PhD ya Musukuma yazua gumzo, Chuo kilichomtunuku hakitambuliki

PhD ya Musukuma yazua gumzo, Chuo kilichomtunuku hakitambuliki

Mbona Mh.kikwete anatumia hiyo Dr popote na hata Marehemu Dr Mengi naye ilikuwa inatumika pote
Ikitumika unavyosema wewe basi itakuwa haina maana sasa.!
Mwalimu Nyerere alikuwa na shahada za heshima zaidi ya 20+ lakini hakuwahi kuitumia hiyo 'ante'.... Rais Obama alikuwa nazo zaidi ya 10+.. hakuwahi kuitumia hiyo 'ante'..
Wao hawatumii isipokuwa magazeti na vyombo vingine vya habari vinatumia pasipo kuelewa..
 
Karibu yote uliyosema ni kweli....

Nilisema hivyo kwa sababu jamii yetu inathamini wenye pesa. Hata uwe profesa uliyeandika mavitabu 100 na unajulikana kimataifa kama huna pesa we ni takataka tu mbele ya jamii. Ndiyo maana akina Musukuma na Kishimba kila siku kutukana maprofesa kwa vile wana pesa japo hawajasoma!

Sijui kama Musukuma anatumia pesa zake kuwakanyaga wengine ila nijuavyo mimi ni mtu mwema na anayejitolea sana jimboni mwake...
Msukuma ni mtanzania mwenzetu ila amepotoka sana kuhusu swala la elimu kwake yeye anahisi kuwa na pesa ndio kuwa na akili nyingi. Siwezi kumlaumu coz psychologically an entertain defense mechanism ili aweze kusurve bungeni ambako kuna wasomi wengi. Asichokijua Mganga wa kienyeji king msukuma kuwa elimu ni mwanga wa jamii ni chungu kinachopika wataalamu wa fani mbalimbali ambao ni treasures of the nation. Mfano madaktari, walimu, marubani, wanamahesabu na wengine wengi. Ukisikiliza mijadala yake bungeni anavyo underrate wasomi utagundua tatizo lake kuwa ni "shule hamna kichwani'' ana attacks watu badala ya mifumo yenyewe ya elimu. Kuwa ni mbunge kama msukuma kwenye chombo cha kutunga sheria ni janga la kitaifa coz hawezi kufanya analysis badala yake atapiga majungu tu kama tulivyomzoea. Tunaomba wanazuoni wenye nia njema na taifa letu wapaze sauti zao za hekima kukemea kuwa na wabunge aina ya msukuma ni hatari kwa maendeleo ya elimu na taifa kwa ujumla
 
Nilipokuwa sekondari Kuna mwandishi mmoja wa vitabu mwenye jina la kihaya nimemsahau alileta TAFRANI kwa baadhi ya VIONGOZI kwa kuwataja kuwa si madaktari wa kweli.......

Kuhusu hizi "HONORIS CAUSA" aliyopatiwa mh.Musukuma anaweza kupewa yeyote mwenye MCHANGO katika jamii ...hoja tu ni kutoka CHUO KIKUU GANI CHENYE ITHIBATI ZILIZOSIMAMA .....

Hata Nassib Abdul "alias" Diamond Platinumz naye ana SHAHADA ya heshima kutoka UDSM ........
Hahahahahah
 
Msukuma ni mtanzania mwenzetu ila amepotoka sana kuhusu swala la elimu kwake yeye anahisi kuwa na pesa ndio kuwa na akili nyingi. Siwezi kumlaumu coz psychologically an entertain defense mechanism ili aweze kusurve bungeni ambako kuna wasomi wengi. Asichokijua Mganga wa kienyeji king msukuma kuwa elimu ni mwanga wa jamii ni chungu kinachopika wataalamu wa fani mbalimbali ambao ni treasures of the nation. Mfano madaktari, walimu, marubani, wanamahesabu na wengine wengi. Ukisikiliza mijadala yake bungeni anavyo underrate wasomi utagundua tatizo lake kuwa ni "shule hamna kichwani'' ana attacks watu badala ya mifumo yenyewe ya elimu. Kuwa ni mbunge kama msukuma kwenye chombo cha kutunga sheria ni janga la kitaifa coz hawezi kufanya analysis badala yake atapiga majungu tu kama tulivyomzoea. Tunaomba wanazuoni wenye nia njema na taifa letu wapaze sauti zao za hekima kukemea kuwa na wabunge aina ya msukuma ni hatari kwa maendeleo ya elimu na taifa kwa ujumla
Kutoka kwenye Mwanasheria wa mchongo hadi mwanazuoni wa mchongo😅
 
ANAANDIKA BABA ASKOFU BAGONZA[emoji116][emoji116][emoji116]

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sasa nimejua. Siku za karibuni Kuna mtu aliniita kutokea Arusha akaniambia jina langu limependekezwa ili nipewe udaktari wa heshima kwa sababu (akataja nyingi). Kisha akasema zinatakiwa dola 500 haraka sana na deadline ni siku ya pili yake. Akataja chuo hikihiki.

Nikamwambia hiyo hela Sina. Akasema basi leta dola 210 kwa punguzo maalum.

Nikamwambia kwa Sasa Kuna vyuo vikuu 3 humu duniani vinaniomba nipokee udaktari wa heshima kutoka kwao lakini itaambatana na cheki ya dola elfu kumi kwangu. Nikamwambia bado nasita kwa sababu walizonitajia kuwa ninazo bado nina mashaka nazo kama ninazo kweli. Tukaachana hivo.

Kumbe wakapatikana kina Msukuma?!
Bagonza umemaliza kabisa Hawa matapeli
 
Kama Msukuma atapewahio PhD ya mti mti mie siwezi enda poteza mda kuandaa machapisho! Wacha niandae dollar 500 tu😅!!!

Kwa hali hii atakayesema pesa sio kila kitu ntamzabua makofi akaseme kituo chochote cha polisi!
Hawa watu wanashusha sn thamani ya elimu yetu
 
Pengine huyu Msukuma, hatimaye amejionyesha kuupenda usomi baada ya kuukandia hadharani kwa miaka mingi.

Sasa ametafuta shortcut, udaktari wa heshima.

Huo siyo usomi, short and simple.

Msukuma hajui, kuwa hajui, na kutokujua kwake kumemletea ujinga zaidi kama vile watoto wa chekechea walivyokuwa wana vaa majoho hadi kupelekea utaratibu huo kupigwa marufuku.

Walio karibu na Msukuma wamwambie, hajachelewa, bado kijana.
Akakinoe kichwa kwa elimu ya awali na juu sekondari, ahenyee shahada ya kwanza na ya uzamili na baadaye anoe kichwa na kuwaridhisha walio katika uzamivu, kuwa anastahili uzamivu.

Kwa majoho aliyovaa kama mbeba maboga, hajamridhisha msomi yeyote ustahili wake.
Joho la kuchonga aka mti mti😅
 
Back
Top Bottom