Picha: Dar es Salaam waonesha uhalisia suala la bandari nchini. Viongozi wajitafakari sana

Habari zenu wana JF na wazalendo wenzangu wote mliopo humu kwa ujumla,

Ndugu zangu wana JF, hapa nchini au duniani tunapozungumzia Mkoa wa Dar es Salaam basi ni ukweli ulio wazi kwamba ni kama vile tunakuwa tumeizungumzia Tanzania nzima. Nasema hivi kwa sababu kuu mbili.

1. Dar es Salaam ndio iliyobeba taaswira halisi ya nchi, ndio maana mkoa huu uliongoza mapambano yote ya kudai uhuru, na mambo mengine mengi ya kiserikali na kijamii yalifanyikia Dar es Salaam, kabla na baada ya uhuru.

2. Dar es Salaam ndio Mkoa uliokusanya makabila yote kutoka mikoa na maeneo mbali mbali ya nchi (kabila langu likiwa moja wapo wa wahamiaji wa Mkoa huu). Hivyo kila linalofanyika mkoa huu linakuwa limegusa kwa kiwango kikubwa mikoa mingine na watu wake kwa ujumla.

Sasa ukiona kiongozi au mtu maarufu anakataliwa katika mkoa wa Dar es Salaam, basi anatakiwa ajitafakari vizuri, kuliko kukimbilia kuwapa vijana vijihela na data za kuja mitandaoni kumsafisha na kutunga propaganda mbalimbali, sababu kuna uwezekano mkubwa wa kukataliwa nchi nzima.

Mwaka 2020 katika kampeni za uchaguzi mkuu, kuna chama kilimsimamisha mgombea kutoka ulaya, kwa kufikiri labda wana Dar es Salaam na watanzania kwa ujumla watadanganyika, watetemeke na kumpa kura mgombea huyo. Lakini kumbe hali ikawa tofauti kwa kuanza kupuuzwa na wana Dar es Salaam na watanzania kwa ujumla, hivyo kupelekea mgombea huyo kutoka ulaya kuangukia pua katika uchaguzi ule.

Na yeye kwa aibu siku mbili tatu baada ya uchaguzi akakimbilia ulaya kwa kudanganya umma kuwa anasakwa na serikali ili iwe rahisi yeye kupewa hifadhi ya ukimbizi na pia kujitoa katika kashfa ya aibu ya kushindwa uchaguzi.

Watu wenye akili tulijiuliza, kama kweli alitakiwa kuuwawa, kwanini asingeliuwawa wakati wa kampeni, badala yake aje auwawe baada ya uchaguzi, tena uchaguzi ambao yeye ndo ameshindwa!

Hilo likapita, sasa likaja hili la bandari chama hicho kilichoangukia pua Dar katika uchaguzi mkuu, kikalivalia njuga na swala hili wakiamini kuwa lingewabeba katika mkoa huo wenye mamilioni ya watu.

Cha kushangaza, pamoja na kualika viongozi njaa wa dini, wanasheria uchwara na wanasiasa wachumia tumbo kutoka maeneo mbali mbali ya nchi lakini bado wana Dar es Salaam wakaendelea kukiadhibu chama hicho na genge lake bila huruma.

Ndio maana nashauri viongozi wa chama hicho wajitafakari upya kuhusu kuelekeo wao. Kuruhusu wapitisha madawa ya kulevya, wezi, wakwepa kodi na ushuru wa bandari wawatumie katika ajenda zao kwa sababu ya malipo madogo tu yanayoliwa na viongozi wachache wa chama lilikuwa ni kosa la kiufundi.

Pia hii style ya kusambaza vijana wenye ID kumi kumi mitandaoni, kwani katika mkutano huonekana watu na sio wingi wa ID zao. Mfano humu tulitangaziwa mkutano wa bandari pale temeke, masham masham mitandaoni yakawa mengi, lakini siku ilipofika watu hawakujitokeza kama ilivyodhaniwa.

Hii ni dalili kuwa hii pinga pinga ya bandari ni ya mitandaoni tu lakini mitaani na nchini hakuna anaepinga.

View attachment 2699597
Umeupiga mwingu mkuu
 
Attachments

  • chadema.jpg
    chadema.jpg
    93.2 KB · Views: 2
Nishamalizana nawe mkuu, sina la ziada la kuongeza katika yale niliyokwishaelza hapo juu.

