Picha: Nimepata msongo wa mawazo baada kuona katuni ya leo ya Masoud Kipanya akizungumzia sakata la Wachina

Kwanini tusiige mbinu zao?

Wachina wanaweza kufanya predatory pricing kwa sababu wanapewa soft loans na serikali yao.

Mchina anaomba mkopo wa Milioni 100 riba ni laki tatu mpaka milioni 1, mfanyabiashara wa kibongo anaenda kukopa CRDB Milioni 100 anarudisha Milioni 15 hadi 20.

Hawa watu unawezaje kuwapambanisha kwenye ulingo mmoja mkuu?

The sad part is, hata serikali ya kibongo ikianza kugawa hizo soft loans kwa Wabongo ili wafanye kama wachina wanavyofanya still Serikali ya Tanzania HAIWEZI kushindana na serikali ya KICHINA.

Mwaka 2020 pekee, serikali ya China ilitoa 1.8 TRILLION USD kama mkopo kwa SMEs, serikali ya Bongo haina uwezo huo.
 
Acheni upumbavu wa kuuza kwa bei ya juu kitu chenye bei dwelele mnapenda faida za juu nakwambia mimi nikikuta mchina anauza kwa bei dwelele na nunua hapo kama mmeshindwa kutuhurumia watanzania wenzenu mchina katuhurumia basi acheni nongwa kusave buku2 si haba asee

Umekurupukia mjadala mkuu.

Soma tena
 
Huyo Mtanzania mwenzako anayeuza mchele elfu tatu ndio huyo huyo anayenunua vitumbua. Nenda kamuungishe mchina ambaye vitumbua hanunui na hela yako anapeleka kwenye bank ya kichina/china, na aliyekuwa anakuuzia mchele elfu tatu kwakua humuungishi, anashindwa kununua vitumbua hivyo vitumbua haviuziki! mwisho mzunguko mdogo wa fedha, uchumi mkua mgumu, umasikini kuongezeka.
Wewe jamaa ndio umemaliza, inabidi ii comment yako iwepo hapo juu.
 
Sijui kwanini watu hawaoni hii.

Kuna mfanyabiashara mmoja wa Kariakoo alikuwa anaongelea hili suala Wasafi.

Wachina kila jioni wakifunga mahesabu wanabadili hela kuwa dola then wanatuma kwao,

Alikuwa anasema hata dola kukosekana hapa katikati wao pia walikuwa ni sababu
Ulitegemea huyo mfanyabiashara mnafiki aseme nini? Amsifie Mchina wakati ni tishio kwake?

Shida ya wafanyabiashara wa kizawa ni tamaa. Nimekwenda kununua deodorant niipendayo naambiwa bei ni 50K. Nakwenda kwa Mchina deodorant ile ile ni 15K. Yaani wana tamaa ukizubaa hata hawasiti kukuuzia kwa gharama mara tatu hata nne. Ujinga tu. Na nimenunua kwa Mchina potelea mbali hata kama hiyo 15K yangu ataituma kwao Beijing lakini mimi nimebaki na 35K ya kunywea bia.

Nguvu za soko lazima ziheshimiwe na ifike mahali tupunguze Uswahili na tamaa katika biashara. Nadhani Wachina wanatufundisha somo hili kwa vitendo. Eti nikapigwe 50K kwa kitu kile kile wakati naweza kukipata kwa Mchina kwa 15K kisa uzalendo na kuinua uchumi. Thubutuuu!

20250325_110537.png

Na shida yetu kubwa wala siyo hawa Wachina maana hawa serikali inaweza kuwathibiti mara moja ikiamua. Shida yetu kubwa ni ufisadi na matumizi mabovu ya fedha za umma na raslimali za taifa; na bila kushughulika nao sawasawa tutaishia kuwa tunaokoteza visababu huku na huko na hakuna kitu kitakachobadilika.
 
Jibu swali unataka raia wachache wawanyonye raia wengi na wao kufaidika Kwa kigezo Cha uraia wao Ili wananchi waumie sio wafanyabiashara waendelee kupata faida kubwakubwa Kwa kupandisha bidhaa ovyo

Usipaniki.

Nimejibu huko juu.

Nimekwambia hizo prices HAZITODUMU. Ni mbinu ya kibiashara tu hiyo.

Ni kama Halotel tu walivyokuja kipindi kile wakiwa wapya na "vifurushi vya bei nafuu" walivyopata wateja hivyo vifurushi vimeishia wapi?

Na inaonekana hukai hata Dar. Kuna maduka mengi ya wabongo wanauza bidhaa za kichina in a very cheap price

Shida mnakaa maporini huko. Vitu mnasoma mitandaoni
 
Ulitegemea huyo mfanyabiashara mnafiki aseme nini? Amsifie Mchina wakati ni tishio kwake?

Shida ya wafanyabiashara wa kizawa ni tamaa. Nimekwenda kununua deodorant niipendayo naambiwa bei ni 50K. Nakwenda kwa Mchina deodorant ile ile ni 15K. Yaani wana tamaa ukizubaa hata hawasiti kukuuzia kwa gharama mara tatu hata nne. Ujinga tu. Na nimenunua kwa Mchina potelea mbali hata kama hiyo 15K yangu ataituma kwao Beijing lakini mimi nimebaki na 35K ya kunywea bia.

