Vyumba viwili, ukubwa miguu 15 Kila upande
Sitting room na dinning ipo ukubwa wake wa kawaida tu
Kila chumba kiwe na choo then choo Cha public hakuna
Nakupa mfano,
1. Nyumba ya two bedrooms, dining, sitting, kitchen ina wastani wa 6windows, 6doors.
Tutengeneze grills sita kwa lowest price (dar), @90,000x6 = 540,000
Grills mbili za milango ya nje na vitasa vyake kwa lowest price @150,000x2 = 300,000
Tuweke aluminium 6 kwenye madirisha at a very low price kwa sasa @250,000x6= 1,500,000. Tuweke aluminium kwenye milango ya chooni, @200,000x2= 400,000
Tuweke milango ya nje miwili na vyumbani, standard panels kwa sasa ni around (bei ya chini)@450,000×4 =1,800,000. Milango na madirisha tu vinaweza kufika 4m kiwango cha chini.
2. Bati ni la kujificha, wastani wa bati 40 kwa design za kisasa na tuchukue mabati kwa bei za kizalendo @25,000×40 = 1,000,000, mbao za kench, 2x4 70 @ 5,500= 385,000 , 2x2 35 @2,500= 87,000.
Blundering 2x2 90 @2,500 = 225,000, misumari na ufundi utajua mwenyewe. Kupaua na ufundi wake fanya 3m makadirio ya chini.
3. Umeme c.pipe 80pcs @2,000(africab)= 160,000, kuna cable 2.5, 1.5, sockets, main switch 70,000, sq boxes za kutosha nk. Ufundi utajua mwenyewe. Ila materials na ufundi 1.5 hadi 2.5m inakata kutegemeana na materials ulizoweka, ukifunga ac tutarajie zaidi.
4. Plumbing materials na ufundi 1m inakata
5. Hatujazungumzia boma, plastering, gypsum board, skimming, tiles, rangi, maji ya kujengea(wengi hawaweki makadirio), landscaping, mashimo ya choo.
Umetaka kitu kizuri, 16m ni utani. Kwanza kuna slab humo.