Ukija na wazo jipya ulilotumia akili kulitambua kuwa ni jamb zuri, nitakusoma na kujadili nawe, lakini siyo takataka hizi unazoleta hapa kwa muda mrefu sasa.
Safi sana mkuu, ndio njia sahihi
 
Watanzania hawajaridhika na uwekezaji wa bandari, serikali isione aibu kuachana na Waarabu​

Watu wenye akili tulijiuliza, kama kweli alitakiwa kuuwawa, kwanini asingeliuwawa wakati wa kampeni, badala yake aje auwawe baada ya uchaguzi, tena uchaguzi ambao yeye ndo ameshindwa!
Ungekuwa na akili usingeandika huu ugoro!
Kichwa bila akili ni adhabu kwa shingo!
Bora ungekaa kimya kuficha upumbavu!
 
Kuna anko wangu alileta mzigo kutoka China figisu figisu alizokutana nazo pale bandarini bado nusu auziwe mbuzi kwenye gunia kwa kubadilishiwa mzigo.

Bahati nzuri anko nae mkorofi ileile ivyo jamaa wakanywea. Imagine kama angekuwa ni mtu kutoka Zambia au Rwanda hali ingekuaje
Acha upotoshaji bandari haziuzwi,kama ccm mnakilalu cha kuuza kauzeni Figo zonu mnazomilike wenyewe sio kuuza mali za watanganyika
 
Habari zenu wana JF na wazalendo wenzangu wote mliopo humu kwa ujumla,

Ndugu zangu wana JF, hapa nchini au duniani tunapozungumzia Mkoa wa Dar es Salaam basi ni ukweli ulio wazi kwamba ni kama vile tunakuwa tumeizungumzia Tanzania nzima. Nasema hivi kwa sababu kuu mbili.

1. Dar es Salaam ndio iliyobeba taaswira halisi ya nchi, ndio maana mkoa huu uliongoza mapambano yote ya kudai uhuru, na mambo mengine mengi ya kiserikali na kijamii yalifanyikia Dar es Salaam, kabla na baada ya uhuru.

2. Dar es Salaam ndio Mkoa uliokusanya makabila yote kutoka mikoa na maeneo mbali mbali ya nchi (kabila langu likiwa moja wapo wa wahamiaji wa Mkoa huu). Hivyo kila linalofanyika mkoa huu linakuwa limegusa kwa kiwango kikubwa mikoa mingine na watu wake kwa ujumla.

Sasa ukiona kiongozi au mtu maarufu anakataliwa katika mkoa wa Dar es Salaam, basi anatakiwa ajitafakari vizuri, kuliko kukimbilia kuwapa vijana vijihela na data za kuja mitandaoni kumsafisha na kutunga propaganda mbalimbali, sababu kuna uwezekano mkubwa wa kukataliwa nchi nzima.

Mwaka 2020 katika kampeni za uchaguzi mkuu, kuna chama kilimsimamisha mgombea kutoka ulaya, kwa kufikiri labda wana Dar es Salaam na watanzania kwa ujumla watadanganyika, watetemeke na kumpa kura mgombea huyo. Lakini kumbe hali ikawa tofauti kwa kuanza kupuuzwa na wana Dar es Salaam na watanzania kwa ujumla, hivyo kupelekea mgombea huyo kutoka ulaya kuangukia pua katika uchaguzi ule.

Na yeye kwa aibu siku mbili tatu baada ya uchaguzi akakimbilia ulaya kwa kudanganya umma kuwa anasakwa na serikali ili iwe rahisi yeye kupewa hifadhi ya ukimbizi na pia kujitoa katika kashfa ya aibu ya kushindwa uchaguzi.

Watu wenye akili tulijiuliza, kama kweli alitakiwa kuuwawa, kwanini asingeliuwawa wakati wa kampeni, badala yake aje auwawe baada ya uchaguzi, tena uchaguzi ambao yeye ndo ameshindwa!

Hilo likapita, sasa likaja hili la bandari chama hicho kilichoangukia pua Dar katika uchaguzi mkuu, kikalivalia njuga na swala hili wakiamini kuwa lingewabeba katika mkoa huo wenye mamilioni ya watu.

Cha kushangaza, pamoja na kualika viongozi njaa wa dini, wanasheria uchwara na wanasiasa wachumia tumbo kutoka maeneo mbali mbali ya nchi lakini bado wana Dar es Salaam wakaendelea kukiadhibu chama hicho na genge lake bila huruma.

Ndio maana nashauri viongozi wa chama hicho wajitafakari upya kuhusu kuelekeo wao. Kuruhusu wapitisha madawa ya kulevya, wezi, wakwepa kodi na ushuru wa bandari wawatumie katika ajenda zao kwa sababu ya malipo madogo tu yanayoliwa na viongozi wachache wa chama lilikuwa ni kosa la kiufundi.

Pia hii style ya kusambaza vijana wenye ID kumi kumi mitandaoni, kwani katika mkutano huonekana watu na sio wingi wa ID zao. Mfano humu tulitangaziwa mkutano wa bandari pale temeke, masham masham mitandaoni yakawa mengi, lakini siku ilipofika watu hawakujitokeza kama ilivyodhaniwa.

