Picha: Inawezekana kujenga nyumba kwa Design hii kwa milioni 16?

Picha: Inawezekana kujenga nyumba kwa Design hii kwa milioni 16?

Naona watu wameshindwa kumuuliza muhusika swali la msingi kwamba hilo jengo anajengea wapi?

Ujenzi wa mji kama wa Dar huwezi kuufananisha na wa Mbeya,gharama zinazidiana mkoa kwa mkoa.
Inajengwa Dar (Mbweni)
 
Muhimu si nikujua kwamba nyumba ni ya vyumba viliwili, sitting room labda na public toilet...kuna Cha ziada?
Kila mtu na fani yake, kiufupi hapo hatuwezi kujua kitu, ramani ya ndani ndo kila kitu!
 
Hii ramani kali sana, nimeipenda ni nyumba ya vyumba viwili, nimeitoa huko Twitter kwa mnigeria, mwenyewe anadai anaweza kukujengea nyumba kama hiyo ya kwa Naira milioni 5 tu ambapo hiyo ni sawa na milioni 15 na laki 9 kwa pesa za kibongo (15,907,496.08)

Yule jamaa kama ni kweli anaweza kujenga hiyo nyumba kwa kiasi hicho Cha pesa basi atapata wateja wengi sana maana nimeona watu wengi wamemuomba mawasiliano yake japo wapo watu walio doubt kwamba ni japo lisilowezekana.

Halafu pia kwenye Comment Section kupitia hiyo tweet yake nimeona jamaa Kasema kwao mfuko mmoja wa cement ni Naira 8,400 ambayo ni sawa na Tsh 26,700, hiyo ni gharama kubwa sana ukilinganisha na bei ya huku kwetu ambayo inachezea kwenye 16,500 hadi 18,000 je kwa fact hiyo inawezekana kushusha mjengo kama huo kwa milioni 16 pekee

Eniwei, Mimi nimeipenda hiyo ramani hata kama itanicost milioni 50 fresh tu ilimradi kitu kitoke kama kilivyochorwa hapo japokuwa jamaa kasema hiyo design ni best suitable for 2 bedroom ila Binafsi ningependa iwe 3 bedrooms hata kwa ku convert hiyo Car garage hiyo hapo chini to another room

Kuna Eng hapa Bongo anaweza modify hiyo ramani iwe 3 bedrooms instead of 2 bedrooms?View attachment 2683359
Bro 16 milioni haitoshi. Sisi ndio wenye mji.
 
Tutoe hiyo Garage tuweke room basi, sema jingine
Hiyo garage ipo chini ya room, ukibadilisha itakua ni room juu ya room, gharama ni zile zile. Otherwise hiyo room ya juu ije chini na juu pasiwe na kitu, hapo mil16 yako unajenga na kupaua
 
Inajengwa Dar (Mbweni)
Mimi siyo mkadiria majengo lakini kama ni huko ulikopataja hutoboi,labda kama utakuwa na wewe siku moja moja unachukua nafasi ya vibarua ili hela zisikutoke nyingi tofauti na hivyo hapana.
 
Mkuu hiyo ni picha tu. Hujapewa dimensions ili kujua size za vitu mbali mbali. Hujaambiwa materials gani yatatumika.

Hivi huwezi kujiuliza hayo maswali?
Ukubwa wa vyumba vya kawaida tu, na materials pia ya standard inaweza isiwe high quality lakini pia iswe low quality
 
Hiyo garage ipo chini ya room, ukibadilisha itakua ni room juu ya room, gharama ni zile zile. Otherwise hiyo room ya juu ije chini na juu pasiwe na kitu, hapo mil16 yako unajenga na kupaua
Aah basi tuache tu kama ilivyo, room ya juu ikija chini Design yote itabadilika

Hapo ni mawili, Either Garage ibebe room au room ibebe room
 
Ukubwa wa kawaida, I mean rooms zetu za kitanzania ambayo unaweza kuweka kitanda na kabati la nguo
Makadirio ni kwa kuangalia ramani ya nyumba nzima na vipimo sio picha ya upande mmoja
La sivyo kwa pesa hiyo inaweza tosha kama utatumia mchanga tu na cement kujengea
 
Kwani hiyo picha hadi imekaa hivyo si imetokana na ramani
Naona unapepelea sana, Hadi nahisi huenda wew ndiye mnufaika wa hiyo project. Samahani!
Labda tukuambie hivi, hiyo ni ghorofa, Si kila fundi atakujengea. Process zake ni ndefu pia
 
Mimi siyo mkadiria majengo lakini kama ni huko ulikopataja hutoboi,labda kama utakuwa na wewe siku moja moja unachukua nafasi ya vibarua ili hela zisikutoke nyingi tofauti na hivyo hapana.
Sasa nikichukua hiyo nafasi ya kibarua ambaye analipwa elfu 10 kwa siku ndio nitakuwa nimeokoa nini?
 
Mkuu amini kwamba jamaa amekuokoa....tengua kauli...
Sitengui na wala hajaniokoa chochote kwasababu nilikuwa sina Mpango wa kumfuata huyo mnigeria

Lengo ni kuuliza kama hiki kitu kinawezekana kufanyika hapa Bongo kwa bei hyo?
 
Back
Top Bottom