Chizi Maarifa, kwanza naanza kutoa lawama kwa jina la utambulisho ulilotumia (ID). Linachangia sisi tukushambulie.
Kati ya chizi na maarifa nafikiri chizi ndilo neno baya hivyo "kibinadamu" tutalichagua hilo baya badala ya zuri. Hivyo wewe ni Chizi.
Sasa kuhusu mada uliyoweka, sitazungumzia juu ya ufahamu wa mtangazaji au watangazaji bali kuhusu
"kijikosa" kidogo katika uvaaji ambacho
kwa sababu ya "uchizi" wako umekosa "maarifa" na kudhani kuwa hilo ni kosa kuuuubwa "kivile."
Dosari hiyo katika kola inaweza kusaidia kuonesha/kuonyesha udhaifu wa watu waliomzunguka huyo dada. Dosari hii, japo watu
wanaichukulia poa lakini inajenga picha kuwa
crew ya kipindi/programu husika (na hata AZAM TV yote) haiko makini.
Kabla ya kwenda hewani kuna mambo kadhaa ya kujiridhisha ikiwa ni pamoja na mavazi, mwonekano, afya na utulivu wa akili wa mtangazaji. Kosa ama dosari ndogo inachangia kujega taswira pana (brand/image) ya kampuni, taasisi au bidhaa.
Ndiyo maana baada ya Mhe. waziri C. K. kuondolewa kwa kuzungumza akiwa "amelewa" lawama hazikuishia kwake tu bali hata kwa wasaidizi wake (hata dereva analaumiwa). Kaondolewa ili kulinda taswira (brand/image) ya uwajibikaji wa serikali mbali na kosa lenyewe la kulewa wakati wa muda wa kazi.
Wabongo (Siyo wote) tumezoea sana mchezo wa
bora liende na kutuhumu watu kuwa ni
haters pale wanapokosoa jambo.
Haitarajiwi dosari kama hii kuonekana CNN ama BBC lakini ikitokea, fahamu tu kuwa kuna watu wanaweza kuwa matatani kwa kuzembea kumkagua mtangazaji. Eti vitu vya
wazungu vinatakiwa kuwa vizuri na vyetu
"siyo mbaya sana." Sijui kwa nini!!
Mchana mwema.
NB. Mojawapo ya sifa za mtangazaji mzuri ni kuwa na ufahamu wa msingi (basic knowledge) wa mambo mbalimbali na hasa yale anayoyajadili.