Picha: Mbunge wa Mlimba akikagua Daraja la Sh. Milioni 31 lilojengwa kwa miti
Mods Uzi wangu unachambua gharama za Daraja

Nawatazama hao watu wawili nyuma, sijui wanateta kitu ambacho hata mimi nakiwaza. Haya Mafundi seremala na wataalamu wa mbao na miti mtuambie gharama ya vifaa hivyo, hela ya ufundi tutajumlisha baadaye.

Kama ni pesa yake binafsi tutamsamehe lakini kama ni hela ya mfuko wa Jimbo imetumika hapo basi kwa uelewa wangu nadhani TAKUKURU wasogelee eneo hilo.

Au wamenunua vifaa kwa njia ya simu na hela nyingine yote imeishia kwenye tozo?

- Pale Buza kwa Mpalange kama unapandisha Kilungule kuna vijana wa mtaani wamejenga kama hilo na wanachaji pikipiki Buku. Nao sijajua iliwagharimu Milioni ngap.

TUMEPIGWA

"Fikiria Mbunge aliyeingizwa bungeni kimabavu anapewa fedha za mfuko wa jimbo toka fedha za walipa kodi, anaenda kujenga daraja la mabanzi halafu anasema bila soni limegharimu 31M. Hakuna mamlaka za kuthibitisha wala nini. Sasa hivi yuko busy kwa wauza mbao anafoji risiti"- Magiri

E7cyoCwX0AE1Lej.jpg
 
Inawezekana ikafika gharama hiyo. Inategemea daraja lilipo, ufikaji wa materials, aina ya mbao zilizotumika.

Mlimba ni moja ya sehemu zenye barabara mbovu sana, kwa kuangalia tu hilo daraja, ni nadra sana magari kufika huko, hivyo hata upelekaji wa hizo mbao unaweza ukawa wa gharama kubwa sana
 
Milioni 31 halikuweza kuwa bora zaidi ya hapo?.

Kweli waliosema 'Mswahili ni ngozi ya taco haitakati hata kwa neko' hawakukosea (kwa Vijana wa sasa wasioijua neko ilikuwa ni sabuni fulani ya kinadada ya kun'garisha/kuchubua uso)
 
Hao ndugu zangu wandamba nawaonea hutuma sana,wanachagua wabunge wanaofanya vituko!

Aende kukagua umeme kama unawaka Kijiji cha Merera, kata ya Chita maana ni zaidi ya mwaka tangu wameweka nguzo bila kuweka nyaya za umeme.
 
PICHA YA SIKU: Hili ni Daraja jipya katika Mto Mngeta uliopo katika mji wa Mlimba wilayani Kilombero.

Daraja hili limejengwa kwa miezi 7 kwa thamani ya shilingi milioni 31, na limejengwa kwa miti.

Pichani ni mbunge wa jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi, akikakagua mradi.

View attachment 1872581
Katiba mpya muhimu Sana huu ujinga kabisa
 
Afu hapo kuna posho watalipana kwa ajili ya ukaguzi 🤣
 
PICHA YA SIKU: Hili ni Daraja jipya katika Mto Mngeta uliopo katika mji wa Mlimba wilayani Kilombero.

Daraja hili limejengwa kwa miezi 7 kwa thamani ya shilingi milioni 31, na limejengwa kwa miti.

Pichani ni mbunge wa jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi, akikakagua mradi.

View attachment 1872581
ukiwa chadema na akili huwaga zinaoza kabisa aliyekuambia zimetumika hizo hela ni nani? je kama wananchi wamejitolea kutengeneza kivuko chao cha muda wakisubiri serikali yao sikivu ya mtukufu rais samia iwajengee la kudumu je? najuwa nyie hamuwezi yaani mnasubiri mpaka mkinya na kutawazwa mtawazwe
 
Inawezekana ikafika gharama hiyo. Inategemea daraja lilipo, ufikaji wa materials, aina ya mbao zilizotumika.

Mlimba ni moja ya sehemu zenye barabara mbovu sana, kwa kuangalia tu hilo daraja, ni nadra sana magari kufika huko, hivyo hata upelekaji wa hizo mbao unaweza ukawa wa gharama kubwa sana
[emoji16]
Uko serious kabisa...[emoji3525][emoji3525][emoji3525]
 
Back
Top Bottom