Juhudi za wana Mzizima kuweka vuguvugu la Uhuru ...ukiwasha Barua hawakuwahi kufanya mkutano ...wowote wa harakati nje ya Kariakoo na Magomeni ...Huo ndio udhaifu mkubwa wa Watu wa Mzizima ...kuamini kuwa Kila KITU kilichoongelewa pale New street ...na mitaa ya msimbazi ..na jioni kwenye dhumna au Kahawa ni cha NCHI nzima .....hatukatai harakati zikianza Dar Ila udhaifu mkubwa waliofanya ni kutokueneza chama nje
TAA na baadaye TANU Ilianza kufanya ziara mikoani kwa kasi Baada ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere ,Rashid Kawawa ,Oscar Kambona ,Titi Mohamed ...na wengine kuingia na kufanya ziara ndefu sana mikoani ...Hii ndio iliunganisha Juhudi zilizokuwa zikiendelea Dar na Kina Paul Bomani ( Ziwa ) , George Kahama ( kagera ), hamza mwapachu ( Tanga ) , abdala said fundikira ,kasela bantu ,kasanga tumbo ( tabora ) , chief kunambi ( tabora ) Amir kaluta ( kigoma ) , Japhet killiro ( Arusha ) , chief marealle ,chief shangali ,Nsillo Swai ( Kilimanjaro ) ...na wengine wengi
Tanzania haingeweza kupata Uhuru Kama TANU au TAA ingendelea kubaki mitaa wa Lumumba !!!! Kwa Baadhi ya maeneo hata ya Kaskazini walikuwa wanakaribiwa kupewa free state ..Hadi Mwalimu alipofika na kutaka Province zote ziunganishe nguvu .....Sasa unawezaje Kusema kuwa Uhuru ulidaiwa Dar tu Kama tayari sehem Kama Kilimanjaro walishafikia kuwa na serikali ya Ndani ya Wenyeji ( native Gorvernment ) ..yenye Ikulu , mahakama , walinzi na mawaziri ...the only second after Buganda In the region ...hata Kikuyu Kenya hawakuwahi kuwa na serikali ya Ndani
Phillemon Mikael,
Inaelekea huijui historia ya TANU.
Mikutano ya hadhara ilianza baada ya kuwa na chama cha siasa.
Isingewezekana kufanya mkutano wa hadhara wa siasa chini ya TAA.
Kwa hili hapakuwa na udhaifu wowote kwa watu wa Dar es Salaam.
Ikiwa unataka tutaje udhaifu basi huo udhaifu utafutwe kwengine ambako
hapakuwa na vuguvugu lolote dhidi ya ukoloni.
Kwa mukhtasari tu nitakueleza kuwa baada ya TANU kuundwa safari ya
kwanza mwaka wa 1954 ilikuwa Morogoro ambako
Zuberi Mtemvu aliongozana
na
Nyerere.
Safari ya pili ilikuwa Lindi ambako
Nyerere aliongozana na
Ali Mwinyi Tambwe na
safari hii ilikuwa lazima ifanyike kwa kuwa Kanisa lilikuwa linawavunja waumini wao
nguvu wasiunge mkono TANU.
Ukipenda kusoma zaidi kuhusu haya kitafute kitabu cha
Abdul Sykes.
Ndani ya kitabu hiki nimeeleza nini kilifanyika kati ya 1950 - 1954 kuwaamsha
wananchi kujiunga na TAA majimboni.
Makaratasi yaliyokuwa yanamwagwa huko majimboni yalikuwa yanachapwa Mtaa wa
Kipata nyumbani kwa
Ally Sykes akitumia mashine ya kudurufu aliyokuwa ameificha.
Katika utafiti wangu nimesoma haya makaratasi na yapo katika orodha ya rejea katika
kitabu cha
Abdul Sykes.
Juu ya juhudi hizi kulikuwa na safari alizofanya
Abdulwahid Sykes kupita majimboni
akifanya mikutano ya siri na viongozi wa TAA kuwaeleza nini kinaendelea New Street.
Katika viongozi mashuhuri aliokutananao ni
Paul Bomani ukimtoa
Chief Kidaha ambae
alikuwa akikutanananae nyumbani kwake Dar es Salaam.
Habari za mikutano hii unaweza kuipata katika Tanganyika Intelligence Gazette taarifa
za kikachero za Special Branch za miaka ya 1950.
Viongozi hawa walikuwa wanajua fika kuwa bila ya kuwa na umoja wa Watanganyika wote
safari ya uhuru itakuwa ndefu sana.
Bahati mbaya wewe umeweka majina tu ya kina
Marealle,
Kirilo, Shangali na wengineo
bila kujua historia zao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Soma kitabu cha
Abdul Sykes uione historia ya uhuru wa Tanganyika kwa ukweli wake.