siku hizi pia kuna masters nyingi za voda fasta ambazo walizichukua watumishi wa umma ili waweze kupandishwa vyeo.ndo maana kwa sasa kuna wimbi kubwa la viongozi wa taasisi za umma ambao hawana maadili ya kazi.hizi masters zilipewa majina ya executive course ambapo unajisomea nyumbani halafu unaenda kufanya mtihani.je wewe mtumishi wa umma huo muda wa kujisomea nyumbani utaupata wapi?kwanza ukitoka kazini umechoka na ukirudi nyumbani unakutana na watoto hapa kuna kujisomea.waafrika tulilogwa tangu dunia inaanza.
Mimi PhD ya Jafo ni Mungu tu anisamehe.
Hawa watu walikuwa mawaziri enzi ya Magufuli, Magufuli yule aliyetaka muda wote watu wafanye kazi. Walipata wapi muda wa kufanyia kazi hizo PhD?
Elimu za watu waliosoma baada ya kuwa viongozi zina mashaka
makubwa sana.