Picha: Nimepata msongo wa mawazo baada kuona katuni ya leo ya Masoud Kipanya akizungumzia sakata la Wachina

Picha: Nimepata msongo wa mawazo baada kuona katuni ya leo ya Masoud Kipanya akizungumzia sakata la Wachina

Mimi nimeelewa mchele ambao wewe unauza Tsh 3000, mchina anauza tsh 1000.
Sasa mteja aliyenunua kwa mchina atabaki na elfu mbili ya kwenda kununua vitumbua, viungo vya kupikia mchele pamoja na dagaa.

Hivyo kama umepata msongo wa mawazo nadhani umepona

Nyie wauza mchele mara nyingi mnakula nyama hivyo acha mteja abaki na salio la kwenda kumuungisha mama vitumbua
Huyo Mtanzania mwenzako anayeuza mchele elfu tatu ndio huyo huyo anayenunua vitumbua. Nenda kamuungishe mchina ambaye vitumbua hanunui na hela yako anapeleka kwenye bank ya kichina/china, na aliyekuwa anakuuzia mchele elfu tatu kwakua humuungishi, anashindwa kununua vitumbua hivyo vitumbua haviuziki! mwisho mzunguko mdogo wa fedha, uchumi mkua mgumu, umasikini kuongezeka.
 
Tazama upya, huyo wa kununua vitumbua sio mteja tu, maana ya ziada kuwa akiuza faida inarudi kwa wananchi nchini, utaona jamaa anatembea anapeleka hela ktk vitumbua.

Mchina faida anapeleka kwao,unaona anatembea kwenda ktk jengo lenye maandish ya kichina badala kurudi kwa wazawa.
Bado hujajua nini maana ya mzunguko wa biashara... Kwani mbongo anaebeba box pale marekani, Uingereza, Japan au hata anaeuchuuza viatu pale Nairobi haruhusiwi kutuma kiasi fulani kwao?
Kuna hela nyingi zinaingia kutoka nje na kuna zinazotoka, na zote zinakatwa makato.... Watu kama nyie nawafananisha na wahadzabe
 
Tazama upya, huyo wa kununua vitumbua sio mteja tu, maana ya ziada kuwa akiuza faida inarudi kwa wananchi nchini, utaona jamaa anatembea anapeleka hela ktk vitumbua.

Mchina faida anapeleka kwao,unaona anatembea kwenda ktk jengo lenye maandish ya kichina badala kurudi kwa wazawa.

Sijui kwanini watu hawaoni hii.

Kuna mfanyabiashara mmoja wa Kariakoo alikuwa anaongelea hili suala Wasafi.

Wachina kila jioni wakifunga mahesabu wanabadili hela kuwa dola then wanatuma kwao,

Alikuwa anasema hata dola kukosekana hapa katikati wao pia walikuwa ni sababu
 
Bado hujajua nini maana ya mzunguko wa biashara... Kwani mbongo anaebeba box pale marekani haruhusiwi kutuma kiasi fulani kwao?
Kuna hela nyingi zinaingia kutoka nje na kuna zinazotoka, na zote zinakatwa makato.... Watu kama nyie nawafananisha na wahadzabe

Wabongo wanaobeba mabox Marekani wana benki ya kibongo, car wash, restaurants na hoteli za kwao tu kama wachina wanavyofanya?

Plus kwa diaspora, watakwambia kwamba ukituma hela nyingi sana kutoka Marekani kwenda nchi nyingi in the name of kutumia familia yako, FBI wana-detect na watakuja on your door kukuuliza kwanini unatuma hela nyingi nje ya nchi.

Mambo sio rahisi kwa wenzetu kama unavyodhani
 
Hakuna cha shallow thinking, watanzania hatupendi ushindani kwenye nyanja yoyote ile.

Hakuna cha ushindani mkuu.

Wachina kwa sasa wanatengeneza monopolies kwa kufanya predatory pricing ili wakamate soko na supermarkets zote.

Ni mbinu inayotumika sana kwenye biashara. Wakshakamata soko watapanga wao bei. Kwa sisi tuliosoma uchumi hiyo ni business practise tu.

Siku wachina wakishakamata soko mtakuwa mnawapigia magoti wawapunguzie bei za bidhaa.

Ni sawa tu kwenye bei za vifurushi.

Ni suala la muda
 
Wanachofanya wachina ndicho ambacho wahindi wamekifanya kwa miaka mingi maana wao wana shule zao binafsi, restaurants na maeneo ya kuishi. Na hata vijana wa kiume wanatafutiwa mabinti kutoka Pakistan na India waje kuoa

Nachokiona tofauti yao na wachina ni kuwa wahindi na waarabu wameingia bongo karne nyingi hivyo namna yao ya kuishi tumeichukulia kama kawaida.. Ila mchina anaonekana mgeni na anapambania kila chocho ambayo muhindi haoni kama ni hadhi yake
 
Wakuu,

Tunaposema Wachina ni existentia threat kwenye nchi hii, basi tunamaanisha mambo kama haya.

Mimi nilivyoelewa hii katuni ya Masoud Kipanya ni kwamba:

Pamoja na kwamba mchele unaouzwa na Mtanzania ni gharama lakini Mtanzania akinunua mchele, muuzaji ataenda kununua vitumbua baadae so kutakuwa na mzunguko wa fedha ndani ya nchi. Yaani wataunganishana.

Ila mchina akiuza mchele, yeye hatumii fedha zake kwa Watanzania yaani HAWAUNGISHI wabongo.

Mkishanunua vitu kwake yeye ataenda ataenda kutumia hizo fedha kwenye hotel, restaurants na kwenye mahotel ya kichina.

Na ndo maana Wachina wana CARWASH, HOTEL, RESTAURANTS, YARDS na HOSPITALI.

Mnawapa Wachina hela lakini hawazirudishi kwenu, wanazitumia kwao.

Nyie wenzangu mmeelewaje?

View attachment 3282509
Tujiulize kwanza mchina anatoa wapi Michele hadi auze 1000 na watanzania wanatoa wapi Michele hadi wauze 3000?
 
Wabongo wanaobeba mabox Marekani wana benki ya kibongo, car wash, restaurants na hoteli za kwao tu kama wachina wanavyofanya?

Plus kwa diaspora, watakwambia kwamba ukituma hela nyingi sana kutoka Marekani kwenda nchi nyingi in the name of kutumia familia yako, FBI wana-detect na watakuja on your door kukuuliza kwanini unatuma hela nyingi nje ya nchi.

Mambo sio rahisi kwa wenzetu kama unavyodhani
Kwahiyo tatizo sio wachina ni wabongo wenyewe sio? Japo sina hakika na ulichosema, huoni serikali ndio ya kulaumiwa?
 
Wanachofanya wachina ndicho ambacho wahindi wamekifanya kwa miaka mingi maana wao wana shule zao binafsi, restaurants na maanee ya kuishi. Na hata vijana wa kiume wanatafutiwa mabinti kutoka Pakistan na India waje kuoa

Nachokiona tofauti yao na wachina ni kuwa wahindi na waarabu wameingia bongo karne nyingi hivyo namna yao ya kuishi tumeichukulia kama kawaida.. Ila mchina anaonekana mgeni na anapambania kila chocho ambani muhindi haoni kama ni hadhi yake

Na ndo maana hata matajiri wakubwa nchi hii wana asili ya kuwa wahindi na waarabu.
 
Back
Top Bottom