PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

HALI NI MBAYA......MA-GREAT THINKERS KUMBE MPO......THINK OUTSIDE THE BOX AND COME WITH SOMETHING
Remember TRUTH is everything.......are ready to accept the truth even if its agaisnt what we BELIEVE?
 
Hivi haya yote yanafanyika ili kutusahaulisha ya ULIMBOKA kule Mabwepande au ni kitu gani?
wanajisafisha kwa Damu isiyohatia!!
 

Acha Useng3 wewe Mbwa Koko wewe, watu tuna hasira na Mauaji mabwana zako wanayofanya, YOYR DAYS ARE NUMBERED, mark my words
 
Upuuzi huu, yani rpc alikiwa wapi ndo issue ya kuzungumzia sasa, sio mwandishi ameuwawa katikati ya kunfi la askari?

Kuna watu humu wanavutika kama bigijii.

Nasema tena, huu ni upuuzi, maneno ya dereva aliyekuwa kwenye gari na kujifanya alisikia marehemu alikuwa anaongea nini, kulinganisha na picha tena zaidi ya moja, ni upuuuzi wa hali ya juu.

Porojo tuu za mtaa wa gerezani, hakuna proof. Leteni uhakiki wa picha kwamba ni photoshop basi ili tujenge hoja, sio kuongelea rpc alikuwepo au hakuwepo kwa story za dereva tax.
 
Candid Scope nimesema nilichokisikia kupitia WAPO Radio kwenye kipindi cha Pata pata na ilikuwa ni mahojiano na RPC, Dereva wa waandishi habari na pia katibu wa Press Club ya Iringa na watu wengine.

Never mind ndugu yangu, cha maana ni riport nzuri iliyofanyiwa utafiti kamili ambayo imerushwa na ITV mmoja wapo wa waandishi akiwa mwadhirika wa kipigo cha polisi ndiyo inayotoa taswira ya kueleweka, vinginevyo katika motion ile kila mmoja alikuwa anatafuta njia yake bila record kamili ya tukio. Kurekodi tukio lile kunahitaji ujasiri na kati ya matukio mengi hili lina akisi ukweli wa mauaji ya polisi bila kisingizio cha silala kutoka kwa raia.
 
elewa hapa, rpc katoka wapi kwenye hii picha wakati maelezo yanasema alikuwa kwenye gari?

Mbona simple sana, rpc alishuka baada ya kuona mwangosi ashughulikiwi ipasavyo. Na walikuwa wanasubiri amri yake ya BOMU
 


OCD aliyeumia katika tukio na ambaye yuko critical condition hospitalini ni yupi katika kundi hili? Au huyo aliyevaa kiraia? Waliopo Iringa wanaweza kutupasha maana wanawajua watu wao.

Huyo aliyenyanyua juu fimbo naona ndiye OCD akiwakataza askari wasiendelee kumpiga Mwandishi wa habari ambaye amapiga magpti na kumkumbatia OCD asisulubiwe zaidi lakini nyuma katokea askari mwenye bunduki inayotumika kurushia mabomu ya kutolea machozi akamfyatulia tumboni, (kwa vile ina batuti pilipili na kopo/ganda linalotoka kwa hiyo ni Bomu ndilo lilomuua Daudi Mwangosi)
OCD alianguka na kuvunjika Mguu na kulazwa Hospital kwa hiyo utaona ukaribu wa ajali hiyo na huyo aliyekumbatiwa
Halafu linganisha hayo mavazi na mkoba wake vyote vinaonekana kwenye tukio la mauaji
Picha ya chini inaonyesha kuna baadhi ya Maswali alitupiwa RPC akashindwa yajibu ndio maana kuna maelezo ya dreva aliyewachukua waandishi anafunuka hapo chini



By Nyakwec's Bro

ALICHOKIFANYA RPC NI KUFUNGUA KIOO CHA GARI NA KUTAZAMANA SURA YAYE NA YULE ASKARI ALIYEKUWA AMEMUWEKEA SILAHA TUMBONI MAREHEMU KWANI WALIKUWA NI JIRANI TU NA KM AKAMUAMURU AFANYEKITU NDIPO DAUDI ALIPOSAMBARATISHWA ANASEMA YULE ASKARI
MWINGINE ALIYEJERUHIWA YEYE ALIKUWA ANAONYESHA KUMFAHAMU MAREHEM NA
ALIKUWA AKIWASIHI WAMUACHE,kisha dereva anasema walipoona wameua wakamuachia yule muandishi mwingine kisha wakaanza kuisonta gari yake yy alikuwa anaona kila kitu anasema ikabidi aliondoe gari lake na kama bahati bomu lilipigwa alipokuwa na bahati nzuri
Waandishi wote waliohojiwa walisema marehemu ameuawa huku policcm wakiwa wamemkumbatia
km picha zinavyoonyesha kwamba walikuwa nae ziro distance.
 
