Mkuu...! Kwa Mwafrica ukiwa na Passport na unasafiri toka Nchi Yako na unapita Nchi kama 3 mpaka kufika unapokwenda, huitaji kuomba Visa Kwa kila Nchi unayopita, wewe unajurikana kama ni TRANSIT, ukifika Boda unaulizwa unakokwenda, kama unapita tu kwenye Hiyo Nchi, unawaambia wewe ni TRANSIT.
Watakupa siku hazizidi 7, kwamba Kwa vile wewe ni TRANSIT na unapita tu kwenye Nchi Yao, ndani ya siku hizo uwe umevuka tayari, otherwise wakikukuta ume overstay ni Jela.
Lakini sio Kwa Hawa Wasomali, Hawa wapo Transit tu...!
Labda kama Kuna Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Ethiopia kuwakamata kila Waethiopia wanaopita hapa.