Picha adimu za TANU, Julius Nyerere na wazalendo waliosahaulika katika Historia ya kudai Uhuru

Massa,
Siwezi kulipa hisani ambayo JF wamenifanyia mimi.
Nani akinijua kabla sijaandika JF?

Hakika sina cha kuilipa JF.
Hata kama nitaanzisha jukwaa langu halitaweza hata kwa mbali kuifikia JF.
Huyu mzee Kiswahili cha kulainisha anakijua sana-katika kuongea kama ni hivi hivi, basi ni mtu hatari sana
 
Jembepori,
Maswali unayouliza hayaendani na mnakasha uliopo Majlis.
Narudia unajadili kitabu ambacho hujasoma.

Kasome kitabu kwanza ukimaliza kusoma rudi jamvini tujadili.
 
Jackline,
Usitishike na lugha.
Mie sina "vernacular."

Kiswahili ndiyo "mother tongue" yangu.

Wala mimi si mtu hatari.

Kilichokugusa wewe ni kuwa hukutegemea
jibu lile.

Ukweli ni kuwa JF ndiyo walonipa uwanja na watazamaji tena
bila malipo yoyote.
 
Huyu mzee Kiswahili cha kulainisha anakijua sana-katika kuongea kama ni hivi hivi, basi ni mtu hatari sana

Umejuwaje kama ni "hatari" sana? Kwa ulaini wa lugha yake tu? Au kwa Uislam wake?
 

Kwa post hii, nimezidi kumkubali Nyerere. Hakuwa mdini kabisa.

Mungu aendelee kumrehemu na hawa wazee wetu ( ambao wameshatangulia mbele ya haki) ambao wametufikisha hapa tulipo kwa moyo wa kishujaa sana.

Wazungu na Waarabu wamefanikiwa sana kutubagua watanzania na hizi dini zao.

Ntabakia kuwa mwafrika na kufuata imani ya mababu zangu.
 

Tazama Nyerere kazungukwa na wadini wangapi hapo?

Ikiwa Udini ni Uislam, basi kwa hakika Nyerere hakuwa mdini. Ila hao Waislam waliompokea, wakamuheshimu, wakamuenzi kwa usomi wake, wakala nae, wakalala nae, wakamfundisha Kiswahili, ndiyo walikuwa wadini wakubwa sana.
 

Hapana. Na wao pia hawakuwa wadini bali wenye upendo mkubwa.

Hao wazee na huyu Julius wote kwa pamoja hawakuwa wadini.

Nashangaa udini umeanzia kwenye kizazi hiki.

Wenye madini yao Uarabuni na Ulaya huko wametulia. Sisi miafrika tunajifanya tunazijua dini zao kuwashinda. Afu tunabaguana. Majinga sana sisi.....

Ama kweli Miafrika Ndivyo Tulivyo.... nakubaliana na komredi Nyani Ngabu
 
Last edited by a moderator:

Udini ulianzishwa na Nyerere.

Rais wa Kiafrika ambae anataka kupewa Utakatifu na Kanisa lake, kwa lipi zaidi? Fikiri.
 
Udini ulianzishwa na Nyerere.

Rais wa Kiafrika ambae anataka kupewa Utakatifu na Kanisa lake, kwa lipi zaidi? Fikiri.

Kumbe?

Hivi alitaka kupewa utakatifu?? Kweli?? Au kuna watu wanajipendekeza kumpa?? Kabla ya kifo chake sijawahi kusikia akitaka afanywe mtakatifu.

Anyway, mi si mdini kivile. Siamini sana kwenye haya madini yenu ya kuambukizwa na ngozi nyeupe.... yaliyokuja kwa meli na ndege...

Usiku mwema mama. (kama uko kwetu huku)
 

achana na hicho kibibi kinapenda udini hujapara kuona...
 

Mkuu mbona unajamba mpaka unaharisha
 

Ukinisoma vizuri utanielewa tu.
 
Hizi picha zinaonyesha hali halisi ya wazee hawa walivyokuwa Wazalendo.
 
Mwenyezi Mungu amzidishie heri Mwl Nyerere hakuwa mdini kabisa alikaa na kuishi katikati ya watu wa dini nyingine lakini hakuwa na dharau,aliishi na watu wa kada ya chini kabisa wasiokuwa na elimu dunia labda elmu ahera bila matatizo yoyote.Hakuna kama Mwl Nyerere Tanzania itachukua miaka mingi kumpata mtu wa aina ya Mwl Nyerere.
 

Ngongo,
Hilo suala la Nyerere kuwa au kutokuwa mdini nani wa kupitisha hukumu?
Wewe au mie?

Hili tulishalizungumza hapa na rejea kadhaa zikatolewa.
Sidhani kama kuna haja kwa sasa kulichokonoa hili jambo zaidi.
 

Kuna mambo ambayo yana ashiria lengo lake lilikua udini. Haya ni pamoja na suala la
Kura tatu kabla ya uhuru , hili waislam walilamika sana nini matokeo yake!
Kuvunjwa kwa baraza la wazee walokua chachu ya kudai uhuru na kumbeba Nyerere
Kuvunjwa kwa jumuia yenye nguvu ya waislam na kuundiwa Bakwata
Sheria ya ndoa
Kutaifisha mashule
Azimio la Arusha na kutaifisha mali na nyumba za watu mijini
Na vijiji vya ujamaa
Yote haya yalikuwa na direct impact na waislam na hali zao. Ukitaka kujua how ni kuingalia kila item kwa upeo wake utagungua tatizo la udini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…