Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,557
- 8,673
Phillemon Mikael,
Inaelekea huijui historia ya TANU.
Mikutano ya hadhara ilianza baada ya kuwa na chama cha siasa.
Isingewezekana kufanya mkutano wa hadhara wa siasa chini ya TAA.
Kwa hili hapakuwa na udhaifu wowote kwa watu wa Dar es Salaam.
Ikiwa unataka tutaje udhaifu basi huo udhaifu utafutwe kwengine ambako
hapakuwa na vuguvugu lolote dhidi ya ukoloni.
Kwa mukhtasari tu nitakueleza kuwa baada ya TANU kuundwa safari ya
kwanza mwaka wa 1954 ilikuwa Morogoro ambako Zuberi Mtemvu aliongozana
na Nyerere.
Safari ya pili ilikuwa Lindi ambako Nyerere aliongozana na Ali Mwinyi Tambwe na
safari hii ilikuwa lazima ifanyike kwa kuwa Kanisa lilikuwa linawavunja waumini wao
nguvu wasiunge mkono TANU.
Ukipenda kusoma zaidi kuhusu haya kitafute kitabu cha Abdul Sykes.
Ndani ya kitabu hiki nimeeleza nini kilifanyika kati ya 1950 - 1954 kuwaamsha
wananchi kujiunga na TAA majimboni.
Makaratasi yaliyokuwa yanamwagwa huko majimboni yalikuwa yanachapwa Mtaa wa
Kipata nyumbani kwa Ally Sykes akitumia mashine ya kudurufu aliyokuwa ameificha.
Katika utafiti wangu nimesoma haya makaratasi na yapo katika orodha ya rejea katika
kitabu cha Abdul Sykes.
Juu ya juhudi hizi kulikuwa na safari alizofanya Abdulwahid Sykes kupita majimboni
akifanya mikutano ya siri na viongozi wa TAA kuwaeleza nini kinaendelea New Street.
Katika viongozi mashuhuri aliokutananao ni Paul Bomani ukimtoa Chief Kidaha ambae
alikuwa akikutanananae nyumbani kwake Dar es Salaam.
Habari za mikutano hii unaweza kuipata katika Tanganyika Intelligence Gazette taarifa
za kikachero za Special Branch za miaka ya 1950.
Viongozi hawa walikuwa wanajua fika kuwa bila ya kuwa na umoja wa Watanganyika wote
safari ya uhuru itakuwa ndefu sana.
Bahati mbaya wewe umeweka majina tu ya kina Marealle, Kirilo, Shangali na wengineo
bila kujua historia zao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Soma kitabu cha Abdul Sykes uione historia ya uhuru wa Tanganyika kwa ukweli wake.
Kitabu cha Mzee Sykes na simulizi zake za mdomo kwa waliobahatika kuongea naye ..kiko biased kiasi Fulani ....Kama ilivyo historia rasmi ya NCHI Hii nayo Ina mapungufu ...LENGO la kitabu cha Sykes linajulikana Pamoja na mengi mazuri yaliyomo ....
Mimi nafikiri historia ya NCHI Hii inatakiwa kuandikwa UPYA Sasa na watafiti Huru wasiopendelea upande wowote
Mfano mchango wa Watu waMikoani kwenye kupambana na uokoloni kwenye vitabu hata historia rasmi haujaandikwa ...kwa kuwa tu Hapakuwa na "kamera ..." lakini waliukataa ukoloni ....
Kuna Watu wana LENGO la kudanganya Watu kuwa wao pekee ndio walipigania Uhuru
