Picha: Mbunge wa Mlimba akikagua Daraja la Sh. Milioni 31 lilojengwa kwa miti
🤣🤣🤣🤣

Baada ya igizo la chanjo jana hili nalo ni igizo jingine.
 
Wangewapigia magoti JWT wawawekee daraja la chuma kwa mda kuliko huo ujinga. Halafu mmeenda na kamati ya siasa kukagua huku mnalipwa posho zitokanazo na tozo zakizalendo. Halafu mnasema tunapiga KELELE
 
PICHA YA SIKU: Hili ni Daraja jipya katika Mto Mngeta uliopo katika mji wa Mlimba wilayani Kilombero.

Daraja hili limejengwa kwa miezi 7 kwa thamani ya shilingi milioni 31, na limejengwa kwa miti.

Pichani ni mbunge wa jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi, akikakagua mradi.

View attachment 1872581
Ukweli ni kwamba hapa mahali panahitaji daraja makini ambalo kimsingi gharama yake ni kubwa, lakini Walau tupongeze hizi jitihada ndogo zilizofanyika wakati tunasubiri serikali itenge pesa kwa ajili ya ujenzi wa daraja la kudumu.

Kwa hizo mbao na si miti kama ulivyongea ni za gharama sana naona mninga umewekwa darajani.

Kinachotakiwa ni uwekwaji wa miti ya pembeni kuzuia ajali zisizo lazima.
 
Mambo ya ajabu sana haya! Alafu ndo wanasema eti hamna hela kweli!! CCM tumewachoka hamna aibu jamani, kukagua daraja la miti miaka hii???? Watanzania nani katuroga? Tunahitaji katiba mpya!!
Katiba mpya itasaidia nini hapo? Ila hawa jamaa bhana miezi 7 daaraja la miti na ukaguzi wa Mh juu
 
Kunambi ni mtu makini sana ila kwa huu ukaguzi ni UTOPOLO amefanya.

Karne hii ya sayansi na technology unajenga daraja kwa miti? Wameshindwa kuweka column kila upande na beam? Daraja ambalo alizidi 15 meter unajenga kwa miti?
Gharama walizopoteza kumkamata Mbowe ambayo sio tija kwa taifa si wangewapa wanakijiji hao wajenge daraja.
 
SI walisema tozo zitaenda kujenga barabara na madaraja, mambo yenyewe ndo haya😀
 
Back
Top Bottom