PICHA: Freeman Mbowe katika uso wa tabasamu na furaha kubwa hii leo Juni 30, 2025

PICHA: Freeman Mbowe katika uso wa tabasamu na furaha kubwa hii leo Juni 30, 2025

Dah, Ila siasa ni field ya ajabu sana. Mbowe alivyoishia kutukanwa na kudhihakiwa na kina Heche! Sikuamini..!
Watu wengine mnapenda kujibebea dhambi ya uongo isiyo hata na sababu..

Hivi bibie mwenye jina la DATAZ Unaweza kuthibitisha kuwa alitukanwa na Heche kwa kutoa mfano hata moja tu wa hayo matusi..?

Kama kuambiwa apumzike kwa kuwa amechoka kuongoza chama ambacho alikuwa anakipoteza mdogo mdogo ni kutusiwa, basi na mimi namwongezea mapipa matatu yaliyosheheni ujumbe wa namna hiyo...!!
Halafu walipofanikiwa Heche akanza Kumwita Mwenyekiti wetu Mungu akubariki sana kwa kazi kubwa ulioifanya CHADEMA!
Hii ni kweli...

Huu ni kweli usio na ubishi kabisa, kwamba alikuwa mwenyekiti wao, mwenyekiti wa John Heche...

Kuna kosa hapo?
 
Nyerere mwenyewe hata baada ya kustaafu, aliendelea kupaza sauti kupinga maovu ya watala. Sasa huyu anae kaa kimya licha ya madudu yote yanayoendelea ni mwanasiasa kweli wa kutetea dhulumu na uonevu dhidi ya wananchi?

Hata kuandika tu chochote ameshindwa?

Bora hata Askofu Bagonza na wengineo kuliko Mbowe.

Yeye alipowekwa ndani wenzake walikaa kimya?

No wonder alimuokoa Masauni kwenye msiba wa Mzee Kibao ila uzuri Lema alimpa ukweli wake.
Ni upumbavu kumlazimisha mtu afanye kitu unachotaka wewe. Mnataka kuingilia uhuru wa mtu kwa siasa zenu za majitaka. Ukimya wa Mbowe utawatesa mno.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Huyu Hapa Mwamba Na Jabali la Siasa za Upinzani hapa Nchini Mheshimiwa Freeman Mbowe Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA na kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni. Mtu aliyekuza na kuibua vipaji vya vijana wengi sana hapa Nchini. Mtu aliyekuwa na moyo wa uvumilivu, upendo,ustahimilivu ,subira na kuupa muda nafasi.

Ni mtu aliyezijua siasa za Upinzani,mtu aliyejua namna ya kudhibiti Mihemuko ya vijana wake,mtu aliyejua kusaka vipaji,kuendana na vijana wa kizazi hiki. Mtu aliyejua maana ya siasa siyo uadui,mtu aliyejua Kuna wakati kunahitaji kukaa mezani na kufanya mazungumzo .

Ni mtu aliyetumia muda wake mwingi, pesa zake,mali zake , rasilimali zake na Maisha yake yoote kuijenga CHADEMA na kuifikisha hapo ilipo. Alikuwa ni Daraja la matumaini kwa vijana na watu wengi wenye ndoto za uongozi kwa Nchi hii kwa ngazi za udiwani na Ubunge. Alikuwa ni Mwalimu wa siasa za Upinzani,alikuwa mfano halisi wa mtu aliyekomaa kiakili na kumudu siasa za upinzani.

Alijua kujitawala jukwaa,alijua kuteka mioyo ya Wafuasi wake ,alijua kupanguilia maneno yake ,alijua nini anakifanya. Leo yupo pembeni ,leo yupo kanda ,leo yupo na Mambo yake ,leo yupo Nje ya uongozi lakini kimvuli chake kingalipo ndani ya CHADEMA,bado unaona nafasi yake na sauti yake ilihitajika kuendelea kuiongoza CHADEMA.

Alikuwa na moyo wa unyenyekevu katika ubinadamu wake ,alikuwa na moyo wa kusamehe na kusonga mbele. Aliweza kukaa mezani na yeyote yule na kuungana na yeyote yule katika kukijenga chama chake alichokijenga kwa jasho na Damu katika ujana wake wote mpaka umri alionao kwa sasa.

Waliofanya maamuzi ya Mihemuko na kukurupuka leo hili wanajutia maamuzi yao na wanatamani muda urudi nyuma na wampigie kura za ndio kwa kishindo kikuu. Leo wanatamani afungue hata kinywa chake ili azungumze nao ,leo ukimya wake unawatesa wana CHADEMA wote waliomtusi na kumuumiza kwa maneno ya kejeri na dharau pamoja na kumdhalilisha.

Leo chama kimeshikwa na watu wasio na muelekeo wala Dira wala maono. Chama kinakwenda kama kipofu gizani au gari lililokatika breki. Chaka kinaendeshwa kilevi kilevi tu. Kila siku chama kinaendelea kupoteza nuru na mpaka sasa hakina ushawishi hata wa kuweza kupata wagombea wa kusimama majukwaani kuomba kura.

