Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
- Thread starter
-
- #81
Dada acha uongo unaota kwa kimalkia Elizabeth, serious?
Ama kweli hiki ndo kiswahili tunachojivunia kinakua kwa kasi na kitumike mh!!!!!shame on us.watarifanyia=watalifanyia
wakijilizisha=wakijiridhisha
Ha ha haYani kola kukaa vibaya ni kuvaa hovyo?
Ila ID yako imenipa majibu.
Hahahahahahah....umenifanya nirud kuangalia ID na kuishia kuvunjika mbavuYani kola kukaa vibaya ni kuvaa hovyo?
Ila ID yako imenipa majibu.
Shangazi FaizaFoxy naunga mkono bidii yako ya kusahihisha makosa katika matumizi ya lugha ya Kiswahili. Siku hizi neno "wimbo" linaitwa nyimbo. Waathirika wakubwa wa kosa hili ni vijana, hii ni ishara kuwa vijana hawajisomei au hawasomi vyanzo sahihi vya lugha fasaha.Akikuwa ataacha.
Mkuu mbona kama umemchukia dada wa watu, kola imekaa vibaya , pia kutojua mambo ya siasa wala mchezo si kigezo.
Kwa hiyo ulitaka aseme kavaa vizuri wakti hata wewe unaona kola imekaa vibaya? Kutokumwambia mtu ukweli ndiko kumpenda? Halafu unasema kutokujua siasa wala michezo si kigezo cha kufanya nini? Unajua maana ya taaluma na ufanyaji kazi wa kitaam? Kama hajui michnzo na siasa maana yake apishe wanaojua wafanye hivyo vipindi badala ya kuharibu muda wa azam na watazamaji.
Nikuambie ukweli, 'UNAFIKI UNAUA", "UJINGA NA DENI", UPUMBAVU NI LAANA", LAKINI "MAARIFA HUTAFUTWA", "UKWELI HUMPONYA MFALME".
Chizi Maarifa, kwanza naanza kutoa lawama kwa jina la utambulisho ulilotumia (ID). Linachangia sisi tukushambulie. Kati ya chizi na maarifa nafikiri chizi ndilo neno baya hivyo "kibinadamu" tutalichagua hilo baya badala ya zuri. Hivyo wewe ni Chizi.
Sasa kuhusu mada uliyoweka, sitazungumzia juu ya ufahamu wa mtangazaji au watangazaji bali kuhusu "kijikosa" kidogo katika uvaaji ambacho kwa sababu ya "uchizi" wako umekosa "maarifa" na kudhani kuwa hilo ni kosa kuuuubwa "kivile."
Dosari hiyo katika kola inaweza kusaidia kuonesha/kuonyesha udhaifu wa watu waliomzunguka huyo dada. Dosari hii, japo watu wanaichukulia poa lakini inajenga picha kuwa crew ya kipindi/programu husika (na hata AZAM TV yote) haiko makini. Kabla ya kwenda hewani kuna mambo kadhaa ya kujiridhisha ikiwa ni pamoja na mavazi, mwonekano, afya na utulivu wa akili wa mtangazaji. Kosa ama dosari ndogo inachangia kujega taswira pana (brand/image) ya kampuni, taasisi au bidhaa.
Ndiyo maana baada ya Mhe. waziri C. K. kuondolewa kwa kuzungumza akiwa "amelewa" lawama hazikuishia kwake tu bali hata kwa wasaidizi wake (hata dereva analaumiwa). Kaondolewa ili kulinda taswira (brand/image) ya uwajibikaji wa serikali mbali na kosa lenyewe la kulewa wakati wa muda wa kazi. Wabongo (Siyo wote) tumezoea sana mchezo wa bora liende na kutuhumu watu kuwa ni haters pale wanapokosoa jambo.
Haitarajiwi dosari kama hii kuonekana CNN ama BBC lakini ikitokea, fahamu tu kuwa kuna watu wanaweza kuwa matatani kwa kuzembea kumkagua mtangazaji. Eti vitu vya wazungu vinatakiwa kuwa vizuri na vyetu "siyo mbaya sana." Sijui kwa nini!!
Mchana mwema.
NB. Mojawapo ya sifa za mtangazaji mzuri ni kuwa na ufahamu wa msingi (basic knowledge) wa mambo mbalimbali na hasa yale anayoyajadili.
Mimi binafsi nitajadili hoja. Sitojadili jina lako maana jina ni jina tu wapo wanaoitwa malaika au majina ya manabii na mitume lakini hakuna uhusiano wa majina yao na matendo. Kulielewa jina langu kunahitaj uwe na uelewa wa juu. Ni jina la kifalsafa si akili za kawaida zinaweza elewa hili so siwez kukulaumu.
Mimi nalaumu sana baadh ya wazaz na mfumo wa elimu tulio nao. Unatengeneza watu ambao ni dhaifu kufikiri na wana ukosefu wa madini fikra kichwan. Kuna mtangazaj aliwah kukataliwa TV flan kusoma TAARIFA YA HABARI kwa kuwa tu ana makovu usoni. Huko saudi arabia kuna mtangazaji alifukuzwa kazi kwa kuwa hakuwa na mvuto. Mtangazaj anapovaa nguo kola imekaa vibaya kwa TV Makini ni tatizo kubwa tu. Maana inaonesha umakini kwa yeye na mpiga picha wake si mzuri. Kuna mambo ambayo tumejikuta tunayapuuzia kwa kutokujua au ujinga. Na ndo maana unaweza ona katka TV zetu mtangazaji kavaa koti oversize au tai na shati alivyovaa mwenzie jana naye kavaa hivyo hivyo na shat linaonekana kubwa au kwake dogo.
Ni tanzania unamwona mtangazaji kavaa shati linalopaswa kuchomekewa yeye hajachomekea unawaza pengine hata chini kavaa sandals au slippers.
Mwonekano ni jambo la muhimu sana. TV za kimataifa hilo ni kosa kubwa sana maybe kwa sabab yetu ni local ndo maana tunasema si jambo la maana sana. Kuna mtangazaji BBC aliwah pewa onyo kwa kukosea kutamka neno mara mbili wakat akisoma taarifa ya habari.
Kwa anayesema mtangazaji hana haja ya kujua mada anayojadili huyu anaonekana kiukwel uelewa wake ni wachini sana. Huyu dada sina tatizo naye taarifa ya habari anasoma vzuri. Kwenye majadiliano mada zilikuwa mbili za siasa na michezo. Hajui mambo hayo naye hatak kuonesha hajui so analazimisha aseme kitu na hapo anakosea.sasa kwa nini basi asipewe kozi kwanza kama ni lazima awepo yeye?kwa nini asijisomee?kwa nini wasifanye mazoez kwanza naye ajue watazungumzia nini? Haya mambo yatasababisha kila siku Tv zetu zibak local. Na ndo maana si ajabu kusikia waandishi wa habar wakat wa taarifa ya habari wanapiga story pasipo kujua wapo hewani. Au kusikia wanacheka wakat wa matangazo kwisha kabla tena ya kusoma taarifa ya hbr.