PICHA: Je Unaikumbuka Jambo Forums? Ulikuwa Wapi enzi hizo?

PICHA: Je Unaikumbuka Jambo Forums? Ulikuwa Wapi enzi hizo?

2006,2007,2008 muda huu mwingi nilikiwa guest, JF ilitawaliwa na mijadala ya kisiasa sana na mimi huwa naona siasa za TZ ni ujinga ujinga tu, chimbo langu lilikuwa kwa blogs za Ankal Michuzi, Mjengwa na jamaa mmoja hivi wa US alikiwa sijui DJ yule nimesahau jina lake (miaka hii blogs zilikuwa maarufu kuliko forums)...

2009 nilijiunga lakini baadaye nikasahau password, 2010 mwanzoni nikajiunga tena kuna jambo nilikuwa nataka nipush hapa kwa wadau...

Nilikuwa naingia sana kusikiliza miziki ya nyumbani, kulikuwa na embedded music player ilikuwa na collection ya zilipendwa na miziki mingine...

Wengi wa kitambo wataikumbuka hii interface...

View attachment 3204643
Hongereni sana aisee,.
Kweli tunatakiwa tuwe na adabu,. Kuna wazazi humu
 
Je Unaikumbuka Jamboforum?
Leo Kwenye Kufukunyua Makabuli kwenye Picha Zangu Nimekumbana na Picha Ya Mojawapo Ya Kurasa za JamboForum enzi Hizo Ambayo Kwa sasa ni Jamiiforum..

Ama Kweli Tumetoka Mbali, asante sana Maxence Melo kwa kutufikisha kwenye Maudhui Bora na Hakika Tumetoka Mbali sana..
View attachment 3204571
Nakumbuka kipindi natumia simu ya NOKIA EXPRESS MUSIC na BROWSER ya OPERA, basi kuload JAMBO FORUMS ilikuwa inanichukua zaidi ya dakika tano.. 😂
 
Watu tulianzia darhotwire ikapotelea mbali sema watumiaji wengi walikuwa watu waliyo mbele huko

Ova
Nimekumbuka mbali kweli; zama za Dar Hot Wire, Bongo 5.
Zama hizo jamaa wa Jahazi - Clouds FM karibia kila siku lazima waisakane Jambo Forum; wakiidhihaki kuwa ni jangwa forum.
Sikuwa nimejiunga, japo nilijiunga baadaye kidogo.
 
Back
Top Bottom