PETER SHALULILE rasmi ni mwananchi Yanga. Asante GSM kwa kuendelea kuonyesha upendo

PETER SHALULILE rasmi ni mwananchi Yanga. Asante GSM kwa kuendelea kuonyesha upendo

Peter ana uwezo wa kufunga ataisaidia Yanga huko Klabu Bingwa jamaa anapambana kweli kama ni kweli ni jambo jema aje awavushe makundi hata hivyo mwaka huu Al Ahly anaepangwa kundi moja kashuka chini huko..
 
Maisha haya,alikotoka hakupewa nafasi kwenye mechi muhimu za kimataifa msimu uliopita halafu waliomsajili sasa hivi wanaamini atawasaidia kwenye mechi hizo.😀

Hapo imesajiliwa historia zaidi.
 
Wakati mwingine tuache ushabiki usio na maana. Kwa Shalulile Yanga imesajili mtu na nusu. Siku hizi washambuliaji wazuri wa kati wamekuwa adimu sana. Na kitu kizuri kwa Shalulile anakuja akiwa tayari anajulikana uwezo wake sio mchezaji yule wa kusikilizia huku mashabiki wanasema apewe muda. Pia anaenda kuongeza uzoefu, kasi na jicho la goli kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga.

Ni mtizamo tu.
 
ASANTE GSM, ASANTE BILIONEA! 💚💛

Straika bora Afrika, Peter Shalulile, sasa ni mali ya Wananchi.

Nguvu mpya safu ya ushambuliaji. Karibu nyumbani, Shalulile! 🔥⚽
============
Yanga SC imemtambulisha rasmi straika wa kimataifa wa Namibia, Peter Shalulile, kuwa mchezaji mpya wa klabu hiyo kuelekea msimu wa 2026/27.

Shalulile anajiunga na Yanga akitokea klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, ambako ameandika historia kama mmoja wa washambuliaji bora kuwahi kucheza katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini. Katika kipindi chake cha miaka sita akiwa Sundowns, alicheza mechi 172 katika mashindano yote na kufunga mabao 92, huku akichangia timu hiyo kutwaa mataji mengi ya ndani na ya kimataifa.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alitwaa tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini msimu wa 2019/20, kabla ya kuendelea kung'ara akiwa Mamelodi Sundowns kwa kutwaa mataji matano ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL), Kombe la Ligi ya Afrika (AFL) na Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League)

nkimcheki veteran Mayele anavyokiwasha ligi ya. mabingwa, nkichungulia uhaba wa wafungaji afrika, nkiwaangalia waarabu mfano Al Ahly walivyojaza wahenga na wanavyosumbua ligi ya mabingwa, nikirudi kwa chama langu Chelsea kumtaka Welbeck!

Najipiga kifua kwamba huyu bwa mdogo Shalulile atafunga sana ligi ya mabingwa✍️✍️✍️👏
 
Maisha haya,alikotoka hakupewa nafasi kwenye mechi muhimu za kimataifa msimu uliopita halafu waliomsajili sasa hivi wanaamini atawasaidia kwenye mechi hizo.😀

Hapo imesajiliwa historia zaidi.
Bush lawyer kwenye moja na mbili. Kwa akili hizi usingemsajili Jamie Vardy, Mo Salah, Pirlo..
 
Bush lawyer kwenye moja na mbili. Kwa akili hizi usingemsajili Jamie Vardy, Mo Salah, Pirlo..
Nisingemsajili? Hueleweki,uliowataja walisajiliwa wakiwa wazee walio-flop kwenye team zao kwa lengo la kusaidia kimataifa?

NB:Kabla hujamlinganisha Shelulile na hao ni kwamba hata recent call ups za national team hajaitwa.
 
Peter ana uwezo wa kufunga ataisaidia Yanga huko Klabu Bingwa jamaa anapambana kweli kama ni kweli ni jambo jema aje awavushe makundi hata hivyo mwaka huu Al Ahly anaepangwa kundi moja kashuka chini huko..
wale watoto wa Azania sekondari walikuwa wanamuongelea Shalulile sasa watamuona Lupaso live
 
Shalulile keshapitwa na wakati; hakuweza kuifunga Yanga wakati akiwa na Mamelodi, je ataweza kuifunga Mamelodi akiwa na Yanga?
Unaweza kuwa na hoja, ila mpira unabadilika,
Ulitegemea kuiona Al Ahly Akicheza CAF CC kwa zama hizi?

Shalulile kwa league hii atawaka sana.
 
Back
Top Bottom