Hii ni dalili kuwa hii pinga pinga ya bandari ni ya mitandaoni tu lakini mitaani na nchini hakuna anaepinga.

View attachment 2699597
Tunangoja kupata elimu uzuri wa mkataba wa bandari kifungu kwa kifungu achana na ngojera marume.
 
Wakazi wa Dar na viunga vyake tunazijuwa fursa zitazozalishwa na bandari ya kisasa.

Hao DP WORLD wengine hapa tunawangoja kwa hamu. Tuna vijukuu vyetu tunataka violewe Dubai.
Fursa hizo.

Wewe huna tofauti na yule Mwenyekiti wa CCM Nyamagana.
Kumbe ndio sera zenu za kutaka kuolewa na waarabu!
Utumwa mbaya sana.
 
Watanzania hawajaridhika na uwekezaji wa bandari, serikali isione aibu kuachana na Waarabu​

Bila shaka unazungumzia watanzania wa mitandaoni ambao kiuhalisia hawafiki hata mia moja.
Huku mitaani ukiachilia mbali wale wanaotafuna mema ya bandari kwa kupitisha biashara zao bila kulipa ushuru au kodi, au wale wanaopiga madili ya kuuza vifaa mbali mbali vya watu vilivyopo bandarini, wananchi wa kawaida wengi wameridhika na mkataba. Ndomaana hawana muda wa kwenda kusimama juani kupotoshwa na wale wanaonufaika na mfumo mbovu wa bandarini.
 
Ungekuwa na akili usingeandika huu ugoro!
Kichwa bila akili ni adhabu kwa shingo!
Bora ungekaa kimya kuficha upumbavu!
Huyo unaemuona ana akili sasa hivi anapambana kupewa nafasi ya kwenda kuhiji katika kaburi la yule aliemsingizia ili atubu dhambi zake na kukiri uongo wake pale kaburini.

Kwa vile umeshikiwa akili basi ni ngumu sana wewe kuwa huru kulijua hili.
 
Tunangoja kupata elimu uzuri wa mkataba wa bandari kifungu kwa kifungu achana na ngojera marume.
Ngonjera ni nyingi mno. Genge la wakwepa ushuru na kodi pale bandarini linazunguka mikoani kuwalaghai watanzania wenzetu kwamba bandari imeuzwa, ila wakiulizwa waoneshe mkataba mzima ili watanzania waone hilo eneo la mauziano kwa lengo la kutaka wasipigwe changa kama lile la enzi ya Lowasa, jamaa wanakuwa wakali na kuanza kumkukana raisi.
 
Hiki ni kufungu namba ngapi kwenye mktaba DPW?
 
Mkuu mbona haueleweki. Nakwambia kwamba kuna genge la wanasiasa uchwara na mawakili njaa na viongozi wa dini waliozoea kupitisha vitu vyao au biashara pale bandarini bila kulipishwa kodi, linazunguka nchi nzima kuwahadaa watanzania kwamba mkataba wa bandari una lengo la kuuza bandari zetu.
Sasa genge hilo linalodanganya kwamba bandari imeuzwa likiulizwa liweke mkabata hadharani ili kila mtanzania aone hicho kifungu cha mauziano kati ya serikali na dp world, genge hilo haliweki mkataba maana linajua kama linapotosha, na badala yake linaanza kumtukana raisi.

Kwahiyo hili swali lako ulitakiwa uwaulize hao wanasiasa uchwara wakuoneshe kifungu kinachoonesha mauziano.
Nina Imani hilo genge unalifahamu ni la kina nani au chama gani
 
Ila mm na familia yangu pamoja na ukoo wangu woooote tunasema tunataka Bandari yetu.
Asante
 
Mkuu mbona haueleweki. Nakwambia kwamba kuna genge la wanasiasa uchwara na mawakili njaa na viongozi wa dini waliozoea kupitisha vitu vyao au biashara pale bandarini bila kulipishwa kodi, linazunguka nchi nzima kuwahadaa watanzania kwamba mkataba wa bandari una lengo la kuuza bandari zetu.
Sasa genge hilo linalodanganya kwamba bandari imeuzwa likiulizwa liweke mkabata hadharani ili kila mtanzania aone hicho kifungu cha mauziano kati ya serikali na dp world, genge hilo haliweki mkataba maana linajua kama linapotosha, na badala yake linaanza kumtukana raisi.

Kwahiyo hili swali lako ulitakiwa uwaulize hao wanasiasa uchwara wakuoneshe kifungu kinachoonesha mauziano.
Nina Imani hilo genge unalifahamu ni la kina nani au chama gani
Wewe onyesha vifungu kwenye mkataba vinavyoonyesha kuwa bandari zetu hazijauzwa.
 
Back
Top Bottom