PICHA: Rais Samia na Peter S Greenberg wakiandaa Royal tour lakini hakuna 'social distancing'

Sioni tatizo lolote la hii picha. Nilienda Canada. Mke wa Waziri Mkuu aliomba kupiga picha nami. Aliyepiga picha ni mume wake. Nilikuwa na shaka kidogo, nikakipu distance, lakini mke wa Waziri mkuu alilalamika akiomba nimkumbatie. Nilishtuka kidogo, nikamtazama mumewe, yeye akafurahi na kuniambia, please do it. Nilimkumbatia, mumewe akapita picha. Tukapeana mikono kwa furaha kubwa.

Kwani kuwa Rais, ubinadamu wake umebadilika?

Tuangalie mambo makubwa. Tukosoa mambo makubwa, kama ya kubambikia watu kesi za ugaidi, siyo picha. Ningeshangaa kama angekuwa amepiga picha, labda akiwa nusu uchi, lakini siyo kwa hii picha.
 
Kwa huyu rais tumepigwa.

Hata kama ni drama avae basi uhusika.
Ajifunze kutoka kwa marais wanawake waliofanya vizuri kama yule wa Ujerumani au hata yule wa Liberia.

Uraisi ni taasisi, una heshima zake.
 
Hivi CCM mlikosa mtu wa kupendekeza kuwa makamu wa Rais,mkatuletea urojo kama huu,huyu alipaswa akaimbe taarabu kule kwao,ona sasa haya maajabu!
Acha kufoka mazee, iyo picha imepigwa lini ? Sidhani kama imepigwa akishakuwa raisi. Ukitaka urojo sema utapewa bure kwa wewe, makubaliano tuu. 😉
 
Kwa huyu rais tumepigwa.

Hata kama ni drama avae basi uhusika.
Ajifunze kutoka kwa marais wanawake waliofanya vizuri kama yule wa Ujerumani au hata yule wa Liberia.

Uraisi ni taasisi, una heshima zake.
 
Baada ya kupiga hiyo picha ikawekwa kwenye mtandao gani?

Huenda waliifuta/choma baada ya wewe kuondoka au wameiweka kwwnye kumbukumbu za kifamilia.

Tatizo hapa ni picha kama hii kuwa public.
 
Covid is real,
 
Hoja yako nzuri,Ila umeingiza ushabiki wa vyama,hapa tunajadili Kama watanzania,sio wanaccm Wala wanachadema,
 
Hebu tutajie nchi tatu ili tuone mafanikio yake
 
Hiyo ni photoshop
Kushikana hivyo kama mume daa
Kweli siasa mbaya sana
 
Du TUMEPIGWA hapa chai tupu waziri mkuu anaitwa nan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…