Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mbona watu wengi wanamjua na wanamjadili?tuache unafikiKibonde anau-superstar gani...???
Habari JF lovers,
Hii ishu ya Kibonde ni kama ime kick sana, kwamba alijaribu kuvunja sheria huku akiwa amelewa,
The fact is Kibonde alikua anatengeneza Tangazo la Usalama Barabarani "TII SHERIA BILA SHURUTI"
mbona watu wengi wanamjua na wanamjadili?tuache unafiki
Habari JF lovers,
Hii ishu ya Kibonde ni kama ime kick sana, kwamba alijaribu kuvunja sheria huku akiwa amelewa,
The fact is Kibonde alikua anatengeneza Tangazo la Usalama Barabarani "TII SHERIA BILA SHURUTI"
habari ya nyongeza kutoka kwa elizabeth hombo iliyopatikana hapa hapa jf inasema kuwa: Watangazaji maarufu wa redio nchini, ephraim kibonde na gadner g. Habash, wametiwa mbaroni katika kituo cha polisi cha oysterbay, jijini dar es salaam baada ya kudaiwa kusababisha ajali na kukaidi amri ya askari wa usalama barabarani. kibonde ambaye amejizolea umaarufu kupitia kipindi cha jahazi kinachorushwa na kituo cha redio cha clouds fm akiwa na mtangazaji mwenzake wa radio times, gadner, walikutwa na mkasa huo jana saa 12 asubuhi katika eneo la makumbusho.
taarifa zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na kamanda wa polisi mkoa wa kinondoni, camillius wambura, zilieleza kuwa kibonde ambaye alikuwa dereva wa gari hilo aligonga kwa nyuma gari lililokuwa likiendeshwa na raia wa kigeni (mzungu).
akizungumza na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani, kamanda wambura alisema baada ya kibonde kusababisha ajali hiyo, alikaidi amri ya askari wa usalama barabarani iliyomtaka asimame ili wapime na badala yake aliondoa gari kwa mwendo kasi hali iliyoashiria alikuwa amekimbia. alisema baada ya kukaidi amri hiyo, askari aliyekuwepo eneo la tukio naye alipanda gari jingine kwa nia ya kumfukuza na kwamba alipofika eneo la mwenge alifanikiwa kumsimamisha na kisha kupanda katika gari lake ili warudi eneo ilikotokea ajali.
kwa mujibu wa wambura, baada ya askari huyo kupanda kwenye gari la kibonde, mtangazaji huyo hakurudi kwenye eneo la tukio na badala yake aliendelea kukata mitaa mingine.
bahati nzuri askari wetu huyo alikuwa anawasiliana na wenzake, walipofika eneo la ubungo mataa wakawawekea kizuizi kilichowasaidia kuwakamata. nilipata taarifa hizo za kibonde nikiwa kwenye kikao, ni kweli alisababisha ajali majira ya saa 12 asubuhi pale makumbusho na alimgonga mzungu ambaye hata hivyo sikuishika namba ya gari lake, alisema kamanda wambura. alieleza kuwa baada ya askari wa ubungo kufanikiwa kuwakamata, waliwafikisha katika kituo cha polisi cha oysterbay na walibaini kuwa watangazaji hao walikuwa wamelewa. walipofikishwa kituoni na kutakiwa kupimwa ulevi waligoma kwa sababu kibonde alikuwa hana uwezo wa kuendesha tena gari na walikuwa wanatoa lugha chafu za matusi kwa askari wetu, alisema.
alipoulizwa kuwa ni sheria zipi walizozivunja, kamanda wambura aliyataja makosa matano, ambayo ni kusababisha ajali, kutokutii amri ya askari, kukimbia na kutoroka na askari, kutoa lugha chafu za matusi na kukataa kupimwa ulevi.
kamanda wambura alisema kwa sasa wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo, na baada ya kuukamilisha watapeleka jalada kwa wakili wa serikali ili watangazaji hao washitakiwe. akiwazungumzia watangazaji hao, kamanda wambura alisema kuwa wao wanawaona kama wahalifu wa makosa ya jinai na kamwe hawatawachukulia kama watu maarufu.
sisi hatutajali kama watangazaji hao ni watu maarufu, na kwamba mbele ya uso wa sheria hakuna umaarufu, alisisitiza wambura ambaye hadi tunakwenda mitamboni jana jioni alisema watangazaji hao walikuwa bado rumande.
Tatizo ni foleni wandugu. Tuko wengi tuna hasira kutokana na kucheleweshwa makazini na foleni ya magari jijini. Maaskari wa barabarani ni wasumbufu sana,mara nyingi wanachelewesha magari ya upande fulani,na kuruhusu ya upande mwingine kwa muda mrefu. Nafikiri jamaa alikuwa anawahi airport. Lakini kwa nini adhalilishwe hadharani kiasi hicho,askari wetu wanatumia maguvu zaidi,kichwani zero. Sikubaliani na kibonde kwa mengi,lakini kwa hili amedhalilihwa.
Yupo peku huyo mchek vizuri.Mbona kaingia na viatu?
