PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

Sababu ya kuzuia mkutano ilikuwa kupisha zoezi la sensa linaloendelea nchini nzima kwa hiyo katazo la mikutano lina apply hata zanzibar. Lengo la serikali ya CCM kuifanya chadema kionekane chama cha fujo lime backfire. Ni watu kama nyinyi mnaofananafanana ndiyo bado mmeshikilia hoja ya fujo. Kwa mwana ccm yeyote makini hawezi hata kidogo kufurahia kitendo hiki.
 
What kind of sicko would write something like this?
Mkuu, jaribu kuangalia post za Zomba na wale wote wanaoona kitendo cha polisi kuua raia kipo sawa. Utagundua wanaweza kuwa wanachama wa CCM au la lakini kuna kitu kinaweka pamoja kwenye msimamo wao especially linapokuja suala la CHADEMA. Waangalie vizuri sana hao jamaa kama akina Zomba wenye kutoa kejeli na kuwa na furaha kwa maafa ya wengine.
 
Eti walinzi wa Amani wakati wauaji wakubwa...wanatufanya tuendelee kujenga chuki juu yako...
 
Mbona umesahau kuweka picha ya Slaa , kwakuwa yeye ndio muanzilishi wa uhuni huu kwa kukaidi amri ya serikali. tuwekee na ya Slaa tafadhali.

Dr. (PHD) Slaa sio aliyelipua bomu lililomuua huyu mwandishi.
Dr. (PHD) Slaa hajaamuru uvunjaji huu wa haki za binadamu kwa raia ambaye hana hata wembe mfukoni akasulubishwa na askari wenye silaha zaidi ya 10.

Polisi hawana mbinu za kuthibiti watu, basi hata sinema hawaangalii wakaona wenzao how do they handle this cases? kutumia silaha ni last option kwa polisi, na hata ikitumika haitakiwi kumdhuru mhusika.

Polisi wameumbuka na mauaji yao wanayoyafanya kila siku. waseme sasa chadema ndio waliolipua bomu lililomuua marehemu. wauaji wakubwa hawa watu
 
Kaka weka hizo video za youtube acha kuogopa chochote kua jarisi baba
 
Je Bilal alifanya mkutano mkubwa wa uzinduzi siku hiyohiyo alikaidi amri ya nani?

Naomba niongezee hapo,

Matamasha ya FIEESTA yanayoendelea katika kipindi hiki cha sensa sio mkusanyiko wa watu? au huo mkusanyiko wa fiesta ni mkusanyiko wa viatu?

Kusanyiko linalokatazwa ni la CHADEMA tu au kusanyiko lolote?

POLI-CCM hawana cha kujitetea wauaji wakubwa nyie, sheria avunche CDM akivunja CCM na makundi mengine haijavunjwa? nyaaaaaau nyie POLICCM wote
 
Reactions: GP

LIKE nyingine mkuu wangu!
 
inawezekana polisi walikuwa na kisa na mwandishi huyu wakatumia fursa ya vurugu kutimiza azma yao.
 
Wanajamvi hivi ni lini hawa polisi wetu wa Tanzania watajifunza kutotumia mabavu kwa wananchi wasio na hatia wala silaha!

Huwa najiuliza huwa hawaoni pilisi wenzao wa nchi za wenzetu wanao jua haki za raia ni nini?

Ikiwa kuna fujo ama maadhamano ya sio na vibali polisi hawatumii nguvu bali wanajitahidi kuwatuliza ama kuwatawanya wananchi kwa maji (sio ya kuwasha) pia wanajikinga kwa ngao kuzuia mawe ana chupa yatakayo rushwa na wananchi na pindi wamkamatapo mhalifu humfunga pingu na kumandisha garini kumpeleka kituoni.

Tofauti ya hawa wa kwetu pindi wamkamatapo mhalifu humrukia kwa virungu na mateke kanakwamba wameona nyoka mwenye sumu kali akitaka kuwajeruhi.

