masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,207
- 13,839
Katika enzi hizi ambazo hata kina Msukuma wanapenda kujiita ni Madaktari wa Falsafa, na hili la mawaziri Jafo na Biteko kutunukiwa na UDOM, Udaktari wa Falsafa, kuna neno.
Prof Mark Mwandosya, msomi wa Udaktari wa Falsafa, mwalimu wa siku nyingi Co Kikuu Dsm na mwandishi wa Research Papers zinazotambulika kimataifa, ameuliza swali la msingi kabisa.
Ameuliza hivi, inawezekana kweli?
Mbunge mwenye shughuli nyingi, Waziri mwenye shghuli nyingi zaidi, kusoma na kuandika Research papers zinazotambulika kimataifa au kitaifa tu, na akatimiza matakwa ya kutunukiwa Udaktari wa Falsafa(PhD)?
Kawaida, PhD hutolewa kwa researcher ambaye anafanya shughuli hiyo si chini ya miaka minne!
Kazi kwako UDOM, kwa kugawa PhD kama peremende!