Ninakumbuka wajomba zangu wawili baada ya kupata mali za urithi kila mmoja alipata nyumba, yule Mmoja alianza kukodisha vyumba mpaka hii leo zaidi ya miaka 20 sasa maisha yake yamekua tegemezi hivyo. Yule mwengine aliuza nyumba ya kwanza akaanza kufanya biashara, Alilaumiwa sana na wanafamilia ila hakuwasikiliza, baada ya muda miaka kama mitatu mambo yakawa magumu biashara zilakwama akaamua kuuza na yapili, Kwa kweli jamii ilimuandama sana mpaka wakawa wanasema amerogwa, Ila jamaa hakurudi nyuma aliamini kwenye Biashara akiamini atafikia malengo yake. Hivi sasa jamaa ni MIlionea. Na yule kaka yake ambae aliekua anasambaza maneno kuwa jamaa amechanganyikiwa anauza nyumba sahivi kawa analalamika mitani kuwa Ndugu yake hamsaidii hali ya maisha ni ngumu.