Mkuu, kuna namna mtu akifanya anakua bora kuliko jana katika muktadha wa utu (siyo uchumi, utu) mojawapo ni namna ya kujua kuwasiliana na wanaomzunguka.
Mfano: Wewe waweza kua una akili kunizidi na mimi ninajua kua umenizidi akili lakini ikatokea siku ukaniambia "Castr nimekuzidi akili" ujue wazi sitafurahia hiyo kauli ingawa ni kweli na ninajua kua ni kweli.
Watu wengi wenye madaraka wanakwama hapo, kuanzia baba mwenye nyumba, bosi ofisini, kaka yako, wabunge, mawaziri n.k.
Na hapo tu kwenye communication ndiyo kumesababisha watu waone sawa Mwakyembe kutemwa "Nina degree nne siwezi kusikiliza ushauri wa la saba" na Makonda (Ana kauli nyingi ambazo alilenga zidisplay ni namna gani hayupo level moja na anaowaongoza/ anaowatawala.
Mkapa amefariki atakumbukwa kwa mengi umeona jingine ambalo watu wanamkumbuka nalo? Neno malofa na wapumbavu. Na hili alitamka mwanadiplomasia.
Hivyo wewe hapa utaweza hisi anachukiwa kisa nyota, kisa madawa, kisa akili n.k. lakini mzizi upo hapo. Amina Chifupa alipigania drugs pia uliwahi sikia anachukiwa?
Anyway usiku mwema.