PICHA: Freeman Mbowe katika uso wa tabasamu na furaha kubwa hii leo Juni 30, 2025

Uwe na heshima kwa mtu aliyejitolea muda na mali zake kukijenga chama. Ona akina lissu na heche wameingia tu wakaanza michango muda wote kwa ajili ya kuhudumia matumbo yao.
Tuliza wengeee gombea wewe uchangiwe na uchawa wako wa kimbozi mbozi kama ni rahisi kuchangiwa
 
Ndugu zangu Watanzania,

Huyu Hapa Mwamba Na Jabali la Siasa za Upinzani hapa Nchini Mheshimiwa Freeman Mbowe Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA na kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni. Mtu aliyekuza na kuibua vipaji vya vijana wengi sana hapa Nchini. Mtu aliyekuwa na moyo wa uvumilivu, upendo,ustahimilivu ,subira na kuupa muda nafasi.

Mtu aliyetumia mikono yake kuwalea ,kuwavusha na kuwafungulia njia vijana wengi sana hapa Nchini. Mtu aliyewabeba vijana mabegani mwake na kuwapeleka ng'ambo ya pili ya mto,mtu aliyekuwa na chemchemi ya upendo kifuani kwake kwa vijana. Mtu aliyeinua vijana wengi na kuwapa majukwaa ya kuzungumza na wananchi,mtu aliyewatambulisha vijana wengi katika anga la siasa za nchi hii.

Ni mtu aliyezijua siasa za Upinzani,mtu aliyejua namna ya kudhibiti Mihemuko ya vijana wake,mtu aliyejua kusaka vipaji,kuendana na vijana wa kizazi hiki. Mtu aliyejua maana ya siasa siyo uadui,mtu aliyejua Kuna wakati kunahitaji kukaa mezani na kufanya mazungumzo .

Ni mtu aliyetumia muda wake mwingi, pesa zake,mali zake , rasilimali zake na Maisha yake yoote kuijenga CHADEMA na kuifikisha hapo ilipo. Alikuwa ni Daraja la matumaini kwa vijana na watu wengi wenye ndoto za uongozi kwa Nchi hii kwa ngazi za udiwani na Ubunge. Alikuwa ni Mwalimu wa siasa za Upinzani,alikuwa mfano halisi wa mtu aliyekomaa kiakili na kumudu siasa za upinzani.

Alijua kulitawala jukwaa,alijua kuteka mioyo ya Wafuasi wake ,alijua kupangilia maneno yake ,alijua nini anakifanya. Leo yupo pembeni ,leo yupo kando ,leo yupo na Mambo yake ,leo yupo Nje ya uongozi lakini kimvuli chake kingalipo ndani ya CHADEMA,bado unaona nafasi yake na sauti yake ilihitajika kuendelea kuiongoza CHADEMA.

Alikuwa na moyo wa unyenyekevu katika ubinadamu wake ,alikuwa na moyo wa kusamehe na kusonga mbele. Aliweza kukaa mezani na yeyote yule na kuungana na yeyote yule katika kukijenga chama chake alichokijenga kwa jasho na Damu katika ujana wake wote mpaka umri alionao kwa sasa.

Waliofanya maamuzi ya Mihemuko na kukurupuka leo hili wanajutia maamuzi yao na wanatamani muda urudi nyuma na wampigie kura za ndio kwa kishindo kikuu. Leo wanatamani afungue hata kinywa chake ili azungumze nao ,leo ukimya wake unawatesa wana CHADEMA wote waliomtusi na kumuumiza kwa maneno ya kejeri na dharau pamoja na kumdhalilisha.

Leo chama kimeshikwa na watu wasio na muelekeo wala Dira wala maono. Chama kinakwenda kama kipofu gizani au gari lililokatika breki mteremkoni .Chama kinaendeshwa kilevi kilevi tu. Kila siku chama kinaendelea kupoteza nuru . na mpaka sasa hakina ushawishi hata wa kuweza kupata wagombea wa kusimama majukwaani kuomba kura.

Watanzania nimewaleteeni somo hili ili mjue na kuogopa kufanya maamuzi ya kukurupuka. Tumieni haki yenu ya kikatiba kuhakikisha mwezi wa Kumi mnakwenda kwenye vituo vya kupigia kura kwenda kutiki kwa Rais Samia Suluhu Hasssan Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi pamoja na wagombea wote wa ngazi za ubunge na udiwani watakaokuwa wamesimamishwa na CCM.View attachment 3389496View attachment 3389498View attachment 3389500

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Umesahau kububujikwa na machozi
 
Mbowe hana mvuto wowote kisiasa kwa sasa ndo maana hata kwenye chama chake alishindwa uchaguzi wa huru na haki huyo siasa zimempita
Mvuto gani unaoutaka wewe? Unaweza kushindana naye kwenye jimbo lake akitaka kugombea?
 
🤔 🤔 🤔
 
Back
Top Bottom