Picha Ajali: Wasiofahamika wateketea kwa moto katika ajali Mufindi, gari zimeisha kabisa yamebaki majivu

Picha Ajali: Wasiofahamika wateketea kwa moto katika ajali Mufindi, gari zimeisha kabisa yamebaki majivu

Hauko serious mkuu, kigogo kibaki wakati binaadam kayaking jivu? Hiyo picha ni baada ya magari kupelekwa pembeni ya barabara.
Gari zimeungua hapo hapo unapoziona faza angalia lile bati kushoto la ukiongo wa bara bara hata sehemu lilipo truck utaona nalo limeungua yaani kusoma picha tu inakushinda aisee daah utawasha G 460 wewe kweli..
 
Nawapa 5 wazee wetu wakongwe, zamani huko.
Kuna mshua alipiga gia najmunisa ilikua MAN Ile au nissan diesel sa 1 tuko kibaha barabara ilikua vumbi na jamaa katoka Shinyanga huko.50
Tukapigwa pini. Kibaha tukae mpk muda wa bus unaotakiwa tufike dar.
Kuna kabus kanaitwa lipuli kalikua kanatambaa balaa
King cross wale madereva achana nao, shalawambe,urafiki kule kulikua na madereva haswa.
Hekima bus ndo mara ya mwisho tumefika ubungo sa tisa jioni na jamaa katoka tunduma asubuhi mi nilipanda mbeya sa 3 asubuhi.
 
We jamaa akiri yako ni nyepesi sana,uko smart sana
Daah jamaa wa Truck waliweka kigogo na jack na upande wa kushoto inaonekana walikua washatoa tairi kwa maelezo ya picha jamaa wa pick up kaenda kugonga Truck lililopaki likitengenezwa na likiwa upande wake...
 
Bakukijana umenikumbusha Hekima bus na ndugu yake Scandinavia bus ambalo wazambia walikua wanaenda mjini kulishangaa wao leo wana bus ambazo Tanzania haizizidi tatu na wao zimejaa mpaka zinaenda vijijini..
 
Maeneo hayo sio ya kukimbia kama ngiri harafu usiku hapo kaua wote waliokuwepo kwenye hilo gari kubwa maana baada ya kugonga matenki ya diesel yakapasuka na kusababisha moto..
Aue watu wote kwenye tanker wakati unaambiwa dereva wa roli anashikiliwa kwa mahojiano? Huwa mnasomaje nyie?
 
Gari zimeungua hapo hapo unapoziona faza angalia lile bati kushoto la ukiongo wa bara bara hata sehemu lilipo truck utaona nalo limeungua yaani kusoma picha tu inakushinda aisee daah utawasha G 460 wewe kweli..
Sasa iweje chuma kibaki hivyo halafu kigogo kisiungue? Moto wa mafuta ni hatari mzee
 
Nawapa 5 wazee wetu wakongwe, zamani huko.
Kuna mshua alipiga gia najmunisa ilikua MAN Ile au nissan diesel sa 1 tuko kibaha barabara ilikua vumbi na jamaa katoka Shinyanga huko.50
Tukapigwa pini. Kibaha tukae mpk muda wa bus unaotakiwa tufike dar.
Kuna kabus kanaitwa lipuli kalikua kanatambaa balaa
King cross wale madereva achana nao, shalawambe,urafiki kule kulikua na madereva haswa.
Hekima bus ndo mara ya mwisho tumefika ubungo sa tisa jioni na jamaa katoka tunduma asubuhi mi nilipanda mbeya sa 3 asubuhi.
Nikiamka nitosoma tena.
 
Ukiangalia kwa makini utagundua tyre iliungua ikiwa kwenye rim yake, hiyo jack pia ilipigwa baada ya ajali' (angalia ilipowekwa) hicho kigogo pia ni baada ya ajali. Nafikiri ni juhudi za kuiondoa gari sehemu hatarishi baada ya ajali.

Pia picha ya pickup imepigwa baada ya kuondolewa kwenye eneo la ajali.
 
Watu wasiofahamika Wamefariki Dunia kwa kuteketea kwa moto na kubakia majivu baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso na kisha kuwaka moto na kuteketea na kusababisha vifo hivyo.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi katika eneo la tukio Mei 29,2025 Mkuu wa wa Polisi Wilaya ya Mufindi SSP Anthony Gwandu, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema chanzo chake ni kuendesha kwa uzembe gari hilo.

SSP Gwandu amesema ajali hiyo imetokea Mei 28 , 2025 saa 19:05 usiku huko kata ya Sao hill Shamba la miti ya kupandwa la Serikali , barabara kuu ya Iringa - Njombe baada ya magari hayo mawili kugongana na kisha kuwaka moto na kusababisha uharibifu huo.

Amelitaja gari lenye namba za usajili AID 4830 ZM/ AID 4831 ZM aina ya IVECO Tenki ikiendeshwa na dereva Gimson Lungu (32) raia na mkazi wa Lusaka Zambia , ikiwa imebeba mzigo wa mafuta aina ya diesel likitokea Dar es Salam kwenda Congo (DRC) iligongana uso kwa uso na gari dogo.

Gari hilo dogo Toyota double Cabin ambayo namba zake na dereva bado kujulikana likitokea Makambako kuelekea Iringa liliungua na kuteketea kwa moto baada ya magari hayo kugongana uso kwa uso.

Hata hivyo Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mufindi SSP Gwandu alisema uchunguzi zaidi unaendelea kubaini gari hilo dogo Toyota Double cabin kulikuwa na Watu wangapi zaidi ya dereva.

Aidha katika gari hilo dogo hakuna mabaki yoyote ya Binadamu yaliyoonekana zaidi ya majivu na kwamba chanzo kinachunguzwa zaidi huku dereva wa gari kubwa akiwa anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano zaidi.
View attachment 3350490
View attachment 3350493
Usikute washamimina mafuta yote wakatafuta pickup mbovu wakazichoma kwa pamoja
 
Back
Top Bottom