Philip Mangula ang'atuka nafasi ya Umakamu Mwenyekiti CCM Taifa. Abdulrahman Kinana apendekezwa na Halmashauri Kuu kuchukua nafasi yake

Philip Mangula ang'atuka nafasi ya Umakamu Mwenyekiti CCM Taifa. Abdulrahman Kinana apendekezwa na Halmashauri Kuu kuchukua nafasi yake

Kwa kuingia kwa hili genge, nadhani haitakuwa rahisi tena kuwang'oa unless yatokee mapinduzi kama ya Arab spring.

Mama Sa100 nae ajiandae kumuachia Maembe
 
Mangula ameachia nafasi ya umakamu mwenyekiti CCM, kaona isiwe tabu.

Ila hii Ni Mara ya Pili mzee anawekwa pembeni, sijajua ana tatizo gani na wenzio huko.

Nafasi imechukuliwa na Kinana

Membe karudishwa CCM

===

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula leo Alhamisi Machi 31, 2022 amewasilisha katika Halmashauri Kuu ya CCM barua ya kuachia nafasi hiyo.

Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM kimependekeza jina la Katibu Mkuu wa zamani Abdulrahman Kinana kuteuliwa kupigiwa kura za kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Bara ambapo atachukua nafasi ya Philip Mangula.

Kikao hicho kimefanyika leo 31 Machi 2022 Jijini Dodoma.

Pia soma;

1). Nashauri Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula ang'atuke na akabidhi mikoba kwa Abdulrahman Kinana

2). Ukatibu Mkuu CCM: Nani anafaa kuchukua nafasi ya Daniel Chongolo? Kinana ndani

View attachment 2170662
Huyu huyu Kinana na tuhuma zote hizo,kwani watu wengine safi hakuna?Watanzania bwana,dah!Huku Tony Blair mshauri,kazi kweli kweli.
 
Mimi ni mwana CCM na kama Mwl. Nyerere aliwahi kusema hajui chama chake kinafanya nini wakati ule. Nami leo sijui CCM ya leo inafanya nini. Kinachofuata huko mbele sio kizuri kabisa!
 
Huyu mzee akiomba kustaafu kwa muda tokea Magufuli ashike usukani, akakataliwa. Amesikika akisema wanangu na wajukuu wananitaka ni staafu. Sidhani kama kalazimishwa, hali yake ya kiaafya nayo inampa taabu tokea alishwe sumu na akina polepole na Bashiru
 
Mimi sikuwa na mrija wowote ila najua kuwa alikuwa kiongozi muovu. Alikata mirija ya aliowachukia, na yeye na genge lake la akina Makonda walikuwa wanaingiza macontainer yao watakavyo bila kulipa kodi.
Ndio nakwambia kama Jiwe asingekuwa anakata mirija ya watu basi usiongeona kelele za watu kuona Jiwe ni muovu, hayo ya yeye na Makonda watu hawana uchungu nayo kama asingekata mirija.
 
Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM kimependekeza jina la Katibu Mkuu wa zamani Abdulrahman Kinana kuteuliwa kupigiwa kura za kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Bara ambapo atachukua nafasi ya Philip Mangula. Kikao hicho kimefanyika leo 31 Machi 2022 Jijini Dodoma.
Mama ushungi ajue 2025 hana nafasi tena kea hiyo safu
 
Sasa Chadema huu ndo muda wenu wa kushine kama mtakuwa na akili. Nendeni kwa wananchi mjijenge. Maana ukweli sasa hii iliyopo ni serikali ya kufavor matajiri ambao ni minority hapa Tanzania.
I wish wangekusikiliza
 
Unajua watu wa ccm huwa nawashangaa, 2015 walisema ili kunusuru chama ilibidi wampitishe jiwe. Bila hivyo maji yalikua ya shingo
Sasa hivi wanasema Bora tukirudishe kwa wenyewe, ambao walikiri 2015 wangeshindwa.

Ila CCM inapaswa kufa kifo matata sana
Tatizo nani wa kukiua. Si unaona Mwenyekiti baada ya kutoka rumande hata kudai katiba amesahau
 
Mangula ameachia nafasi ya umakamu mwenyekiti CCM, kaona isiwe tabu.

Ila hii Ni Mara ya Pili mzee anawekwa pembeni, sijajua ana tatizo gani na wenzio huko.

Nafasi imechukuliwa na Kinana

Membe karudishwa CCM

===

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula leo Alhamisi Machi 31, 2022 amewasilisha katika Halmashauri Kuu ya CCM barua ya kuachia nafasi hiyo.

Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM kimependekeza jina la Katibu Mkuu wa zamani Abdulrahman Kinana kuteuliwa kupigiwa kura za kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Bara ambapo atachukua nafasi ya Philip Mangula.

Kikao hicho kimefanyika leo 31 Machi 2022 Jijini Dodoma.

Pia soma;

1). Nashauri Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula ang'atuke na akabidhi mikoba kwa Abdulrahman Kinana

2). Ukatibu Mkuu CCM: Nani anafaa kuchukua nafasi ya Daniel Chongolo? Kinana ndani

View attachment 2170662
Muda wake umefika
 
Siasa za bongo ni ngumu kumeza hatari sana. Likianguka kundi hili ni nafuu ya lile
 
Maoni yake kuhusu ujenzi wa kifisadi wa bandari ya bagamoyo uliwaudhi mafisadi
 
Back
Top Bottom