Nguvu za soko lazima ziheshimiwe na ifike mahali tupunguze Uswahili na tamaa katika biashara. Nadhani Wachina wanatufundisha somo hili kwa vitendo. Eti nikapigwe 50K kwa kitu kile kile wakati naweza kukipata kwa Mchina kwa 15K kisa sijui uzalendo na kuinua uchumi. Thubutuuu!

View attachment 3282633

Na shida yetu kubwa wala siyo hawa Wachina maana hawa serikali inaweza kuwathibiti mara moja ikiamua. Shida yetu kubwa ni ufisadi na matumizi mabovu ya fedha za umma na raslimali za taifa; na bila kushughulika nao sawasawa tutaishia kuwa tunaokoteza visababu huku na huko na hakuna kitu kitakachobadilika.

Umeleta hadi picha?

Ni umasikini tu unakusumbua na kukosa exposure.

Hiyo bidhaa yako nenda kwenye "Duka La Fursa" pale Sinza unaipata kwa price ya chini kama hiyo ya kichina,
 
Umekurupukia mjadala mkuu.

Soma tena
Nimeelewa sana. Kama wa Tz wangekuwa wanauza kwa bei sawa na mchina hakuna angeenda wa machine kununua pale....ukisema serikali iwatoe wachina hakika maisha yetu yatakuwa magumu mno Nina uhakika watu wanaenda kwa mchina kqa sababu ya bei hayo mambo uliyosema hakuna anaye yawazia kwanza huo mzunguko eti muuza Mchele ataenda kununua vitumbua kwa mama lishe... huoni kuna buku2 ataenda pia yule aliyenunua Michele na bado atanunua dagaa ?
 
Kuna swali limeulizwa hapo juu naona wanazi wamelikimbia
Mchina anatoa wapi mchele na mbongo anatoa wapi mchele hadi watofautiane bei namna hiyo?

Limefafanuliwa.

Soma tena comments
 
Wabongo wanaobeba mabox Marekani wana benki ya kibongo, car wash, restaurants na hoteli za kwao tu kama wachina wanavyofanya?

Plus kwa diaspora, watakwambia kwamba ukituma hela nyingi sana kutoka Marekani kwenda nchi nyingi in the name of kutumia familia yako, FBI wana-detect na watakuja on your door kukuuliza kwanini unatuma hela nyingi nje ya nchi.

Mambo sio rahisi kwa wenzetu kama unavyodhani
Wakulaumu sio wachina bali ni CCM ambayo iko madarakani. Wameshindwa kuweka mifumo ambayo itawabana wawekezaji ili walipe kodi stahiki, waajiri wazawa na kuzuia mianya yote ya kutorosha fedha nje ya nchi. Tutapiga kelele mitandaoni lakini hakuna kitakachobadilika kama hakuna mfupo wa usimamizi na uwabikaji kutoka serikalini.
 
Wachina wanaweza kufanya predatory pricing kwa sababu wanapewa soft loans na serikali yao.

Mchina anaomba mkopo wa Milioni 100 riba ni laki tatu mpaka milioni 1, mfanyabiashara wa kibongo anaenda kukopa CRDB Milioni 100 anarudisha Milioni 15 hadi 20.

Hawa watu unawezaje kuwapambanisha kwenye ulingo mmoja mkuu?

The sad part is, hata serikali ya kibongo ikianza kugawa hizo soft loans kwa Wabongo ili wafanye kama wachina wanavyofanya still Serikali ya Tanzania HAIWEZI kushindana na serikali ya KICHINA.

Mwaka 2020 pekee, serikali ya China ilitoa 1.8 TRILLION USD kama mkopo kwa SMEs, serikali ya Bongo haina uwezo huo.
Kama hatuwezi kushindana kwanini tushindane?
Mchina anauza 1000, wewe unauza 3000. Sasa si bora uwe unachukua mzigo kwa mchina ukauze mbali na hapo kwa Tsh 1200?😁
 
Ni umasikini tu unakusumbua na kukosa exposure.
Haya mkuu. Ni uzi wako. Na naona unahangaika nao kweli kweli kwa kumkoromea kila mtu mwenye mawazo tofauti na yako. Na hili huwa linanishangaza sana. Kwa nini unaanzisha uzi halafu unaanza kumshambulia kila mwenye mawazo tofauti na yako? What's the point?

By the way; mimi siyo masikini na exposure nadhani ninayo ya kutosha tu. Hapa duniani sijafika Antarctica tu na Australia. Na hapa Bongo sijafika Kigoma tu 😂😂😂

#Nguvu za Soko Ziheshimiwe 📌📌📌
 
Usipaniki.

Nimejibu huko juu.

Nimekwambia hizo prices HAZITODUMU. Ni mbinu ya kibiashara tu hiyo.

