Philip Mangula ang'atuka nafasi ya Umakamu Mwenyekiti CCM Taifa. Abdulrahman Kinana apendekezwa na Halmashauri Kuu kuchukua nafasi yake

Philip Mangula ang'atuka nafasi ya Umakamu Mwenyekiti CCM Taifa. Abdulrahman Kinana apendekezwa na Halmashauri Kuu kuchukua nafasi yake

Ally Happy inabidi afute Ile kauli yake kabla ya upanga....
 
FPMUyTuXoAE9IHO.jpeg
 
Nadhani umri ndio sababu kuu....

Kuna kitu hakiko sawa! Katika hali ya kawaida, kiongozi hawezi (na hatakuwa na sababu ya) kujiuzulu mwaka wa uchaguzi. Kama aliweza kuhudumu kwa miaka yote hiyo, asingeshindwa kumalizia hii miezi michache iliyobaki kabla ya uchaguzi.
 
Mangula ameachia nafasi ya umakamu mwenyekiti CCM, kaona isiwe tabu.

Ila hii Ni Mara ya Pili mzee anawekwa pembeni, sijajua ana tatizo gani na wenzio huko.

Nafasi imechukuliwa na Kinana

Membe karudishwa CCM

===

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula leo Alhamisi Machi 31, 2022 amewasilisha katika Halmashauri Kuu ya CCM barua ya kuachia nafasi hiyo.

Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM kimependekeza jina la Katibu Mkuu wa zamani Abdulrahman Kinana kuteuliwa kupigiwa kura za kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Bara ambapo atachukua nafasi ya Philip Mangula.

Kikao hicho kimefanyika leo 31 Machi 2022 Jijini Dodoma.


Pia soma;

1). Nashauri Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula ang'atuke na akabidhi mikoba kwa Abdulrahman Kinana

2). Ukatibu Mkuu CCM: Nani anafaa kuchukua nafasi ya Daniel Chongolo? Kinana ndani

View attachment 2170662
Ni kwel kuwa nchi inaongozwa kutoka m.sog,a kwenda ddm.. hata kama hujui kusoma na picha hujui? Ongera sana comredi, twende sasa kuleeeee...
 
Kwa akili ya kawaida unaweza kuhisi hao ndyo walikuwa maadui wakubwa wa JPM.huenda hata uhai wake walichukua.
Sasa wanarudi Tena kutafuna Mali za watanzania
 
Huna akili mkuu. Unahemuka tu bila kuelewa chochote.

Sasa hapa umeandika kitu gani ninachoweza kukujibu!
Namimi nakazia ni punguani huyo hajui ili ccm itolewe nilazima yeye aunge nguvu kwa chadema au siyo wakenya waliamua kuigomea kanu anaandika Kama vile vyama vilivyopo madarakani hujiamualia vyenyewe kutoka ..aise chadema inakaazi kwelikweli
 
Mafisadi huwa yana demokrasia sana yanaiba ila yanakuachia uhuru wa kuyasema

Yanaruhusu mikutano ya hadhara na maandamano
Madikiteta huwa yanafanya vyote yanafisadi,yananyima uhuru wa kusema,yanabana demokrasi,yanaua na kutupa baharini,yanakuwa juu ya sheria nakadhalika yaani madikiteta hayaachi kitu CAG akiyakagua na kuyakosoa yanamufukuza...yanatafuta kundi dhaifu kwenye jamii kv wakulima na wajasiriamali yanalipa upendeleo kinyume na sheria ili yapendwe...madikiteta noma bora mafisadi
 
Subiri 2025 utajua hujui!

Ccm ina wadharau sana, si unaona hata baada ya kelele zenu za miaka nenda rudi kwamba kina kinana hawafai lakini bado wamerudishwa chamani, hii yote ni kuonesha kuwa hamna la kufanya!

Na hivi mmeungana na ccm kumsifia Samia ili kumkomoa marehemu,! Ccm 2025 itakuwa na kazi nyepesi sana.

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
Huo ndo ukweli.cdm ni kibaraka wa mafisadi.
Km wangekuwa ni wazalendo kweli wangeungana na magufuli kuyamaliza mafisadi.lakini walisaliti maneno yao.na Leo hawana Cha kusema,na hawana ujasili wa kuwasema mafisadi WALIO rudi Tena kuiba katika nchi hii.

Ili kuwasema mafisadi reference ni magufuli,na magufuli ndye walimgeuka na ndyo maana AKAONA hata bungeni hawana sababu ya kuwemo.

Sasa basis yao itakayowapa kuaminika Kwa wananchi kwamba wao ni watetezi wa wananchi ni ipi??

Uzalendo wao utaonekana wapi wakati waligeuka kusifia na kutetea mafisadi wakati wa jpm??

Nchii hii CCM itatawala muda mrefu sana
 
Back
Top Bottom