Uchaguzi 2020 PICHA: Ingetokea kada wa CHADEMA ndiye angetinga hivi kwenye mkutano wa mgombea wa CCM, angetoka salama?

Ndiyo mnadamganyana na MATAGA wenzio,hamjui WANANCHI siyo wale wa Zama za mawe
 
Hawa masikini wanatumika kama chambo ili wakong'otwe tulete shida
 
Hata hivyo nadhani tusimhukumu bila kujua kwa undani alifuata nini kwa sababu wakati anasogea Mh. Tundu Lissu alikuwa anabamiza spana si mchezo. Yawezekana alikuwa kanogewa hivyo alikuwa anasogea karibu apate hizo nondo. Lakini pia tuwe tunachukua tahadhari hasa ninapokumbuka hii video hapa chini...

Your browser is not able to display this video.

Hawa vijana ni magaidi...
 

Kauli kali kabisa hii kutolewa hadharani ,CCM ni wauaji wakubwa na ukizingatia wana Serikali inakuwa yale yale ya Bashiru .
 
Hata club huwa yanaingia mamanzi hata mia hayana. Sasa kuondoa aibu ya kuchuniwa na kila mtu huwa yanajifanya kuongea na simu wakati kuna makelele kumbe yanazuga tu. Ndicho kilichotokea kwa hili jeba! Yani hapo lilijikuta kama liko uchi chekwaaaa sasa kuua soo likajifanya mara kupiga simu au kuwasiliana na mtu ili lionyeshe nalo ni somebody ni sawa na parcel tu! Usipate shida na hizi mbwa zetu koko inayobweka usiku ili kupata justification ya kutupiwa tonge la ugali.
 
Hata hivyo nimepatwa na wasiwasi huyu mtu nafikiri siyo salama. Hisia zangu tuu
 
Mbona hatuoni akiwasiliana na mtu??? Au unamaanisha huyo jamaa wa nyuma mwenye kofia nyekundu?
Wewe lazima utakuwa MATAGA, hebu jaribu kutumia akili kidogo...ama anaripoti kwa bosi wake Lumumba au kama ni katika wale wasiojulikana anawasiliana na bosi wa kikosi. Itazame kwa makini pia hiyo kofia, inakupa picha gani?
 
Hata hivyo nimepatwa na wasiwasi huyu mtu nafikiri siyo salama. Hisia zangu tuu
Alivyo mjinga, watu wameshamsoma kitambo. Hawa watu wanaotumiwa wakati mwingine ni zero brain, unajianika hovyo namna hiyo! Ama hivyo au kama alivyotoa wazo jamaa moja, anatafuta shari. Nikikumbuka ile cinema ya kihindi ya Mbatia, yawezekana kuna kitu kinasukwa. Chadema wawe makini sana.
 
Wewe lazima utakuwa MATAGA, hebu jaribu kutumia akili kidogo...ama anaripoti kwa bosi wake Lumumba au kama ni katika wale wasiojulikana anawasiliana na bosi wa kikosi. Itazame kwa makini hiyo pia hiyo kofia, inakupa picha gani?
Kwani MATAGA wamekufanyeje? Unaonekana unawaogopa sana
 
Huwa unajimwambafai kuwa na hekima lakini kwa hii post nimehitimisha mashaka yangu pasi na shaka yeyote juu yako.
 
Huwa unajimwambafai kuwa na hekima lakini kwa hii post nimehitimisha mashaka yangu pasi na shaka yeyote juu yako.
Acha kurukaruka jibu swali, Ingetokea kada wa CHADEMA ndiye angetinga hivyo kwenye mkutano wa mgombea wa CCM, angetoka salama?
 

YUVISISIEMU na lichama lao ni wakorofi,siasa hawawezi wamebakiza kufanya vurugu na kubebwa na NECCM na POLICCM tu.
 
Sasa nikabaki najiuliza, je hali ingekuwaje kama mwana Chadema ndiye angetinga katika mkutano wa CCM na magwanda yake halafu mara anapiga picha, mara kama vile anawasiliana na mtu, mara anajaribu kusogea na alipo mgombea...je kweli angetoka salama?
Kama sio chizi basi katumwa kama chambo kunasa samaki kwenye ndoana.

Kapelekwa hapo maksudi ili apate kipigo, na hiyo iwe sababu ya kudai CHADEMA wanatishia 'AMANI'; ile amani wanayoifahamu CCM na viongozi wao wa dini na IGP.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…