Ni kama Halotel tu walivyokuja kipindi kile wakiwa wapya na "vifurushi vya bei nafuu" walivyopata wateja hivyo vifurushi vimeishia wapi?

Na inaonekana hukai hata Dar. Kuna maduka mengi ya wabongo wanauza bidhaa za kichina in a very cheap price

Shida mnakaa maporini huko. Vitu mnasoma mitandaoni
Hazitodumu kwani maisha si Kila siku yanapanda unataka Leo mchina auze suruali 5000 baada ya miaka 50 auze Bei hiyo hiyo tunachotaka sisi ni unafuu wa Bei Kwa wakati tuliopo sio kupandishia wananchi Bei bidhaa ambayo haistaili hiyo Bei Kwa mda huo tumia akili ukiwa unaandika vitu
 
Nimeelewa sana. Kama wa Tz wangekuwa wanauza kwa bei sawa na mchina hakuna angeenda wa machine kununua pale....ukisema serikali iwatoe wachina hakika maisha yetu yatakuwa magumu mno Nina uhakika watu wanaenda kwa mchina kqa sababu ya bei hayo mambo uliyosema hakuna anaye yawazia kwanza huo mzunguko eti muuza Mchele ataenda kununua vitumbua kwa mama lishe... huoni kuna buku2 ataenda pia yule aliyenunua Michele na bado atanunua dagaa ?

Mkuu,

Nimesema huko juu kuwa ni business strategy, hizo prices ni za muda mfupi. Wakisha-control prices mtawapigia magoti wapunguze bei

Unajidanganya sana kama unadhani Wachina wako nchini "kuboresha" maisha yako kwa kukuuzia vitu cheaply.

Ngoja nikuulize mkuu.

Wafanyabiashara wengi locally hawawezi ku-afford frame MIKOCHENI kwa sababu ni eneo very expensive

Lakini Wachina wamechukua jengo Mikocheni pembeni ya Clouds inaitwa CITI STORE alafu wanauza KILA KITU cha humo 3,000

Hivi kwa akili y kawaida who rents a space in Mikocheni alafu auze vitu cheaply kiasi hicho? Kwa kuwa wanawapenda sana sio?
 
Haya mkuu. Ni uzi wako. Na naona unahangaika nao kweli kweli kwa kumkoromea kila mtu mwenye mawazo tofauti na yako. Na hili huwa linanishangaza sana. Kwa nini unaanzisha uzi halafu unaanza kumshambulia kila mwenye mawazo tofauti na yako? What's the point?

By the way; mimi siyo masikini na exposure nadhani ninayo ya kutosha tu. Hapa duniani sijafika Antarctica tu na Australia. Na hapa Bongo sijafika Kigoma tu 😂😂😂

#Nguvu za Soko Ziheshimiwe 📌📌📌

Mkuu,

Mimi nna tabia ya kupokea mtu kwa namna alivyokuja

Asante
 
Mkuu,

Nimesema huko juu kuwa ni business strategy, hizo prices ni za muda mfupi. Wakisha-control prices mtawapigia magoti wapunguze bei

Unajidanganya sana kama unadhani Wachina wako nchini "kuboresha" maisha yako kwa kukuuzia vitu cheaply.

Ngoja nikuulize mkuu.

Wafanyabiashara wengi locally hawawezi ku-afford frame MIKOCHENI kwa sababu ni eneo very expensive

Lakini Wachina wamechukua jengo Mikocheni pembeni ya Clouds inaitwa CITI STORE alafu wanauza KILA KITU cha humo 3,000

Hivi kwa akili y kawaida who rents a space in Mikocheni alafu auze vitu cheaply kiasi hicho? Kwa kuwa wanawapenda sana sio?
Yote tisa mkuu kumi uzeni bei nzuri kwa manufaa ya raia wenzenu. Kila kitu tunajua ila waacheni kwanza wampe akili zikiwaijia wataondoka tu
 
Huyo Mtanzania mwenzako anayeuza mchele elfu tatu ndio huyo huyo anayenunua vitumbua. Nenda kamuungishe mchina ambaye vitumbua hanunui na hela yako anapeleka kwenye bank ya kichina/china, na aliyekuwa anakuuzia mchele elfu tatu kwakua humuungishi, anashindwa kununua vitumbua hivyo vitumbua haviuziki! mwisho mzunguko mdogo wa fedha, uchumi mkua mgumu, umasikini kuongezeka.
Kwaiyo ninunue kwa mtanzania kisa anaenda kuungisha sehem nyingine?
Mitanzania ni mijizi mitupu! Sukari ya nje inabei ndogo kuliko ya ndani?
Acha wachina waje tu tena wajae
 
Wenzetu wana agenda ya kuwa super power na kuwa successfully countywide, sie tunawaza kubakia madarakani na kupambana na upinzani yaani kwa kifupi hajioni kama taifa baada ya miaka 50 mbele tuko wapi, kwa hiyo acha wajazane kanisa ili likija suala la watu kudai haki zao kusiwe na nani ataanza varangati yaani ni mtu anaamka na familia yake asubuhi anangaalia anakiamshaje… Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu
 
Back
Top Bottom