Mwendawazimu kaingiaje apo?
Invisible
mlituambia Jamii Media imeajili waandishi wake wa habari sasa wanafanya
nini hii thread tumeshaanza kulishana matango pori ni kwa nini
waandishi wa Jamii media polisi tupate usahihi wa habari hii?
Sasa gadna anaunganishwaje kwenye kesi hyo?maana nijuavyo mm dreva ni kibonde, mtusaidie ili wengine tujue!
Ataibuka name kukana picha hiyo na kusema ya dukani
Unaambiwa askari katekwa, katukanwa bado unataka amkamate kwa kwa mahaba? Ok foleni inachelewesha watu, kwa hiyo unaamua kumgonga aliyembele yako kisha husimami unakimbia kwani huyo aliyembele yako ndiye kasababisha foleni.
Kitendo alichofanya Kibonde ni huo ulevi na majidai tuu kwa kujidhania ana umaarufu wa kumwezesha kufanya atakalo. Hapo kuna makosa ya faini na ya jela, ngoja sheria ichukue mkondo ndio watu watajifunza.
Sent from my iPad using JamiiForums
Habari ya nyongeza kutoka kwa ELIZABETH HOMBO iliyopatikana hapa hapa JF inasema kuwa: Watangazaji maarufu wa redio nchini, Ephraim Kibonde na Gadner G. Habash, wametiwa mbaroni katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, jijini Dar es Salaam baada ya kudaiwa kusababisha ajali na kukaidi amri ya askari wa usalama barabarani. Kibonde ambaye amejizolea umaarufu kupitia kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha redio cha Clouds Fm akiwa na mtangazaji mwenzake wa Radio Times, Gadner, walikutwa na mkasa huo jana saa 12 asubuhi katika eneo la Makumbusho.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, zilieleza kuwa Kibonde ambaye alikuwa dereva wa gari hilo aligonga kwa nyuma gari lililokuwa likiendeshwa na raia wa kigeni (mzungu).
Akizungumza na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani, Kamanda Wambura alisema baada ya Kibonde kusababisha ajali hiyo, alikaidi amri ya askari wa usalama barabarani iliyomtaka asimame ili wapime na badala yake aliondoa gari kwa mwendo kasi hali iliyoashiria alikuwa amekimbia. Alisema baada ya kukaidi amri hiyo, askari aliyekuwepo eneo la tukio naye alipanda gari jingine kwa nia ya kumfukuza na kwamba alipofika eneo la Mwenge alifanikiwa kumsimamisha na kisha kupanda katika gari lake ili warudi eneo ilikotokea ajali.
Kwa mujibu wa Wambura, baada ya askari huyo kupanda kwenye gari la Kibonde, mtangazaji huyo hakurudi kwenye eneo la tukio na badala yake aliendelea kukata mitaa mingine.
Bahati nzuri askari wetu huyo alikuwa anawasiliana na wenzake, walipofika eneo la Ubungo Mataa wakawawekea kizuizi kilichowasaidia kuwakamata. Nilipata taarifa hizo za Kibonde nikiwa kwenye kikao, ni kweli alisababisha ajali majira ya saa 12 asubuhi pale Makumbusho na alimgonga Mzungu ambaye hata hivyo sikuishika namba ya gari lake, alisema Kamanda Wambura. Alieleza kuwa baada ya askari wa Ubungo kufanikiwa kuwakamata, waliwafikisha katika kituo cha Polisi cha Oysterbay na walibaini kuwa watangazaji hao walikuwa wamelewa. Walipofikishwa kituoni na kutakiwa kupimwa ulevi waligoma kwa sababu Kibonde alikuwa hana uwezo wa kuendesha tena gari na walikuwa wanatoa lugha chafu za matusi kwa askari wetu, alisema.
Alipoulizwa kuwa ni sheria zipi walizozivunja, Kamanda Wambura aliyataja makosa matano, ambayo ni kusababisha ajali, kutokutii amri ya askari, kukimbia na kutoroka na askari, kutoa lugha chafu za matusi na kukataa kupimwa ulevi.
Kamanda Wambura alisema kwa sasa wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo, na baada ya kuukamilisha watapeleka jalada kwa wakili wa serikali ili watangazaji hao washitakiwe. Akiwazungumzia watangazaji hao, Kamanda Wambura alisema kuwa wao wanawaona kama wahalifu wa makosa ya jinai na kamwe hawatawachukulia kama watu maarufu.
Sisi hatutajali kama watangazaji hao ni watu maarufu, na kwamba mbele ya uso wa sheria hakuna umaarufu, alisisitiza Wambura ambaye hadi tunakwenda mitamboni jana jioni alisema watangazaji hao walikuwa bado rumande.
Kama ni tangazo litavunja record ya matangazo dunian kote kwa kufuatiliwa na watu wengi, ila najua pombe sa iv zimekwisha so anaomba msmaha wayamalize na aliyemgonga, kama namuona anavyo;!!Et Tangazo la kutii sheria bila shuruti!