Sasa najiuliza kule CCP Moshi huwa wanafundishwa kupiga wahalifu ama kukamata wahalifu.

Hao polisi wanapoiga wahalifu kanakwamba wameona chatu huwa hawana watoto ama ndugu wa damu pindi umpigapo mwenzio hivyo fikiria ni mwanao wa kumzaa anapigwa hivyo utajisikia vipi?

Polisi kazi yenu ni kulinda usalama wa raia sasa hapa ni usalama gani wa raia unalindwa ama ni kuondoa usalama na uhai wa raia!

Nadhani Jeshi la Polisi liitwe Jeshi la Kuondoa Uhai wa Raia na sio Jeshi la Usalama wa raia!
 
Shetani amefanikiwa kupandikiza roho za kishetani ndani ya jeshi la polisi. Wanamgombania mtu kama simba wanavyokuwa wanagombania mawindo yao!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Halsfu tunaomba huu upotoshaji wa Magamba na watumwa wao humu ndani ufe, Huyo kwenye picha sio RPC, huyo kwenye picha ni OCD aliyekuwa anajaribu kuwazuia hao Mbwa Koko wa Magamba wasimdhuru Mwangosi
 
Inatisha sana na kuhuzunisha.Wametumwa kufanya hivyo ili Watanzania waache kuhudhuria au kushiriki chochote kinachofanywa na wapinzani. Pia kila Polisi wasemacho tutii bila shurti. Ujumbe umefika na wote wanafurahi wakiona picha yao imeonekana pembe zote za dunia. MTAOGOPA 2015.
 
Kwa hali ilivyo sasa katika Jeshi la Polisi, inaniaminisha kuwa Polisi hawapo kwaajili ya kuwalinda Raia na Mali zao bali wapo kwaajili ya Kuilinda CCM na Mafisadi wake, na mali zao na watoto wao. Lakini kama hali ni hii sisi raia tutajilinda wenyewe.
 
RIP Ndugu mwandishi. Hii haiwezekaniki kutetewa. Ni lazima watu wawajibike
 
Nakumbuka nilivyokuwa kijana mdogo, kulikuwa na kipindi cha Jeshi la Polisi Radio Tanzania ambacho kilikuwa kinatumika kutoa elimu kuhusiana na masuala mbalimbali ya Polisi kwa umma. Wimbo uliokuwa ukipigwa kabla kipindi kuanza ulikuwa na maneno haya

'Jeshi letu, la Polisi, ni chombo cha wananchi. Usalama wa raia ndio kazi ya jeshi letu'

Jeshi hili halina ujasiri tena wa kuurudia huu wimbo kwa hali ilivyo sasa! Inauma sana.
 
Life is the most basic human rihgt. If justice means anything at all it must protect life.that should be a constant underlying purpose of all social economic and political activities of any state since fundamental rights are not gift frome state.they inhere in a person by reason of his/her birth and are therefore prior to the state and the law
 
kweli inauma sana ukiangalia walidhamilia hakukuwa na mtu yeyote na yeye alikuwa peke yake tu. ina maana waliua kwa makusudi kabisa
 
Inaleta hasira sana pale serikali kupitia hilo jeshi la polisi inahusika kwenye hili, kwanini hata kama uchunguzi unaendelea suspects wasikamatwe? Yaani huyo kaka wa watu aliyekuwa na familia yake inamtegemea tena alikuwa akifanya kazi yake, leo ameondoka kwa kifo cha unyama vile...Ni huruma jinsi gani mkewe, watoto na ndugu zake wameumizwa kwa hili tena wakiona hizo picha na wahusika wanadunda tu kazi kupindisha habari. Na kwa taifa zima inaumiza kujua unyama kiasi hiki unatendeka kweupe lakini wahusika hawachukuliwi hatua ipasavyo.
I hate this stup.i.d. government!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…