Picha: Nimepata msongo wa mawazo baada kuona katuni ya leo ya Masoud Kipanya akizungumzia sakata la Wachina

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Tunaposema Wachina ni existentia threat kwenye nchi hii, basi tunamaanisha mambo kama haya.

Mimi nilivyoelewa hii katuni ya Masoud Kipanya ni kwamba:

Pamoja na kwamba mchele unaouzwa na Mtanzania ni gharama lakini Mtanzania akinunua mchele, muuzaji ataenda kununua vitumbua baadae so kutakuwa na mzunguko wa fedha ndani ya nchi. Yaani wataunganishana.

Ila mchina akiuza mchele, yeye hatumii fedha zake kwa Watanzania yaani HAWAUNGISHI wabongo.

Mkishanunua vitu kwake yeye ataenda ataenda kutumia hizo fedha kwenye hotel, restaurants na kwenye mahotel ya kichina.

Na ndo maana Wachina wana CARWASH, HOTEL, RESTAURANTS, YARDS na HOSPITALI.

Mnawapa Wachina hela lakini hawazirudishi kwenu, wanazitumia kwao.

Nyie wenzangu mmeelewaje?

kipanya.jpeg
 
Mimi nimeelewa mchele ambao wewe unauza Tsh 3000, mchina anauza tsh 1000.
Sasa mteja aliyenunua kwa mchina atabaki na elfu mbili ya kwenda kununua vitumbua, viungo vya kupikia mchele pamoja na dagaa.

Hivyo kama umepata msongo wa mawazo nadhani umepona

Bora basi ununue huo mchele wa mchina uuze 1200😊
 
Mimi nimeelewa mchele ambao wewe unauza Tsh 3000, mchina anauza tsh 1000.
Sasa mteja aliyenunua kwa mchina atabaki na elfu mbili ya kwenda kununua vitumbua, viungo vya kupikia mchele pamoja na dagaa.

Hivyo kama umepata msongo wa mawazo nadhani umepona

Nyie wauza mchele mara nyingi mnakula nyama hivyo acha mteja abaki na salio la kwenda kumuungisha mama vitumbua

Unadhani kwanini Kipanya kaweka hiyo frame namba 3?

Ya Mchina kushika fedha, akienda kwenye jengo la kichina?
 
Wakuu,

Tunaposema Wachina ni existentia threat kwenye nchi hii, basi tunamaanisha mambo kama haya.

Mimi nilivyoelewa hii katuni ya Masoud Kipanya ni kwamba:

Pamoja na kwamba mchele unaouzwa na Mtanzania ni gharama lakini Mtanzania akinunua mchele, muuzaji ataenda kununua vitumbua baadae so kutakuwa na mzunguko wa fedha ndani ya nchi. Yaani wataunganishana.

Ila mchina akiuza mchele, yeye hatumii fedha zake kwa Watanzania yaani HAWAUNGISHI wabongo.

Mkishanunua vitu kwake yeye ataenda ataenda kutumia hizo fedha kwenye hotel, restaurants na kwenye mahotel ya kichina.

Na ndo maana Wachina wana CARWASH, HOTEL, RESTAURANTS, YARDS na HOSPITALI.

Mnawapa Wachina hela lakini hawazirudishi kwenu, wanazitumia kwao.

Nyie wenzangu mmeelewaje?

View attachment 3282509
Nami nimeelewa kama ulivyoelewa wewe.
 
Mimi nimeelewa mchele ambao wewe unauza Tsh 3000, mchina anauza tsh 1000.
Sasa mteja aliyenunua kwa mchina atabaki na elfu mbili ya kwenda kununua vitumbua, viungo vya kupikia mchele pamoja na dagaa.

Hivyo kama umepata msongo wa mawazo nadhani umepona

Nyie wauza mchele mara nyingi mnakula nyama hivyo acha mteja abaki na salio la kwenda kumuungisha mama vitumbua
Tazama upya, huyo wa kununua vitumbua sio mteja tu, maana ya ziada kuwa akiuza faida inarudi kwa wananchi nchini, utaona jamaa anatembea anapeleka hela ktk vitumbua.

Mchina faida anapeleka kwao,unaona anatembea kwenda ktk jengo lenye maandish ya kichina badala kurudi kwa wazawa.
 
Hao wachina ni nafuu kwa wananchi ila threat kwa wafanyabiashara.

Hizi mbanga angeanza nazo Nyerere kwa kutoruhusu wahindi & waarabu huko nyuma hata hawa wachina naona wamechelewa sana, walikua na muda wa kufanya haya kitambo kabla mitandao haijawa mingi ili waweke mizizi kama wenzao wahindi.
 
Acha madalali wafundishwe jinsi ya kufanya biashara... Mbongo anataka kwenye mauzo ya siku 1 apate faida ya kwenda kufanya starehe na kuwatukana maskini 🤣🤣
 
Mimi nimeelewa mchele ambao wewe unauza Tsh 3000, mchina anauza tsh 1000.
Sasa mteja aliyenunua kwa mchina atabaki na elfu mbili ya kwenda kununua vitumbua, viungo vya kupikia mchele pamoja na dagaa.

Hivyo kama umepata msongo wa mawazo nadhani umepona

Nyie wauza mchele mara nyingi mnakula nyama hivyo acha mteja abaki na salio la kwenda kumuungisha mama vitumbua
Huyo Mtanzania mwenzako anayeuza mchele elfu tatu ndio huyo huyo anayenunua vitumbua. Nenda kamuungishe mchina ambaye vitumbua hanunui na hela yako anapeleka kwenye bank ya kichina/china, na aliyekuwa anakuuzia mchele elfu tatu kwakua humuungishi, anashindwa kununua vitumbua hivyo vitumbua haviuziki! mwisho mzunguko mdogo wa fedha, uchumi mkua mgumu, umasikini kuongezeka.
 
Watanzania wanapenda faida mara mbili wapuuzi tu, bora wageni wabaki

Usidhani hizo prices za Wachina ni permanet mkuu.

Kwenye Uchumi kuna kitu kinaitwa PREDATORY Pricing. Unashusha bei chini sana sometimes hata kwa hasara ili kukata ushindani na kupata wateja.

Ukishacontrol supply na kupata wateja, unaongeza bei kwa namna unayotaka wewe.

Thats exactly what Chinese wanafanya sasa hivi

Once wachina wakisha-control Kariakoo in 5 years time, tutaona kitachotokea
 
Back
Top Bottom