PICHA: Kazi ya Padre au Askofu ni kupatanisha sio katika siasa tu hata kwenye ndoa. Wanaoshangaa Dkt Kitima kuwapatanisha CHADEMA hao si wakatoliki

Rula ya Mafisadi

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2024
Posts
404
Reaction score
852


===
Kwanza, Nataka nyie msio wakatoliki mfahamu kuwa Mapadre na maaskofu wa Katoliki sio ngurumbili kama baadhi ya Viongozi wetu wengine wa dini hapa nchini.

Mapadre na maaskofu wa kikatoliki ni watu wasomi na wabobevu wakubwa katika maswala mbalimbali ya Kijamii kama siasa, Uchumi, Elimu etc

Kazi kubwa ya Padre au Askofu Mkatoliki kwa jamii ni kupatanisha sio katika siasa tu hata kwenye ndoa , Mirathi , biashara na mafarakano mengine yoyote,

Wanaoshangaa Padre Dkt Kitima wa TEC kuwapatanisha CHADEMA hao si wakatoliki kwani hakuna jambo la kushangaza hapo.


Hongera sana Father KITIMA kwa kutafuta amani ndani ya Wakristo wenzako wanaoitwa WanaChadema huko ni kuyaishi maneno ya kristo

Ukisoma kitabu kitakatifu Cha mwinjili ya Mathayo 5:9 Yesu mwenyewe amefundisha hivi,
"Heri wapatanishi, Maana hao wataitwa wana wa Mungu"

Au kwa kimombo "Blessed are the peacemakers: for they shall be called the children of God"



Nchi ngumu sana hii, Maaskofu wakipatanisha kati ya Freeman Mbowe na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inakuwa sawa, ila wakipatanisha kati ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu inakuwa nongwa. Hii imekaaje?
 
Ni watu wasioelewa wanaweza mdhambulia kitima
 
Namkubali sana father Kitima
 
Kitima anastahili pia kupatanishwa kwa vitendo viovu na vichafu kwa wanafunzi wa sauti mwanza,ndipo sasa na yeye apatanishe wengine
 
Kichwa cha habari kibadilike siyo Wakatoliki bali WAKRISTO. YESU anaeaminiwa na wakristo wote kwenye moja ya ile injili ya kheri, Matahayo sura 5 ; anasema kher wapatanishi, maana hao .....
 
Kitima apewe uaskofu na awe kadinari
 
kupatanisha watu ni ibada takatifu ya kumtukuza Mungu, na kufarakanisha watu ni ibada ya Shetani.
fr.kitima amefanya kazi ya Mungu. apongezwe.
 
Mathayo 5:9
[9]Heri wapatanishi;
Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
Blessed are the peacemakers: for they shall be called the children of God.
 
Acha porojo bwana mkubwa kama huna Cha kuandika kuhusu father kitima
wewe huwezi kumjua kama navyomjua mimi,tuishie hapa tu kwakuwa mimi naheshimu dini sana,lakini huyo mtu,ni wengi wanamjua undani wake,kama wewe humjui basi ni busara ukae kimya tu
 
Singida bwana ina wasomi wachache lakini ni moto wa kuotea mabali,huyu Fr.Kitima ni kichwa balaa.ukimweka Lisu na kuna Mwingine anaitwa professor MKHANDI anafundisha polical science Hurvad university
 
Singida bwana ina wasomi wachache lakini ni moto wa kuotea mabali,huyu Fr.Kitima ni kichwa balaa.ukimweka Lisu na kuna Mwingine anaitwa professor MKHANDI anafundisha polical science Hurvad university
Kitima ni balaa na nusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…