Rula ya Mafisadi
JF-Expert Member
- Dec 28, 2024
- 404
- 852
===
Kwanza, Nataka nyie msio wakatoliki mfahamu kuwa Mapadre na maaskofu wa Katoliki sio ngurumbili kama baadhi ya Viongozi wetu wengine wa dini hapa nchini.
Mapadre na maaskofu wa kikatoliki ni watu wasomi na wabobevu wakubwa katika maswala mbalimbali ya Kijamii kama siasa, Uchumi, Elimu etc
Kazi kubwa ya Padre au Askofu Mkatoliki kwa jamii ni kupatanisha sio katika siasa tu hata kwenye ndoa , Mirathi , biashara na mafarakano mengine yoyote,
Wanaoshangaa Padre Dkt Kitima wa TEC kuwapatanisha CHADEMA hao si wakatoliki kwani hakuna jambo la kushangaza hapo.
Hongera sana Father KITIMA kwa kutafuta amani ndani ya Wakristo wenzako wanaoitwa WanaChadema huko ni kuyaishi maneno ya kristo
Ukisoma kitabu kitakatifu Cha mwinjili ya Mathayo 5:9 Yesu mwenyewe amefundisha hivi,
"Heri wapatanishi, Maana hao wataitwa wana wa Mungu"
Au kwa kimombo "Blessed are the peacemakers: for they shall be called the children of God"
Nchi ngumu sana hii, Maaskofu wakipatanisha kati ya Freeman Mbowe na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inakuwa sawa, ila wakipatanisha kati ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu inakuwa nongwa. Hii imekaaje?