Pre GE2025 Peter Msigwa: Nimemtuhumu Mwenyekiti wa Chama, sijamtuhumu Mbowe

Pre GE2025 Peter Msigwa: Nimemtuhumu Mwenyekiti wa Chama, sijamtuhumu Mbowe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Bilion 5 zimeshamvuruga, mara yuko tayari kupambana mahakamani, mara ooh Haya ni mambo ya kisiasa hapo anataka kuninyamazisha, mara oooh sijamtaja Mbowe nimemtaja mwenyekiti
Amekwishachanganyikiwa huyu. Hapa ndipo CCM itajua imemwokota mtu wa namna gani. Naona na yeye anajibrand kikamilifu kwenye ile sifa kuu ya wanaCM, kwa kadiri ya matokeo ya utafiti ule wa TWAWEZA, "CCM inapendwa zaidi na wajinga". Anataka usitofautiane na wenyeji wake kikamilifu.
 
Kweli CCM imekwishamwondoa akili. Yaani kwa kusema hivyo anaona amekwishatoa utetezi wa kumwondoa kwenye kesi?
Kwa hiyo nanyi bado mnamuamini Mbowe? Hivi pesa za Join the chain zipo wapi?????
 
Tatizo la mchungaji Msigwa ni Elimu ndogo

Sasa Ndio atamjua Mbowe na marafiki zake wa Upendo Kwaya Kijitonyama 😂😂😂😂😂
Acha vimaneno vyako vya uongo uongo hapa wewe. Mbowe na mchungaji peter Msigwa ni nani mwenye Elimu ndogo? Unaifahamu Elimu ya Mbowe??
 
Kwa hiyo nanyi bado mnamuamini Mbowe? Hivi pesa za Join the chain zipo wapi?????
Hizo pesa zinazchangwa na wananchi kwaajili ya shughuli za CHADEMA, ulitaka wakuletee wewe ndiyo umwamini Mbowe? Kama una ushahidi kuwa pesa wanazochanga wananchi kwaajili ya shughuli za CHADEMA, zinaingia kwenye account ya Mbowe au zimranzisha Mbowe Foundation, mwombe Msigwa ukawe shahidi wake muhimu huko mahakamani ili uokoe michango ya wananchi.
 
Mbowe alikuwa Benki Kuu ya Nchi kama Mwigullu Nchemba na Vicky Kamata usimchukulie poa

Nyie Watoto wa vijijini hamjui lolote sawa na huyo Mkinga mchungaji wenu 😂😂😂
Hata walinzi tu wapo Benki kuu.kwahiyo acha ulimbukeni wako hapa wewe.
 
Kuepusha shari Msigwa awahi mapema mnoo kumuomba radhi Mbowe ama sivyo atafirisiwa vibaya. Mdomo wake utamponza.
 
Hizo pesa zinazchangwa na wananchi kwaajili ya shughuli za CHADEMA, ulitaka wakuletee wewe ndiyo umwamini Mbowe? Kama una ushahidi kuwa pesa wanazochanga wananchi kwaajili ya shughuli za CHADEMA, zinaingia kwenye account ya Mbowe au zimranzisha Mbowe Foundation, mwombe Msigwa ukawe shahidi wake muhimu huko mahakamani ili uokoe michango ya wananchi.
Lini mmewapa mrejesho wachangiaji juu ya kiasi kilichopatikana na matumizi yake? Hizo pesa za Join the chain imekuwaje hata makamu mwenyekiti lissu naye hajuwi chochote juu ya kiasi kilichopatikana wala matumizi yake?

Wewe akili yako huwa ni ndogo sana ndio maana majibu yako ni ya kitoto sana na yaliyokosa mashiko. Ndio maana huwa nakwambia kuwa hoja kubwa na usiwe unazikurupukia.uwe unasubiri hoja ndogo ndogo ndio ujadili.
 
Mwashambwa hata kama ugumu wa maisha umekufanya uwe hivyo jlivyo, lakini ishia huko huko kwenye upuuzi uliouchagua. Usimwingize Mungu mwenye mamlaka kuu kwenye upuuzi huu, unajitengenezea laana ambayo hutakuja kuijua chanzo chake. Tamaa ya msigwa usiishikamanishe na Mungu wala Malaika wake au chochote kilichopo kwenye ufalme wa mbingu. Yachukue maneno haya kwa uzito wa pekee.
 
Hata walinzi tu wapo Benki kuu.kwahiyo acha ulimbukeni wako hapa wewe.
Unadhani Mlinzi wa Benki Kuu ya Nchi wanajibebea tu Wasafwa mnaojitangaza kwa namba zenu za Simu mitandaoni? 😂😂😂

Wewe endelea kuwapikia Chai Wanyakyusa akina Tulia na Kasesera 😂😂😂😂😂

Siasa Siyo uadui 🌹
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hayo ni maneno ya Mtumishi wa Mungu Mheshimiwa Mchungaji peter Msigwa kada wa CCM kutokea mkoani Iringa na mbunge wa zamani wa Jimbo la Iringa Mjini.

Ambapo amesema ya kuwa yeye amemtuhumu Mwenyekiti wa chama na siyo kumtuhumu Mbowe.
View attachment 3089039

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Freeman Mbowe amtaka Mchungaji Peter Msigwa kumuomba radhi kwenye Magazeti na kulipa fidia ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumkashifu na kumchafua jina

CCM wamfukuze Msigwa haraka sana .
Ni pandikizi la Kambi moja ndani ya Chadema. Hiyo kambi ikifanikiwa ,Msigwa atarudi Chadema . Ni kama ilivyokuwa Kwa Nyarandu na Chadema.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hayo ni maneno ya Mtumishi wa Mungu Mheshimiwa Mchungaji peter Msigwa kada wa CCM kutokea mkoani Iringa na mbunge wa zamani wa Jimbo la Iringa Mjini.

Ambapo amesema ya kuwa yeye amemtuhumu Mwenyekiti wa chama na siyo kumtuhumu Mbowe.
View attachment 3089039

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Freeman Mbowe amtaka Mchungaji Peter Msigwa kumuomba radhi kwenye Magazeti na kulipa fidia ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumkashifu na kumchafua jina
Anzeni kumchangia tu
 
Back
Top Bottom