Watanzania nimewaleteeni somo hili ili mjue na kuogopa kufanya maamuzi ya kukurupuka. Tumieni haki yenu na kikatiba kuhakikisha mwezi wa Kumi mnakwenda kwenye vituo vya kupigia kura kwenda kutiki kwa Rais Samia Suluhu Hasssan Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi pamoja na wagombea wote wa ngazi za ubunge na udiwani watakaokuwa wamesimamishwa na CCM.View attachment 3389496View attachment 3389498View attachment 3389500

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
WEWE NI MNAFIKI SANAA WEE JAMAAA ,SIJUI TUNAISHIJE MTOTO WA KIUME KINAA ,MBOYE ALIPOKUWA NA KESI YA UGAIDI ULIJITETEA UKASEMA NI GAIDI ,SASA LEO HANA CHEO KABISA UNAMSIFIAA ETI MWAMBA WA SIASA ,AKILI KAMA KISHUNGII WEWE
 
Ndugu zangu Watanzania,

Huyu Hapa Mwamba Na Jabali la Siasa za Upinzani hapa Nchini Mheshimiwa Freeman Mbowe Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA na kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni. Mtu aliyekuza na kuibua vipaji vya vijana wengi sana hapa Nchini. Mtu aliyekuwa na moyo wa uvumilivu, upendo,ustahimilivu ,subira na kuupa muda nafasi.

Mtu aliyetumia mikono yake kuwalea ,kuwavusha na kuwafungulia njia vijana wengi sana hapa Nchini. Mtu aliyewabeba vijana mabegani mwake na kuwapeleka ng'ambo ya pili ya mto,mtu aliyekuwa na chemchemi ya upendo kifuani kwake kwa vijana. Mtu aliyeinua vijana wengi na kuwapa majukwaa ya kuzungumza na wananchi,mtu aliyewatambulisha vijana wengi katika anga la siasa za nchi hii.

Ni mtu aliyezijua siasa za Upinzani,mtu aliyejua namna ya kudhibiti Mihemuko ya vijana wake,mtu aliyejua kusaka vipaji,kuendana na vijana wa kizazi hiki. Mtu aliyejua maana ya siasa siyo uadui,mtu aliyejua Kuna wakati kunahitaji kukaa mezani na kufanya mazungumzo .

Ni mtu aliyetumia muda wake mwingi, pesa zake,mali zake , rasilimali zake na Maisha yake yoote kuijenga CHADEMA na kuifikisha hapo ilipo. Alikuwa ni Daraja la matumaini kwa vijana na watu wengi wenye ndoto za uongozi kwa Nchi hii kwa ngazi za udiwani na Ubunge. Alikuwa ni Mwalimu wa siasa za Upinzani,alikuwa mfano halisi wa mtu aliyekomaa kiakili na kumudu siasa za upinzani.

Alijua kulitawala jukwaa,alijua kuteka mioyo ya Wafuasi wake ,alijua kupangilia maneno yake ,alijua nini anakifanya. Leo yupo pembeni ,leo yupo kando ,leo yupo na Mambo yake ,leo yupo Nje ya uongozi lakini kimvuli chake kingalipo ndani ya CHADEMA,bado unaona nafasi yake na sauti yake ilihitajika kuendelea kuiongoza CHADEMA.

Alikuwa na moyo wa unyenyekevu katika ubinadamu wake ,alikuwa na moyo wa kusamehe na kusonga mbele. Aliweza kukaa mezani na yeyote yule na kuungana na yeyote yule katika kukijenga chama chake alichokijenga kwa jasho na Damu katika ujana wake wote mpaka umri alionao kwa sasa.

Waliofanya maamuzi ya Mihemuko na kukurupuka leo hili wanajutia maamuzi yao na wanatamani muda urudi nyuma na wampigie kura za ndio kwa kishindo kikuu. Leo wanatamani afungue hata kinywa chake ili azungumze nao ,leo ukimya wake unawatesa wana CHADEMA wote waliomtusi na kumuumiza kwa maneno ya kejeri na dharau pamoja na kumdhalilisha.

Leo chama kimeshikwa na watu wasio na muelekeo wala Dira wala maono. Chama kinakwenda kama kipofu gizani au gari lililokatika breki mteremkoni .Chama kinaendeshwa kilevi kilevi tu. Kila siku chama kinaendelea kupoteza nuru . na mpaka sasa hakina ushawishi hata wa kuweza kupata wagombea wa kusimama majukwaani kuomba kura.

Watanzania nimewaleteeni somo hili ili mjue na kuogopa kufanya maamuzi ya kukurupuka. Tumieni haki yenu ya kikatiba kuhakikisha mwezi wa Kumi mnakwenda kwenye vituo vya kupigia kura kwenda kutiki kwa Rais Samia Suluhu Hasssan Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi pamoja na wagombea wote wa ngazi za ubunge na udiwani watakaokuwa wamesimamishwa na CCM.View attachment 3389496View attachment 3389498View attachment 3389500

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
FB_IMG_1748360197313.jpg
 
WEWE NI MNAFIKI SANAA WEE JAMAAA ,SIJUI TUNAISHIJE MTOTO WA KIUME KINAA ,MBOYE ALIPOKUWA NA KESI YA UGAIDI ULIJITETEA UKASEMA NI GAIDI ,SASA LEO HANA CHEO KABISA UNAMSIFIAA ETI MWAMBA WA SIASA ,AKILI KAMA KISHUNGII WEWE
Ulifundishwa na nani ujinga wa kuandika kwa herufi kubwa maelezo yako?
 
Back
Top Bottom