PICHA: Mzee Jakaya hilo shati nimelielewa sana

Salaam, Shalom!!

Kwenye mambo ya mpira mtaani, ni nadra sana kukuta mshabiki wa Yanga amevaa nguo zenye RANGI nyekundu.

Sasa Leo inatembea picha Moja ikimuonyesha Mzee wetu mstaafu aliyebaki akiwa amevaa shati lenye RANGI mchanganyiko nyeupee, bluu na nyekundu, na chini kavaa suruali ya bluu.

Sasa RANGI hizi zinafanana 100% na RANGI za bendera ya CDM!!

Hii inaleta picha na ujumbe Gani kuelekea chaguzi za 2024&2025?

Karibuni🙏
 
mpaka uchaguzi 2025 yeye atakuwepo?
 
Coda zimewakaa ka Wajinga flani hivi na Sura zao za Taharuki🤣
 
Namuona Riz1 hapo meza ya nyumaa anamtazama dingi wakee. Royal Family km Royal Family. Watu na life lao Duniani.
Woiiiiih
 
Kizimkazi na suti hiyo na peni hizo zimeharibu picha , ukijijini nao tabu

Wote,mliopo karibu na vice presidential office ,mwambieni mpango abaki na sura yake ,mambo ya tabasamu aachie wenyewe

Mstaafu ,kavaa bahama yangu ya Christmas 1976, lakini imewafunika wooote ,aibu
 
Suti ya Mzee imemwaga kidogo ila mnaoshona nguo za viongozi Mungu anawaona.

Eti bahama, Mzee Jakaya ni nembo ya furaha na amani ya Taifa letu
Ila Mpango wa Mungu suti imemkataa! Na bahama la JK nalo halijakaa sawa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…