yote wa yote waliotenda wanAjua walichokitenda wametumwa kufanya hayo wamepewa baraka na watawala,watawala wanadhani itawasaidia wamepotoka. hivi ni kweli hakuna wakuwaadhibu hawa. je wanafahamu ni ukiwa wa kiasi gani wameleta kwa familia ya daudi, watoto wake, baba yake mama yake na ndugu zake. yote hii ili Kulinda maslahi yao na ya watoto wao. hapana kama MUNGU AISHIVYO HAWATAPONA WATAVUNA WALICHOPANDA.EE MUNGU WA MAJESHI SIKIA SALA ZA WATOTO NA MAMA MJANE HUYO.
halafu watakuja watu na poropaganda hapa wakisingizia chadema na mikutano yao, utafikiria CHAMA CHA MAJAMBAZI HAKIFANYI MIKUTANO YAO
 
hivi ulimsikia mandishi aliyeojiwa na itv? anasema wakati marehemu anapigwa rpc alikuwa kwenye gari

Naona tunapishana katika kuelewa! Hata Mimi miliamini kwa kuangalia hii mishale aliyemkinga marehemu ni RPC, lakini baada ya kusikia ushuhuda aw waandishi wale wawili ndani ya ITV saa 2 usiku, huyo hakuwa RPC bali Askari aliyeumizwa mwenye nyota tatu. Ndiye Alikuwa karibu zaidi na rahisi kuumizwa na milipiko iliyomuua marehemu. RPC aliona yote akiwa ndani ya gari. Alaaniwe!
 
Unajua wanachofanya hapa ni kutaka kuwaondoa watu katika mada ya MAUAJI YA POLISI. Jana zimewekwa picha zote kwa wakati mmoja na kila aliyeona tukio hakuna anayebisha hilo.

Nimesoma gazeti la mwananchi msemaji wa JESHI LA POLISI TANZANIA amekuja na madai ya kipumbavu na kijinga sana. Anasema Mwangos alikuwa anakimbia kutoka kundi la watu kuja kwa askari na kuna kitu kilirushwa kutoka kwa wananchi kikamuangukia tumboni.

Jeshi la Polisi linapoongoza kwa ujinga inatia wasi wasi. Ni ujinga kwasababu Msemaji wa jeshi hakujua kuwa picha zipo katika mtandao tayari. Sijui kama msemaji anajua hata key board ikoje achilia mbali kutafuta habari.
Matokeo ya kuwa na mazuzu kama hawa ni matumizi ya mabomu ya moshi kufumua watu.
Tayari amesha pre-empty uchunguzi wa IGP kwasababu tu idha ya mafunzo kidogo, au uweledi sifuri

Tatizo linalotukabili kama nchi ni ile tabia yetu ya kudhani kuwa ili uwe askari Polisi ni lazima uwe mjinga.
Tunajeshi lisilo na watu wenye uwezo kabisa. Imagine msemaji wa jeshi hajui nini kinaendelea katika nchi, je,askari aliye na risasi anajua kuitumia?

Jeshi la Polisi halina maana ya genge la watu wajinga au wapumbavu, halina maana watu wasiojua mazingira na mawasiliano.Jeshi la Polisi ni taaluma muhimu sana katika jamii kama taaluma zingine.

Kwakweli inauma sana! Niiweni radhi
Ifike wakati tuwe na jeshi la Polisi siyo wapuuzi, wajinga na mazuzu waliovaa uniform na kutoa roho za watu.
 
Mkuu Kimbunga,
Asante sana kwa swali lako. Maana yangu kuhusu ‘Chadema na Mileage' ni kwamba matukio kama haya yana faida zaidi kwa Chadema kuliko CCM regardless nani ana makosa katika hili kwani kwa mujibu wa Katiba ya nchi, serikali (ambayo tangia uhuru ipo chini ya TANU-CCM), ndiyo yenye mamlaka ya kuunda majeshi yote ya ulinzi na usalama, hivyo jukumu la kulinda usalama wa raia wote na mali zao bila ya kujali dini, kabila, jinsia, political orientation, occupation (ajira) n.k, ni ya majeshi ya ulinzi na usalama, jeshi la polisi likiwa ni moja wapo. Kwa mfano, katika sura ya tisa ya katiba yetu, ibara ya 147, [sehemu 1,2, & 3] inatamka kwamba:

(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote au shirika lolote au kikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote.

