha huu uovu
Hakuna anayeweza kuuza bandari ni uelewa wetu kuwa mdogo na kuwasikiliza sana wanaharakati wenye kupotosha jamii wakiwa na malengo maalum.

Bandari inakodishwa, hii ya Dar inakwenda kuwa na wapangaji wawili DPW na mwingine wa magati namba nane mpaka namba kumi na moja.

Ile ya Tanga inakwenda kuwa na mwendeshaji mmoja, ile ya Bagamoyo inakwenda kuwa na mwendeshaji mwingine.

Haya ni masuala ya kiuchumi yenye kuhitaji mtu kuyatazama kiuchumi, mtu tu layman mwenye uelewa mdogo wa masuala nyeti hawezi kuelewa nini haswa kinachotafutwa.

Tunatoka katika mfumo wa mmiliki wa bandari kuendelea kumiliki yeye kama yeye tunaingia katika mfumo wa Land lord Port ambao mwendeshaji mkuu TPA anakuwa na wapangaji wengine ili kuongeza ufanisi na kurahisisha mzigo mwingi sana uliopo ndani ya Tanzania na nchi zinazotuzunguka kuweza kuyafikia mataifa ya nje haraka.

Kuna tani zaidi ya milioni 30 za mizigo mbalimbali inayotakiwa itoke huko bara na kwenda nje ya nchi, huo ni mzigo mwingi sana na kwa aina ya uendeshaji wa kizamani wa bandari tulionao hakuna nafasi ya kitaifa kuweza kuinuka kiuchumi.

Haya ni masuala ya kiuchumi yenye kutaka ufafanuzi wa kina wa kiuchumi, huu sio wakati wa kufikiria kizamani halafu matokeo ya ufikiriaji huo yawe na mashiko kwenye maisha ya kisasa.
 
Hata hao ambao hujawaweka kwenye kundi la moles ni watumishi wa hatari wa mfumo uliopo, kwa kifupi usimuamini mwanasiasa yoyote yule.

Muamini mama yako mzazi pekee, mimba yako ilitungiwa tumboni mwake na ukakua kwa miezi tisa humo ndani.
 
Safari inazidi kuwa ngumu
Usimsingizie JPM, hawa waliopo ndio walikuwa wakitenda kwa nia ya kumchafua kwa kuvizia akitamkacho mdomoni. Viongozi waliopo sasa ni bingwa sana wa kutenda uovu kwa kuvizia mbaya wao kasema nini na kuitumia kauli hiyo kutekeleza ili aonekane ni yeye kumbe sivyo.

Kama hauamini subiri watakavyomgeuka aliyekalia kiti cha dhahabu kwa sasa na hatapata fursa ya kuhoji kwanini imetokea hivyo!!!
 
Nyani haoni kundule
 
Ulivyompuuzi unadhania bandari inauzwa kama mchele sokoni.
 
Alikuwa ni askari mwenzao kabla hajawa mtakatifu
 
Acheni uongo? Kama kasingiziwa kwanini sikusikia hao waliotekeleza uhalifu wamekamatwa?? Yaani mtu amuue mwanao alafu asingizie baba yake ndio umemuua then na wewe ukae kimya tu kisa "umesingiziwa"? Si lazima utatafuta aliyefanya hicho kitendo Ili ujisafishe!!

Ukikaa kimya means umekubaliana na shutuma so huwezi kwepa lawama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…