Picha: Nyumba mpya ya Diamond ya South Africa

Picha: Nyumba mpya ya Diamond ya South Africa

Bei ya nyumba Afrika Kusini ni ndogo kuliko Tanzania. Nyumba nzuri ambazo zinauzwa ziko nyingi sana kuliko Tanzania
Ooh...
Kumbe..!!?
Basi ngoja na mimi niendelee kuBet nikanunuage nyumba huko kwa MADIBA..!
 
7 out of 10 ya wasanii wanasemaga nyumba walizopanga ni zao (wamezinunua)!

Hat hivyo Zari akienda South utakuta anaishi kwa mume wake mwingine.
Haya ni maigizo mengine tena sijui kuna mijitu imeumbwa kusifia tu hapa duniani? Nakumbuka sana magazeti ya udaku yalivyokuwa yakipamba majumba hewa ya wasanii ambayo hayana utofauti na hili.
Amjengee mama yake kama ile yangu niliyokuonyesha? 😉

Ila nyie si mlikuwa mnasema Zari katoswa?

Kulikoni tena?

Au ndo yaleyale...uzushi tu?
 
Kwa hiyo diamond anamaanisha kuwa ivan hana nyumba na pale ile nyumba zari alikua kapanga tu kumbe hehehe katupa siri tulikua hatuijui,,,yaan ivana na mapesa yote yale hana nyumba kweli kua na nyumba ni kipaji[emoji23]mi nasubiri mapigo ya ivana nyumba atakayodondosha np (natabiri tu)
yaani nimeshangaa
 
Najiuliza kwa sauti ivi nyie wasichana warembo wa tz hamkuiona hii fursa kwa diamond mkamdharau mkacheka ule mdomo wee waganda wakaula denda wakaupetipet wakamzalie leo hii ndo wanapeta nae jamani mmeniangusha warembo wetu wa kibongo msirudie tena hebu kamatien fursa kwa kina raynavy sasa maana diamond kasha bebwa na idd amin afu we chibuu una bahati nyerere hayupo angekucharaza bakora uyo mganda alimsumbua sana[emoji23][emoji23]
 
nyumba iko sauzi mtaa gani na hati ni ya nani? kama kweli amenunUa bora angewajengea watoto yatima hapa bongo waishi au talent center btw muda wote zari alikuwa anaishi kwenye nyumba ya kupanga au kwa baba watoto wake ivan....kichwa kinauma
 
Nyumba ugenini tena ya gorofa aisee very expensive house in soth afrika nadhani iyo pesa ya hapo kwa bongo unaweza kujenga kama izo mbili kutokana na tofauti ya uchumi wetu na bondeni
Kinyume chake. Tz nyumba bei ghali zaidi ya SA na nchi nyingi tu duniani.
 
Nyumba kama hiyo kwa Dar itakuwa Masaki au Mikocheni kwavile ina Swimming Pool, au?! Ndio maana nikakuambia hujazingatia mambo ya msingi! Aidha na ndio maana nikakupa mfano wa Masaki na Westcliff kv ni maeneo yanayowiana kwa hadhi! Na ndio maana pia nikahoji unataka kuniambia nyumba yenye sifa zile zile (achana na hiyo ya Chibu); ya Masaki itakuwa ni expensive kuliko ya Westcliff?!
Nimeangalia bei ya nyumba westcliff, honestly same house ikiwa masaki itauzwa bei ghali zaidi.

http://www.property24.com/for-sale/westcliff/johannesburg/gauteng/4396/104119810
 
You have to attack my points not my person. It is always important to remember that in discussion/debate. You don't know me, what I know, and what I have got just as I don't know you.

Back to the point. Mimi sijasema hiyo nyumba ni cheap.

Lakini ninachokuambia ni kuwa Tanzania tuna tatizo kubwa sana la kutokupima ardhi hasa mijini. Sehemu kubwa ya mji wa Dar es Salaam imekuwa ni ghetto tu. Hakuna barabara, sewage system, ukusanyaji takataka, n.k. Hata huko mnakosema kumepimwa ni vumbi tu. Tazama Mbezi Beach, Sinza, n.k. Sehemu ambayo ni afadhali ni Oysterbay. Hata Masaki kuna barabara nyingi tu za vumbi na maji kwa ndoo/simtank.

Miji ya South Africa ipo vizuri kama ulaya. Lakini kwa vile miji yote imepimwa, basi viwanja na nyumba huwa ni vingi sana na bei hupungua sana. Vilevile wenzetu wanajenga kwa mikopo kuliko Tanzania ambako ni lazima udundulize au uibe. Ndiyo maana wewe unapoona hiyo nyumba unafikiria itakuwa Masaki ya South Africa.

Unapozungumzia slums South Africa kumbuka kuwa kwa vile South Africa kila kipande cha ardhi kina mwenyewe ambao wengi ni wazungu siyo rahisi kwa mtu wa kawaida sana, asiye na kazi ya maana kumiliki nyumba ya maana.

Ukitaka kujua bei za nyumba South Africa tembelea tovuti za Property Agents kama Seeff Properties na linganisha bei za hizo nyumba na bei ambayo ungeambiwa Tanzania. Kumbuka Rand 1 ni sawa na USD 14.

Nakupa tovuti ya Seeff Properties kwa maeneo ya Centurion. Kama unajua mitaa mingine badilisha unavyotaka:

Properties for sale in Centurion | Seeff Properties
Watu wengine wanapenda ligi na matusi, kiukweli SA nyumba bei ni rahisi kuliko Tz, nashangaa watu wanabisha vitu viko wazi. Kusema nyumba bei rahisi kule haina maana kwamba kumiliki nyumba kama hii ya Diamond ni rahisi kwa kila mtu. Ni rahisi kulinganisha na bei za ajabu za Tz.
 
Back
Top Bottom