(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza, kwa mujibu wa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa Tanzania.

(3) Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.

Kwa maana hii, matarajio yetu kutoka jeshi la polisi ni kinyume cha yaliyotokea huko Iringa. Hata kama ilibidi jeshi litumie nguvu ya ziada, nguvu hiyo haina mahusiano na waandishi wa habari kwani kazi yao pale sio ushabiki wa siasa bali wao ni sikio la umma. Kama vile media wanapokuwa ni watu wa mwisho kuondoka kwenye press conferences, makongamano n.k, ilitakiwa iwe vivyo hivyo katika sakata la Iringa, na uwepo wa Polisi sana sana iwe kuwalinda waandishi wa habari na mali zao ili wakimaliza shughuli zao waondoke salama.

Lakini ukitazama the strained relationship iliyopo baina ya vyombo vya habari na jeshi la polisi kwa muda mrefu sasa, na pia the combative relationship iliyojitokeza baina ya CCM na Chadema in the context ya dhana za Nguvu ya Umma versus Amani na Utulivu, na vile vile given upepo wa kisiasa wa sasa nchini, in the final analysis juu ya tukio hili, ''Either Way', it is Chadema that gets more political mileage than CCM.

Sasa kuhusu maswali yako kwamba: (1) Who provides Chadema with the political mileage…, jibu langu ni ‘the political atmosphere in the country ambayo itaendelea to favour Chadema pengine mpaka uchaguzi mkuu ujao (2015);

Na swali lako la pili kuhusu mazingira ya kifo cha mwangosi kuwa ya utata, ni kweli, lakini sote tunatoa tu maoni yetu based on how mashahidi wanavyotujuza, na kwa vile we are both entitled to our own opinions, itabakia hivyo while we await for the facts kwani katika suala la facts, none of us is entitled. Lakini hata tukija pata the actual facts that gives an account of what happened, in totality,BADO it offers more political mileage for Chadema than CCM. That's the bottom line. Inawezakana majibu yangu yasiwe ya kuridhisha sana lakini ni kutokana na kuheshimu dhana ya kwamba We are all entitled to our own opinion but not our own facts.

Until then, tusubiri kupata 'Raw facts', not 'Processed facts';
 

Kwanza Makene hakuweka picha. Pili; ni kweli kuna makosa katika maelezo hayo ya picha. Kwa kadri ya maelezo ya wenyeji na mashuhuda, huyo askari mkubwa aliyekuwa anawazuia askari wadogo (hawakumtii) anaitwa Mwampamba. Ni ofisa nafikiri kama sitakosea nyota tatu.

Unaweza kuona jinsi marehemu Mwangosi alivyokuwa amemkumbatia kiunoni katika hali ya kutaka kujiokoa na kuomba msaada. Unaweza kuona kamera yake iko mikononi bado. Kuna ile picha nyingine inayoonesha mwili ulivyosambaratika, pembeni unaona begi la kompyuta yake. Come on, Mwangosi died on field...working! Where is that camera, where is that compyuta...confiscated or taken? Why and by whom? If not where are they?????????????????

Ofcourse kwa wale wanaomjua RPC Michael Kamuhanda, si huyo wala hawezi kuwa huyo aliyenyoosha fimbo.
 
Hivi tukio hili nalo linahitaji uchunguzi badala ya kuwaweka ndani wauwaji na RPC afutwe kazi na Rais pamoja na IGP wake?
 
Jamani watu tunashikwa vibaya huyo aliyeziwekea hizo picha majina analengo la kupotosha umma huyo mtu aliyesimama siyo rpc ni rco na ndiye askari aliyejeruhiwa katika tukio hata hapo inaonyesha wazi kwa jinsi alivyosimama na huyo muuaji akafyatua hilo bomu lazima ajeruhiwe na huyo rco ndiye aliyekuwa anaonekana kumfahamu marehem hivyo alikuwa akiwazuia wasiendelee kumdhuru,unaweza ukafananisha picha ya huyo aliyesimama na anayebebwa baada ya tukio na rpc utapata jibu huyo siyo rpc ni rco.rpc hapo hakuwepo alikuwa kwenye gari akitazama tukio.
Kwakweli ninasikitika sana kwa huyu mtu aliyeweka majina kwa kujua au kutojua bila kujua madhara yake ningekuwa ninauwezo wa kumlaani ningemlaani.
 
Uongozi usiotenda haki hauwezi kudumisha amani.

Uongozi usiotenda haki utakataliwa na wananchi!

Polisi mnaisaidia CCM kuondoka madarakani kwa uhakika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…