PICHA: Hii biashara ya usafirishaji wahamiaji inafanywa na matajiri wakubwa wenye connection na vigogo

PICHA: Hii biashara ya usafirishaji wahamiaji inafanywa na matajiri wakubwa wenye connection na vigogo

Kongo kwa barabara hamna kitu kutoka dar mfano kwa barabara kama unataka kwenda Kinshasa utatumia miezi mitatu

Tanzania haikwepeki kwenye safari yao ya kwenda South Africa sababu wakitaka kupitia kongo lazima wapitie Kenya Uganda halafu waingie Eastern kongo kwenye waasi kama wote wataporwa kila walichonacho wakiweza ndio wasafiri hadi lubumbashi

Wasomali wanakuwa na passport waethiopia hamna

Tanzania pia ni wahanga hili swala watanzania kibao wanakamatwa Afrika kusini hawana passport sababu ya ugumu kupata wanarudishwa nchini asante kwa mahakama huwapiga faini ndogo elfu 50 na kuwaachia faini ambayo ni ndogo kuliko bei ya passport kama serikali ingewapa bila longolongo asante mhimili wa mahakama kujitambua na kutambua changamoto ya waomba passport wanapata na kuwapa hukumu ya huruma

Mahakama mbariiiwe
Watanzania wengi wanaoishi South Africa Kwa sasa Wana Passport, coz Kuna Utaratibu pia wa ku apply Passport mpya ukiwa huko huko kupitia Ubalozi wa Tanzania hapo Pretoria.

Kinachofanya Watanzania wengi kukamatwa na kurudishwa ni Kwa sababu wame overstay....! Free Visa ni kuanzia mwezi 1 mpaka 3, Sasa muda ukiisha Kwa sababu za Maisha wengi hushindwa kwenda ku renew, mfano mtu anaishi Cape town, inabidi asafiri Boda ya jirani labda Namibia, ni masaa kadhaa, gharama za safari n.k Watu wengi wanaamua kuendelea na Maisha Yao, siku akikamatwa, Passport anayo lakini anakua ame overstay, kama huna pesa utaenda Jela na utarudishwa Bongo.
 
Kwenye Sector ya usafiri kuna Ma mafia wengi sana. I just saw picha ya gari la mzigo tena loose cargo inasafirisha wahamiaji haramu nikashangaa sana.

Yaani gari ukiona mzigo ni bomba za maji zimewekwa kwa kichanja. Ila ndani kuna chumba raia wamepumzika wanasafiri na maisha yanaendelea.

Sasa ukisikia BEI ya kusafirisha kichwa kimoja ndo utajua kwanini wanene ndo wanapiga hizi kazi. Chuma imekula Raia 62 ndani Yani inakimbizana na uwezo wa Bus kubeba abiria na huwezi hisi.

Aliyegundua hili nafikiri kuna namna anahusika hapa maana huwezi fikiria kwa akili hizi za Kizimkazi festival.

Anyway video ya wasafi iko hapo chini angalie ujionee wenyewe kwa undani zaidi.

Huyu dogo mbele kushoto mara ya 3 hii anakamatwa na kuwa deported back lakini hakomi, yani kila wakikamatwa baada ya mwaka miaka 2 unamuona tena
 
Back
Top Bottom