PostGE2025 Picha: Polisi wampandisha mtuhumiwa kizimbani kusomewa mashtaka akiwa na BOKSA

PostGE2025 Picha: Polisi wampandisha mtuhumiwa kizimbani kusomewa mashtaka akiwa na BOKSA

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kijana huyu amesimama kizimbani akiwa na vest na boksa—baada ya kunyimwa hata ruhusa ya kupiga simu kuomba nguo za kubadilisha.

Ni miongoni mwa vijana walioshtakiwa pamoja na Niffer kwenye kesi ya uhaini. Taarifa zinaeleza kuwa Jeshi la Polisi lilimzuia kuwasiliana na familia yake, hata kwa dharura ya mavazi.

Leo, mbele ya Mahakama, amesomewa mashtaka akiwa katika hali isiyo ya heshima kwa utu wa binadamu.

Soma Zaidi: Wengine 95 wapandishwa Kisutu jioni hii kwa Mashtaka ya Uhaini, idadi yafikia watuhumiwa 291 nchi nzima

1762533652767.png
 
Vipi wale waliovunjiwa maduka, kuchomewa magari na kuibiwa mali zao, ilhali hawahusiki na huo ufuska semwa wa serikali? Je huo sio ukatili kwao?
 
Kijana huyu amesimama kizimbani akiwa na vest na boksa—baada ya kunyimwa hata ruhusa ya kupiga simu kuomba nguo za kubadilisha.

Ni miongoni mwa vijana walioshtakiwa pamoja na Niffer kwenye kesi ya uhaini. Taarifa zinaeleza kuwa Jeshi la Polisi lilimzuia kuwasiliana na familia yake, hata kwa dharura ya mavazi.

Leo, mbele ya Mahakama, amesomewa mashtaka akiwa katika hali isiyo ya heshima kwa utu wa binadamu.

Soma Zaidi: Wengine 95 wapandishwa Kisutu jioni hii kwa Mashtaka ya Uhaini, idadi yafikia watuhumiwa 291 nchi nzima

Huyu ndio yule mwenye majeraha ya kuchomwa na pasi mikononi?
 
Na hakimu anakubali mtuhumiwa asimame mbele ya mahakama akiwa amevaa hivyo. Shida inaanzia hapo.

Nimesikia kuna hakimu amekataa kupokea ripoti ya hospitali itakayothibitisha hali ya afya ya watuhumiwa waliopigwa wakiwa mikononi mwa polisi.

Si muda mrefu mahakamani nako kutakuwa sehemu ya kuonyesha kutoridhika na muelekeo wa nchi.
 
Hawa mashetani wahukumiwe haraka ili vijana wengine wa hovyo wajifunze.
Eti unamkata mwenzako vidole au kumchinja kisa kapiga kura.
Wamechoma moto vituo vya mafuta, maduka, ofisi za umma. Hawapaswi kuonewa huruma.
Mimi sijapiga kura but my lovely alipiga kura na wala hajamchagua mwana CCM. Kwahiyo huyu wangemdaka wangemkata vidole pia .
 
Inaonekana Magereza yamekua mengi sana hii nchi wanalimisha watu wa kuwawekamo
 
Back
Top Bottom