Wakuu,
Tunaposema Wachina ni existentia threat kwenye nchi hii, basi tunamaanisha mambo kama haya.
Mimi nilivyoelewa hii katuni ya Masoud Kipanya ni kwamba:
Pamoja na kwamba mchele unaouzwa na Mtanzania ni gharama lakini Mtanzania akinunua mchele, muuzaji ataenda kununua vitumbua baadae so kutakuwa na mzunguko wa fedha ndani ya nchi. Yaani wataunganishana.
Ila mchina akiuza mchele, yeye hatumii fedha zake kwa Watanzania yaani HAWAUNGISHI wabongo.
Mkishanunua vitu kwake yeye ataenda ataenda kutumia hizo fedha kwenye hotel, restaurants na kwenye mahotel ya kichina.
Na ndo maana Wachina wana CARWASH, HOTEL, RESTAURANTS, YARDS na HOSPITALI.
Mnawapa Wachina hela lakini hawazirudishi kwenu, wanazitumia kwao.
Nyie wenzangu mmeelewaje?
View attachment 3282509