Picha: Rejeta yangu inamwaga maji kwa presha

Picha: Rejeta yangu inamwaga maji kwa presha

Hapo gadketi au
Wakuu Habari za weekend

Jana nimedrive gari Kwa umbali kama wa kilometres 2,

Nikafungua mfuniko wa rejeta, kilichotokea ni maji kuruka Kwa nguvu Sana kama video inavyoonyesha,

Maswali yangu ni kama ifuatavyo

1 shida ni Rejeta

2 shida ni engine

3 shida ni gasket

4 au shida ni feni zile za kupoza?

Haya maswali 4 ndio mafundi wamesema ndio tatizo kuna mmoja kanambia nishushe injini kabisa

Sasa naomba mawazo kidogo

Hii gari ni NISSANI TEANA 230JM

View attachment 2675046
View attachment 2675047
Hapo ni gasketi au Cylinder head imepinda
 
Umeunguza gasket. Peleka gereji wabadilishe gasket. Pia mwambie fundi apime rejeta kama ni nzima na pia apime mfuniko.

Kitu ambacho watu wengi hawajui ni kwamba.

Kila mara unapofanya service ya gari fanya nayafuatayo kulinda mfumo wa upoozaji.

Pima rejeta, pima mfuniko, safisha rejeta na badilisha coolant.
Kwa gari za siku hizi full aluminium alloys inaweza shida isiwe gasket pekee: head na blocks za aluminium huwa zinapinda zikiwa subjected kwa exess heat. Making them to be useless.
 
Back
Top Bottom