Mtaani kulikuwa kuna kijana mmoja alikuwa anajihusisha na masuala ya sanaa za maigizo, sasa kikundi chao kwa pamoja waliamua kwenda kwa mganga ili kusafisha nyota zao waweze kung'aa kisanaa.
Walipokwenda kwa mganga walichanjwa chale,kisha wakapakazwa na usembe pamoja na dawa nyingine za kijadi kisha mambo mengine ya kijadi yakafuatiwa ambayo sitayaweka wazi hapa.
Baada ya muda wale vijana wakawa wamejiunga moja kwa moja na dini hiyo ya freemasons.
Cha kwanza kabisa walichoambiwa walitakiwa waende baharini usiku wa manane (kila mmoja kwa wakati wake(walikuwa watatu)),kisha waite majina yao mara tatu baada ya muda atatokea mtu sawa na huyo mtu aliyeita jina lake kisha huyo mtu atampa maelekezo yote na mambo yote yatakayotokea mbeleni.
Baada ya kufanya hivyo hatimaye wakawa wamejiunga kikamilifu na hiyo dini lakini mara nyingi walikuwa wanahudhuria vikao bila wengine kujua haswa nyakati za usiku ,kwa sababu wanaweza kwenda kulala kumbe jamaa wameenda mfano nchi jirani au nje ya mkoa japo kitandani walipolala miili yao ilikuwa inaonekana.
Wakifika huko mara nyingi walikuwa wanafanya biashara ndogo ndogo kwa njia za giza na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa mno kipesa.
Changamoto kubwa ilianza kutokea mara baada ya kufikia hatua ya kutakiwa kutoa sadaka.