bitimkongwe
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 7,794
- 7,551
Ndiyo kawaida ya binadamu ukiwa mgeni sehemu fulani unajitahidi kujikomboa kiuchumi. Utafanya kazi yoyote alimradi mkono uende kinywani. Hii ni tafauti na wenyeji wa eneo husika utakuta wametulia na maisha wala hawaoni fursa zilizoko.Waasia wengi babu zao waliingia na idea za biashara. Waliuza meno ya tembo, madini na ngozi za wanyama na waliingiza sukari, nguo, mchele, unga wa ngano, sabuni na mafuta yote.