nimesoma maoni ya wadau nilichogundua ni kwamba wanaolalamika wengi ni hao madalali wanaovuna faida mara mbili kabla ya ujio wa wachina so far watz wanapenda wabaki wao ili kuwakandamiza maskini wa hali ya chini ,imagine nguo inauzwa 15k lets say china ila kibongo bongo mtu anakuuzia 30k 😡😡😡 siamini kwamba hiyo faida ya 15k inaishia kwenye VAT yaan anaona jau kupata faida ya 5k so sad ......vua inyeshe tuone panapovuja
Ajabu sana kwamba mtu anashindwa kuona athari katika mapana yake. Ni kweli wachina wanauza vitu kwa bein nafuu, ni kweli wafanya biashara wanapata faida nzuri kununua kutoka china na kuuza hapa kwetu ila hayo yote sio conclusive.
Nakubaliana na wazo la kuruhusu wawekezaji wa nje kuja kuchechemua uchumi wetu ila ni lazima tulifanye hili kwa udhibiti mkali na ikiwezekana kwa awamu ...
1) Udhibiti lazima uwepo kuona mchina haendi kumiliki uti wa mgongo wa uchumi wa watu wetu i.e. kilimo na mazao ya kilimo, leo hii kumekuwa na wimbi kubwa mikoani na wanaonekana wachina wakianza kumili ardhi indirectly kupitia wazawa wenye njaa, pia wapo mstari wa mbele katika kununua mazao ya kilimo directly kutoka kwa wakulima, hapa wanaweza kuitia nchi kwenye njaa ama wakishamiliki manunuzi. Hii inaweza kutengeneza
Monopsony wakati wa manunuzi ya bidhaa ghafi na
Monopoly wakati wa mauzo ya their final product.
2) Lazima tudhibiti ustawi wa viwanda na biashara za wazawa, wachina wasije kushindana na wajasiriliamali wadogo bali waje kuongeza thamani ya kwa wajasiriamali wadogo
3) Lazima tudhibiti ajira za wazawa, Engeneer wa kichina mwenye experience ya miaka 3 anaweza kuwa na utaalam kumzidi Engeneer wetu mwenye experience ya miaka 6 ama zaidi, Kuwapa wao tenda kunapaswa kwenda sambamba na masharti ya kuwa-involve qualified locals katika projects na kuwe na kipimo cha kuonyesha baada ya project atakuwa ame-develop kwa kiwango gani. Pia kusiwe na mchina atakayefanya kazi ya mzawa ikiwa hiyo kazi inaweza kufanywa na mzawa
4) Kuwe na chombo kinacho harmonise maslahi ya waajiriwa wazawa katika kampuni za kichina ili kuhakikisha wazawa hawanyonywi na kukandamizwa, leo hii ni kawaida kuona graduate amaejiriwa na wachina lakini analipwa kima cha chini cha mshahara ambacho hata serikali hailipi hivo katika kada hiyo i.e. mhasibu kulipwa 350,000 kwa mchina ni kawaida.
5) Kuwe na udhibiti wa ukaguzi, makadirio na malipo ya kodi. Wachina ni mabingwa na ubabaifu, na wapo vizuri katika hili kwa mbali sana.
Tusipofanya haya tunafanya matayarisho ya raia wetu kuwa watumwa wa kiuchumi kwa wachina, tena ndani ya ardhi yetu.