Picha na Maelezo: Yaliyojiri ktk Viwanja vya Jangwani Mkutano wa UKAWA 26/10/2014

Picha na Maelezo: Yaliyojiri ktk Viwanja vya Jangwani Mkutano wa UKAWA 26/10/2014

Status
Not open for further replies.
Nimeuliza hapa konda kasema ni shilingi 100000 kuwapeleka tu huko jangwani wakitaka na kurudi tsh 250000

Nilikuwa nafikiri wanasombwa bure baadaye kuachwa huko mkutanoni kama lichama fulani lifanyavyo kumbe wanajitolea wenyewe kuhudhuria kwa hela zao kweli magamba lazima watage
 
Kila kitu kinamwanzo na mwisho CCM mwisho wao ndio huu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hakika leo ni siku ya kihistoria siku ambayo itakumbukwa na vizazi vijavyo ni siku ya kusaini kifo cha mkoloni mweusi(CCM), Kwa watakao fatilia kupitia mtandao huu nitaanza kuwarushia kinachoendelea kutoka uwanja wa Jangwani ni siku ya kusaini MoU kati ya vyama vinne vya kisiasa yaani CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI NA NLD.. Radio 1, ITV, Sibuka zitakuwa hewani kuanzia saa kumi mpaka kumi na mbili jioni
watu kwasasa wanazidi kufulika.

Updates;
Msafara ndo unaondoka makao makuu ya CUF, unaongozwa na king'ora as we have Makamu wa kwanza wa Rais...
tayari usafara uko uwanjani wa jangwani..
attachment.php


MWANZO WA MVUA NI MAWINGU. KWA UMATI HUU WA WATU INAONYESHA JINSI WATANZANIA WALIVYOTAMANI SANA VYAMA HIVI VIUNGANE,NA MOJA YA SILAHA WALIYOTUMIA CCM NI KUHAKIKISHA KWAMBA VYAMA HIVI VINAPAMBANA VYENYEWE.SASA CCM WATAJUTIA KOSA LA KARNE WALILOFANYA. WALIDHANI WAMEPATA KUMBE WAMEPATIKANA.ALL THINGS WORK TOGETHER FOR GOOD. CCM IS IN DANGER ZONE NOW
 
ili waendelee kuwepo ( japo kwa muda tu ) kwenye ulingo wa siasa inawapasa haraka sana wahamie ccm , hakuna namna yoyote kwa watu hawa hata kuandikwa kwenye gazeti la UHURU kwa hivi sasa , wamefunikwa kabisa na tukio hili la KIHISTORIA LA UKAWA , sasa nimekubali rasmi kwamba USALITI NI LAANA .
 
ikumbukwe kwamba lengo la wasaliti ilikuwa kuua kabisa upinzani nchi hii , hata hivyo kwa msaada wa Mungu imeshindikana !
 
Taratibu CCM inaelekea ilikoelekea KANU ya Kenya!!
Watafurukuta lakini hawataweza.... haya ni matakwa ya MUNGU kwa watu wake!!!
 
Makubaliano yaliyotiliwa saini na viongozi wa UKAWA ni haya Yafuatayo;

1.Kuhuisha sera za vyama vyetu; ili vyama vyote viwe vinazungumza mambo yanayofanana.

2.Kusimamisha mgombea mmoja kila jimbo la uchaguzi,(Serikali za mitaa...hadi rais wa JMT).

3.Utaratibu wa namna gani vyama vyote vitashirikiana katika chaguzi zote, Utaratibu wake utatolewa hivi karibuni.

4. Kushiriki katika mchakato wa kuwafahamisha Watanzania katika kukataa Katiba inayopendekezwa, haijazingatia maoni ya Wananchi,bali kikundi cha wachache,CCM na wafuasi wake.

5.Kujenga ushirikiano katika mambo yote muhimu kwa Taifa hili.

6.Kuhakikisha Muungano wetu unalindwa kwa gharama zozote zile.

7.Mambo yote yatafanyika bila ubaguzi wowote.
~MWISHO~
 
Pumzika kwa amani sasa ndugu UKAWA, CCM hawana chao kabisaaaaa, umoja ni nguvu..........
 
Iyena iyenaaa iyena iyenaaa iyena iyenaaa CCM nambari one....sasa kazi imekuwa rahisi sana tunapiga jiwe Moja kwa ndege wote wanne yaani CDM, CUF, NCCR na NLD.

Subirini majibu serikali za mitaa lazima mkae!
 
Pumzika kwa amani sasa ndugu UKAWA, CCM hawana chao kabisaaaaa, umoja ni nguvu..........

Ulitakiwa kusema sasa CCM kinaendelea na kitaendelea kuongoza kwa Amani kwani kazi imekuwa rahisi kupambana na UKAWA badala ya mmoja mmoja!

Majibu serikali za mitaa ndio mtajua mbivu na mbichi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom